Makamu wa Kwanza wa Rais Utawala wa Riadha Tanzania (RT), William Kalaghe akifungua mafunzo ya siku mbili ya walimu wa mchezo huo watakaowafundisha makocha wa riadha katika shule za msingi nchini. |
Na Mwandishi Wetu
WASHIRIKI wa mafunzo ya riadha kwa watoto wametakiwa kupokea kwa makini
mafunzo hayo ili nao wakawafundishe walimu wa shule za msingi ili kuwa na
msingi imara wa mchezo huo na kuiwezesha Tanzania kupata wanariadha bora kama
huko nyuma.
Hayo yalisemwa jana na Makamu wa Kwanza wa Rais Utawala wa Riadha
Tanzania (RT), William Kalaghe wakati akifungua mafunzo hayo Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi
wa mafunzo ya walimu wa walimu watakaofundisha wanafunzi wa shule za
msingi nchini katika mchezo wa riadha, Dk. Hamad Ndee.
|
Kalaghe alisema kuwa, mafunzo hayo ni muhimu kwao, kwani wataweza
kuwafundisha walimu wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika
kuuendeleza mchezo huo.
Alisema bila kuwa na msingi imara kamwe Tanzania haitaweza kurejea katika
mafanikio ya mchezo huo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma wanariadha wake
walipofanya vizuri.
Aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kupokea kwa makini, kwani huo ndio
msingi imara wa Tanzania kufanya vizuri katika mchezo huo.
Naye mkufunzi wa mafunzo hayo, Dk Hamad Ndee alisema kuwa hakuna msingi
imara katika mchezo fulani bila kufundisha watoto wadogo.
Alisema hata akina Usain Bolt walianzia utotoni na kutokana na msingi
imara walioupata, sasa wanatamba duniani kwa kufanya vizuri katika mchezo huo.
Mmoja wa washiriki wa mchezo hyo kutoka mkoani Mbeya, Lwiza John alisema
mafunzo hayo yatawasaidia kuwafudisha walimu wa watoto wadogo katika mikoa
watokayo.
John ambaye pia ni mmoja wa makocha wa timu ya taifa yam bio za nyika ya
Tanzania inayojiandaa kwa mashindano ya dunia wiki ijayo nchini Uganda alisema
mafanikio ya kila mchezo yanaanzia chini kabisa.
Jumla ya washiriki 29 wanashiriki katika mafunzo hayo kutoka mikoa
mbalimbali huku sita wakitoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yatafungwa leo na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mkufunzi Dk. Hamad Ndee leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment