Wachezaji, viongozi na benchi la ufundi la timu ya taifa ya Tanzania, Taifa wakiwa katika picha ya pamoja. |
NA Mwandishi Wetu
TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo
inaikaribisha Misri katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika
(Afcon) zitakazofanyika Gabon mwakani, katika mchezo utakaofanyika kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ni wa Kundi G, huku Nigeria ambayo
nayo iko katika kundi hilo ikiwa tayari imeiaga michuano hiyo na Chad ilijitoa
mapema na kufanya zibaki timu tatu katika kundi hilo badala ya nne.
Katika mchezo wa leo, Taifa Stars inahitaji
ushindi ili kufufua matumaini ya kucheza fainali za Afcon mwakani.
Tanzania inashika mkia katika Kundi G, baada
ya kucheza mechi mbili, ikifungwa moja ugenini na Misri 3-0 na kutoa suluhu na
Nigeria nyumbani.
Misri inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi saba baada ya kucheza mechi tatu sawa na
Nigeria yenye pointi mbili.
Zote, Misri na Nigeria zimebakiza mchezo
mmoja mmoja, wakati Tanzania ina faida ya mechi mbili – kwanza hiyo ya kesho dhidi ya Misri na baadaye
Septemba watacheza dhidi ya Nigeria, ambayo tayari imeshatolewa.
Iwapo Tanzania itashinda mechi zote mbili za
mwisho watamaliza na pointi saba sawa na Misri, hivyo timu ya kufuzu kutoka
Kundi G, itapatikana kwa uwiano wa mabao.
Misri wanahitaji sare tu katika mchezo huo wa
kesho ili kujihakikishia nafasi ya kutinga fainali hizo za Afcon, huku Stars
ikiombea Misri wafungwe kesho ili kurejesha matumaini hayo ya Taifa Stars
kufuzu kwa mara ya kwanza kucheza fainali tangu walipofanya hivyo kwa mara ya
mwisho mwaka 1980 nchini Nigeria.
Ukiangalia katika msimamo wa kundi G, Misri
inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi saba, ikifuatiwa na Nigeria ambao wana
pointi mbili huku Taifa Stars ikiwa na moja.
Lakini Stars ina faida ya kuweza kuzifikia
pointi za Misri kutokana na kubakisha michezo miwili, tofauti na wenzake ambao
wamebakisha mechi moja moja.
Kocha wa timu ya Taifa, Boniface Mkwasa
akizugnumzia mchezo huo alisema “ Mchezo utakuwa mgumu, hii ni naweza kusema ni fainali, sisi tunahitaji
matokeo mazuri zaidi, tunahitaji kushinda magoli si chini ya manne ili tufufue
matumiani ya kufuzu, lakini ukiangalia wenzetu Misri wanataka sare ili
iwavushe.”
Kikosi kamili cha Mkwasa kitakachoivaa Misri ni makipa; Deogratius Munishi ‘Dida’ (Yanga SC), Aishi Manula
(Azam FC), Beno Kakolanya (Prisons FC). Mabeki; Aggrey Morris (Azam FC), Erasto Nyoni
(Azam FC), David Mwantika (Azam FC), Juma Abdul (Yanga SC), Mwinyi Hajji
Mngwali (Yanga SC), Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC) na Andrew Vicent (Mtibwa Sugar).
No comments:
Post a Comment