Mwandishi Wetu, Dodoma
KATIBU
Mkuu Kiongozi, ambaye pia ni Mkuu wa Utumishi wa Umma, Balozi Mhandisi John
Kijazi amewaagiza Makatibu Wakuu kuhimiza michezo mahala pa kazi kwa vitendo ili
kuwa na watumishi wa Umma wenye afya njema.
Kauli
hiyo ilitolewa leo na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), Maimuna
Tarishi kwa niaba ya Balozi Kijazi katika Bonanza la Michezo lililoandaliwa
na Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu
wa Mikoa (SHIMIWI), na kufanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Tarishi ameweka msisitizo kwa kuwa michezo ni kazi na kazi ni michezo, ambapo
sasa Makatibu Wakuu waweke mazingira yatakayowezesha watumishi wa umma kupitia
taasisi zao waweze kushiriki kwenye michezo mbalimbali, ambayo inajenga umoja
na ushirikiano baina ya watumishi.
Washiriki wa bonanza la Shirikisho
la Michezo Wizara, Idara, Taasisi, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa
Mikoa (SHIMIWI), wakifanya mazoezi ya viungo wakiongizwa na Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu (Bunge), Bi. Maimuna Tarishi (watano kulia mstari wa mbele) jana
kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
“Haya
ni maagizo ya Katibu mkuu kiongozi amenituma nije niseme kwa kuwa yupo katika
kazi nyingine, wito ni kwa Makatibu Wakuu wote na wakuu wa taasisi kuhakikisha
wanaweka mazingira wezeshi yatakayowezesha watumishi kufanya mazoezi mara kwa mara
na hata katika michezo kama hii ya Shimiwi,” amesema Bi. Tarishi.
Amesema
sasa uwekwe utaratibu kwa Watumishi wa Umma kushiriki michezo ambayo haitatumia
gharama kama wanavyodhania wengine.
“Kwa waajiri hatuna budi kuweka mazingira
wezeshi ya kuwawezesha Watumishi kuwa na utaratibu wa kushiriki kwenye michezo
yeyote na hii inafanyika bila gharama yeyote kabisa kwani wakati mwingine
tunakimbilia hatuna fedha au hajatenga kifungu katika bajeti wakati hata hapa
ukiangalia hakuna gharama kubwa iliyotumika,” amesisitiza Bi. Tarishi.
Amewataka watumishi wa umma kufanya mazoezi ya kila wakati ili kujiweka
katika afya kwa wakati wote, ambayo itawasaidia kufanya kazi kwa weledi.
Bi.
Tarishi ametoa pia maagizo kwa viongozi wa Shimiwi, kwa kuwa sasa wameanza kufufua
michezo hii baada ya kusimama kwa muda mrefu, na sasa waendelee mbele kwani yanawakutanisha
Watumishi wa maeneo mbalimbali ya kazi ya serikali na husaidia kubadilishana
uzoefu.
“Hii
ni rai yangu kwenu kwa kuwa sasa mmeanza tena michezo yenu hii tunapenda tuone
inasonga mbele kwani hushirikisha watumishi kutoka Wizara na Taasisi
mbalimbali, na yanajenga umoja kama watumishi wa umma, na tuwekee maanani na
kutekeleza haya,” amesema Bi. Tarishi.
Hatahivyo,
amesema michezo ni nidhamu hivyo kuwe na nidhamu kwenye michezo kwani
kutasaidia watumishi kufanya kazi kwa bidii na kuwa na ubinifu wa hali ya juu.
Naye
Mwenyekiti wa Shimiwi, Daniel Mwalusamba amesema wachezaji wanahimizwa
kufanya mazoezi kwa ajili ya kujenga, kulinda na kuimarisha afya zao.
“Michezo
ni kazi hivyo wanapaswa kuzingatia taratibu na miongozo inayokuwa imetolewa
kila wakati na serikali, na kama agenda ya kitaifa ilivyo ya kujenga Tanzania
ya Viwanda, na ili tufanikiwe tunahitaji kuwa na Watumishi wenye afya bora
wanaoweza kufanya majukumu yao kwa wakati na kushiriki michezo mbalimbali,
ambapo sasa wanaweza kuandaa mabonanza sehemu za kazi kwa siku ya za mwishoni
mwa wiki,” amesema Bw. Mwalusamba.
Hatahivyo,
amesema katika kikao cha juzi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hazina na kuwahusisha
Wenyeviti na Makatibu wa klabu za michezo mahala pa kazi, ambapo wamekumbushwa
kusimamia michezo kwa kuwa ni sehemu ya kazi na wanapaswa kusimamia na kutekeleza
majukumu yote yanayotolewa na serikali.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma, Bi. Bertha Bankwa (wa kwanza kulia mstari wa nyuma) leo akijumuika kufanya mazoezi na watumishi wa Umma katika bonanza la Shirikisho la Michezo Wizara, Idara, Taasisi, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), lililofunguliwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), Bi. Maimuna Tarishi (Hayupo pichani). (PICHA NA BAHATI MOLLEL WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA- TAA). |
Katika
michezo iliyochezwa jana kwa upande wa kuvuta Kamba wanaume timu ya Waziri Mkuu
wametoa jasho na Mambo ya Ndani na kutoka sare ya mvuto 1-1; wakati katika
netiboli timu ya Utumishi imechapwa na Tamisemi magoli 24-17; huku Afya
wakiwashinda GST magoli 9-6.
Katika
mchezo wa soka Utumishi wamewachapa Afya magoli 2-0; huku Ardhi wamewashinda
Mwanasheria Mkuu kwa magoli 4-0.
No comments:
Post a Comment