Diego Costa, mfungaji wa bao nne pekee wakati Real Madrid ikifungwa 7-3 na Atletico Madrid. |
NEW JERSEY, Marekani
DIEGO Costa alifunga mabao manne na alitolewa wakati Atletico
Madrid ikiisambaratisha Real Madrid kwa mabao 7-3 jijini hapa.
Costa alifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya
kwanza na kukamilisha hat-trick yake kwa bao la penalti alilofunga katika
dakika ya 45.
Joao Felix, mchezaji aliyesajiliwa katika kipindi
hiki cha majira ya joto kwa ada ya pauni
milioni 113, naye pia alifunga bao lake la kwanza katika klabu hiyo wakati Atletico
ikiongoza kwa mabao 5-0 hadi mapumziko.
Costa alingeza la nne dakika sita baada ya kuanza kwa
kipindi cha pili, kabla ya yeye na mchezaji wa Real Dani Carvajal hawajatolewa
kwa kadi nyekundu baada ya kupigana katika dakika ya 61.
Angel Correa, aliyeingi aakichukua nafasi ya majeruhi
Alvaro Morata, naye pia alizifumania nyavu katika kipindi cha kwanza, wakati Vitolo
alifunga bao la saba kwa Atletico katika dakika ya 70.
Real waliendelea kuwa nyuma kwa mabao 6-0 kabla Real Madrid
haijarekea katika ubao wa matangazo kwa mabao kupitia kwa Nacho, wakati Karim
Benzema na Javier Hernandez wote wakifunga mabao katika dakika za majeruhi.
Gareth Bale, ambaye anajiandaa kuondoka Real Madrid
na kujiunga klabu ya China ya Jiangsu Suning, alianzia katika benchi, lakini
aliingia katika dakika 30 za mwisho.
Real, ambayo ilitumia kiasi cha pauni milioni 300
katika kipindi cha majira ya joto, ilianza kusajili kwa kumsajili Eden Hazard na
Luka Jovic.
Lakini walipambana katika ziara yao ya Marekani kabla
ya kuanza kwa ligi, ambapo walifungwa 3-1 na Bayern Munich na kuifunga Arsenal kwa
penalti baada ya kutoka sare ya 2-2.
"Tulipoiangalia Madrid, tulikuwa tukiangalia
wapi tutaimaliza, “alisema kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone. "Tulikuwa
na muda mzuri hapa.”
Nahodha wa Real Sergio Ramos alisema: "Ni wazi
hatuikuwa tukijisikia vizuri hapa. Na huu ndio mwanzo wa maandalizi yetu, Kuna
njia nyingi zinazokufanya ushindwe, lakini hatuwezi kufanya kama tulivyofanya
leo.
Kocha wa Real Zinedine Zidane aliongeza: "Hatuna
haja ya kumtafuta mchawi katika hilo, hii ni mechi za maandalizi kabla ya
kuanza kwa msimu mpya.
No comments:
Post a Comment