LONDON, England
KOCHA Mkuu wa Arsenal Unai Emery kumpanga mchezaji
mpya aliyesajiliwa juzi Denis Suarez (pichani) na kuichezea kwa mara ya kwanza katika Ligi
Kuu ya England dhidi ya Mabingwa wa ligi hiyo Manchester City katika mchezo
utakaofanyika kesho.
The Gunners wanasafiri hadi kwenye Uwanja wa Etihad kwa
ajili ya mchezo huo unaotarajia kuwa mkali na wa kusisimua baada ya kukamilika
kwa dirisha la usajili, ambapo klabu hiyo ilikamilisha usajili wa Suarez kwa
mkopo akitokea Barcelona hadi mwishoni mwa msimu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye
ameichezea mara mbili timu ya wakubwa ya Man City katika kipindi chake cha
mwanzo cha kuichezea klabu hiyo, ndio mchezaji pekee aliyetua Arsenal, ambaye
alishindikana kupata mkataba wa kudumu kutokana na ufinyu wa fungu.
Mkataba huo wa mkopo ni pamoja na kuwemo kipengele
cha kuweza kuongeza mkataba wa muda mrefu kwa Suarez katika kipindi cha majira
ya joto wakati mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania akihusishwa na kiujiunga
tena na Emery, wakati akicheza chini ya Mhispania mwenzake katika klabu ya
Sevilla.
"Nitafanya uamuzi kesho (leo) lakini endapo
ataanza katika mchezo huo nina imani naye, “alisema Emery alipouilizwa ikiwa Suarez
ataenda moja kwa moja katika timu ya Arsenal katika mchezo huo wa Jumapili.
"Namjua mchezaji huyo na alianza kujifua binafsi
juzi. Leo alikuwa na wenzake. Ni jambo zuri, anaonekana kuelewa haraka.
"Ni mchezaji mwenye kiwango na nafikiri anaweza
kutusaidia sisi kutokana na kiwango chake…, “alisema.
Ushindi kwa Manchester City utashuhudia timu hiyo
ikiwakaribia vinara wa ligi hiyo Liverpool kwa pointi mbili, ambao watacheza
dhidi ya West Ham siku moja baadae.
Kikosi cha Pep Guardiola alikuwa mpinzani wa kwanza
wa Emery katika soka la Uingereza, ambako waliibuka na ushindi wa mabao 2-0
dhidi ya Arsenal Agosti.
Emery anatarajia kukutana na kikwazo kingine lakini
alisema wachezaji wake wako tayari kuonesha uwezo wao dhidi ya wapinzani
wazuri.
"Itakuwa mechi ngumu, tunacheza dhidi ya timu
bora, “alisema.
"Sasa, Liverpool, wamefanya kazi kubwa sana
wakati wa Ligi Kuu msimu huu. Labda wamepoteza baadhi ya mechi., lakini hiyo ni
kama ajali tu.
No comments:
Post a Comment