CAIRO, Misri
TIMU ya taifa ya Tanzania imepangwa katika Kundi J
pamoja na Tunisia, Libya na Guinea ya Ikweta, katika mbio za kuwania kufuzu kwa
fainali zijazo za michuano ya Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Cameroon 2021.
Hilo limebainka baada ya Shirikisho la Soka la Afrika
(Caf) kupanga ratiba hiyo katika hafla iliyofanyika jijini hapa.
Katika kundi hilo la Tanzania na Tunisia ndizo pekee
zilikuwepo katika fainali za mwaka huu ambazo zinamalizika kesho jijini hapa, kwa
kuzikutanisha Algeria na Senegalm ambazo zote zimetoka katika Kundi C pamoja na Tanzania, huku Guinea ya Ikweta na Libya zilishindwa
kufuzu.
Tunisia wenyewe ilifungwa na Nigeria 1-0 jana katika
mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Afcon 2019 Misri wakati Tanzania ilifungwa
mechi zote tatu za Kundi C, ikiwa 2-0 na
Senegal, 3-2 na Kenya huku Algeria ikiichapa Stars 3-0.
Kenya iliyokuwa kundi moja na Tanzania kwenye fainali
za mwaka huu, yenyewe kwenye mbio za kusaka tiketi ya kwenda Cameroon 2021, imepangwa
Kundi G pamoja na wenyeji wa mwaka huu Misri, Togo na Comoro.
Uganda wamepangwa Kundi B pamoja na Burkina Faso,
Malawi na ama Sudan Kusini au Shelisheli, wakati Algeria imepangwa Kundi H
pamoja na Zambia, Zimbabwe na Botswana na Senegal ipo Kundi I pamoja na Kongo,
Guinea Bissau na Eswatini.
MAKUNDI
YOTE KUFUZU AFCON 2021 CAMEROON
Kundi
A:
Mali, Guinea, Namibia, Liberia/Chad
Kundi
B:
Burkina Faso, Uganda, Malawi, Sudan Kusini/Shelisheli
Kundi
C:
Ghana, Afrika Kusini, Sudan, Mauritius/Sao Tome
Kundi
D:
DRC, Gabon, Angola, Djibouti au Gambia
Kundi
E:
Morocco, Mauritania, CAR, Burundi
Kundi
F:
Cameroon, Cape Verde, Msumbiji, Rwanda
Kundi
G:
Misri, Kenya, Togo, Comoro
Kundi
H:
Algeria, Zambia, Zimbabwe, Botswana
Kundi
I:
Senegal, Congo, Guinea Bissau, Eswatini
Kundi
J:
Tunisia, Libya, Tanzania, Equatorial Guinea
Kundi
K:
Ivory Coast, Niger, Madagascar, Ethiopia
Kundi
L:
Nigeria, Benin, Sierra Leone, Lesotho
No comments:
Post a Comment