GARETH Bale anakaribia kukamilisha uhamisho kutoka
Real Madrid kwenda katika klabu ya China ya Jiangsu Suning kwa mkataba wa miaka
mitatu utakaomuwezesha kuweka kibindoni mshahara wa pauni milioni 1 (sawa na sh
bilioni 3) kwa wiki.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales, yuko katika
hatua za mwisho za makubaliano na Jiangsu, ambao sasa wana uhakika wa
kukamilisha usajili wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.
Endapo mpango huo utakwenda vizuri, basi Bale atakuwa
amelamba dume kwa kupata karibu mara mbili ya mshahara wake wa pauni 600,000
kwa wiki ambao analipwa Real Madrid na atakuwa nyota mkubwa kujiunga na Ligi
Kuu ya China.
Klabu ya Beijing Guoan nayo pia imeulizia kutaka
kumsajili, lakini Jiangsu ndio inaonekana kushinda mbio hizo za kumpata
mchezaji huyo.
Lionel Messi ndiye mchezaji soka anayelipwa zaidi
duniani, ambapo kwa wiki anaondoka na karibu pauni milioni 1.7 katika
Barcelona, na mkataba wa Bale pale Jiangsu utamuwezesha kumkaribia mchezaji huyo wa
Barca.
Chanzo cha karibu kabisa na mchezaji huyo wazamani wa
Tottenham Hotspur kimeelezea ofa hiyo ya Jiangsu kama ni “isiyoelezeka”.
Bale alikuwa akijiandaa kung’ang’ania kubaki Real
Madrid, licha ya kocha Zinedine Zidane kuweka wazi kuwa anamtaka mchezaji huyo
kuondoka katika klabu hiyo, lakini taarifa zilizotolewa na Telegraph Sport, zinasema
mchezaji huyo yuko tayari kwenda China.
Chanzo kutoka Hispania kinadai kuwa Bale atasaini
mkataba wa miaka mitatu ndani ya saa kadhaa, ingawa marafiki wa mchezaji huyo
Ijumaa walisema mpango huo bado haujakamilika vizuri.
Zidane alimaliza kipindi cha Bale Real Madrid baad
aya mchezo wa kirafiki wa maandalizi uliofanyika Jumapili iliyopita dhidi ya Bayern
Munich aliposema:
“Hajamuhusisha mchezaji huyo katika kikosi chake wakati klabu
hiyo ikifanyia kazi suala la kuondoka kwake, na ndio maana hakucheza.
“Tutaangalia nini kitatokea katika siku zijazo.
Tunatakiwa kuangalia nini kitatokea kesho, endapo kitatokea, basi ni jambo
zuri. Acha tuwe na matumaini kwa faida ya kila mmoja, na hilo litatokea haraka
sana. Klabu inawasiliana na klabu nyingine…”
Wakala wa Bale, Jonathan Barnett aliendelea kusema
kuwa Zidane “amekywqa amuheshimu” mteja wake, lakini kocha huyo ameendelea
kusisitiza kuwa hali ya mshambuliaji hyo bado inabaki vile vile licha ya Marco
Asensio kuendelea kuwa majeruhi kwa muda mrefu.
Zidane pia aliendelea kumbania Bale, huku akiendelea
kuwa kimya bila kuelezea mcheaji huyo anataka nini.
Sasa inaonekana kipindi cha miaka sita cha Bale kukaa
Real kimekaribia kumalizika na kuiacha klabu hiyo aliyotwaa nayo mataji manne
ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na taji la La Liga.
Hiyo inamfanya Bale kuwa mwanasoka wa Uingereza
mwenye mafanikio zaidi anayecheza soka nje hasa pale aliponunuliwa kwa rekodi
ya ada ya pauni milioni 85 wakat akitua Real akitokea Tottenham mwaka 2013.
Dirisha la usajili China linatarajia kufungwa
Jumatano ijayo, lakini Bale anatarajia kuwa mchezaji wa Jiangsu katika kipindi
hicho na kuhamia kwake China kutamfanya kupata mapokezi ya kishujaa.
Kwa sasa Ezequiel Lavezzi ndiye mchezaji anayelipwa
zaidi China kwa anapewa pauni 500,000 kajubu mkataba wa Bale utafunika huo wa
Muargentina huyo.
No comments:
Post a Comment