Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice-Tanzania, Jacqueline Woiso akizungumza na waandishi wa habari wa wakati wa kutangazwa
rasmi kwa ushirika kati ya SportPesa na SuperSport ambapo SuperSport kupitia
DStv itarusha mubashara michuano hiyo itakayoanza wiki ijayo hapa jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji na Udhibiti wa SportPesa Tanzania
Tarimba Abas.
Na Mwandishi Wetu
KING’AMUZI cha DStv ndicho pekee kitaonesha mubashara
mashindano ya tatu ya SportPesa yatakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia
Januari 22 hadi 27 na kushindanisha timu za Tanzania na Kenya ili kumpata
mshindi atakayecheza na Everton, imeelezwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice-Tanzania, Jacqueline
Woiso alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa mashindano ya kombe hilo
yataoneshwa na DStv kupitia Super Sports, ambayo ndio iliyopata udhini ya
kuonesha mashindano hayo kama mshirika rasmi.
Mkurugenzi wa Uendeshaji na Udhibiti wa SportsPesa
Tarimba Abas (Katikati) akizungumza wakati wa kutangazwa rasmi kwa ushirika
kati ya SportPesa na SuperSport ambapo SuperSport kupitia DStv itarusha
mubashara michuano hiyo itakayoanza wiki ijayo hapa jijini Dar es Salaam. Kulia
ni Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice TanzaniaJacqueline Woiso na Mkuu wa
Uendeshaji Baraka Shelukindo (kushoto)
Mbali na vigogo vya soka Tanzania vya Simba na Yanga,
timu zingine zitakazoshiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Mbao FC pamoja
na Singida United za Tanzania wakati zile za Kenya ni Gor Mahia, AFC Leopard,
Bandari na Kariobangi.
Gor Mahia ndio washindi wa kihistoria baada ya
kulitwaa taji hilo mara mbili na kufanikiwa kucheza mara mbili dhidi ya Everton
inayoshiriki Ligi Kuu ya England.
Michuano hiyo itakuwa na mvuto wa aina yake kwani
mbali na ukubwa, umaarufu na utani wa timu shiriki, pia kila timu itataka
kutwaa kombe hili na hatimaye kupata fursa ya kucheza na moja ya timu maarufu
ya soka nchini Uingereza – Everton FC.
Mkurugenzi wa Uendeshaji na Udhibiti wa SportsPesa
Tarimba Abas (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Uendeshaji wa MultiChoice
Tanzania Baraka Shelukindo wakati wa hafla ya kutangazwa rasmi kwa ushirika
kati ya SportPesa na SuperSport ambapo SuperSport kupitia DStv itarusha
mubashara michuano hiyo itakayoanza wiki ijayo hapa jijini Dar es Salaam.
Woiso alisema
jana kuwa SuperSport kupitia DStv itarusha mubashara mashindano hayo
yatakayoanza wiki ijayo jijini Dar es Salaam.
“Tunafurahi
kuujulisha umma wa watanzania kuwa hamu yao ya kushuhudia michuano hii
mubashara kupitia DStv sasa imepatiwa jibu, sasa watashuhudia burudani hii ya
aina yake tena kuanzia kifurushi cha chini kabisa cha Bomba,” alisema Jacqueline.
“Michezo yote itaonekana kupitia DStv SuperSport 9, ambayo
inapatikana katika vifurushi vyote. Tumeamua kufanya hivyo ili kuwapa
watanzania fursa ya kushuhudia mashindano haya ambayo yanazidi kujipatia
umaarufu kila uchao”.
Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania
Jacqueline Woiso akimkabidhi mpira Mkurugenzi wa Uendeshaji na Udhibiti wa
SportsPesa Tarimba Abas muda mfupi baada ya kutangaza rasmi ushirika kati ya
SportPesa na SuperSport ambapo SuperSport kupitia DStv itarusha mubashara
michuano hiyo itakayoanza wiki ijayo hapa jijini Dar es Salaam.
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa
Tanzania, Tarimba Abbas amesema “Tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo miaka
mitatu iliyopita, mashindano haya yamekua moja ya mashindano makubwa na
yanayopendwa sana Afrika Mashariki yote.
Hili ni jambo kubwa sana kwani wachezaji wetu
wataweza kuonesha vipaji na viwango vyao na hivyo kuwatangaza kote duniani.
Natoa rai kwa timu zinazoshiriki kuhakikisha zinaonesha viwango vya juu kabisa kwani huu ni ulingo muhimu wa kuonesha
uwezo na ujuzi wao wa soka kwa timu husika lakini pia na kwa wachezaji,”
alisema Tarimba.
Mshindi wa Kombe la SportPesa 2019 atajishindia dola
za Marekani 30,000 pamoja na kucheza dhidi ya Everton, moja ya timu maarufu
kabisa za soka Uingereza wakati mshindi wa pili atapata dola za Marekani 10,000
wakati mshindi wa tatu atapata dola 7,500 na mshindi wa nne dola 5,000. Timu
zote zitakazo tolewa robo fainali zitapata dola 2,500 kila moja.
Michuano ya Kombe la SportPesa ilianza rasmi mwaka
2017 katika michuano iliyofanyika hapa Tanzania, ambapo mshindi – Gor Mahia
alicheza na Everton hapa hapa Tanzania. Msimu wa pili wa mashindano hayo
yalifanyika huko Nakuru Kenya mwaka jana, mshindi kwa mara ya pili Gor Mahia
alikwenda kucheza na Everton huko Liverpool Uingereza mwezi Novemba.
No comments:
Post a Comment