Mwenyekiti,
Chama cha “Sailing” Tanzania (TSAA)
Makamu Mwenyekiti Chama cha “Sailing” Tanzania (TSAA)
Waratibu wa Mafunzo, TOC/TSAA
Mkufunzi wa Kimataifa,
Washiriki wa Mafunzo,
Waandishi wa Vyombo vya Habari
Wageni waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
Kwanza
napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru TSAA kwa jitihada walizofanya kupata
mafunzo haya ya kwanza ya aina yake.
Pamoja
na kwamba mchezo huu ni mpya hapa Tanzania mtakubaliana nami kwamba siyo mpya
kwa Watanzania kwani mara nyingi tumeona wavuvi wakienda kuvua samaki wakiweka
matanga kwenye vyombo vyao vya kusafiria kwenda baharini.
Nimefahamishwa
matanga katika vyombo hivyo ni kwa ajili ya kutafuta mwelekeo na kasi ya chombo.
Nimefahamishwa
vile vile kwamba siku 11 zilizopita mafunzo haya yalipoanza rasmi pale DYC yalihudhuriwa
na washiriki 12 kutoka Dar Es Salaam,
Zanzibar, Pwani na Tanga, Washiriki hao ndio wanaomaliza leo kwa sura ya
furaha.
Nikiwa
kama mtendaji mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, idadi ya washiriki 12 ni
ndogo sana nikilinganisha na mafunzo ya aina hii kwa walimu wa michezo mingine
tuliyowahi kuandaa.
Pamoja
na uchache wenu ni matumaini yangu kuwa mmepata dozi nzuri ya taaluma na mbinu
mbalimbali ya kufundisha mchezo huu. TOC inauthamini sana mchezo wa “Sailing” pamoja na kuwa mpya hapa nchini na
ukitawaliwa zaidi na vijana wa wageni hasa panapotokea mashindano ya Kimataifa.
Kwa
kuwa mchezo huu ni mpya, kwa kweli unahitaji kuenezwa nchi nzima pale miundo
mbinu inaporuhusu (bahari na ma-ziwa “lakes”) kwani TOC inaamini kuwa mchezo huu ni kati
ya michezo ambayo inapendwa na itazidi
kupendwa na Watanzania pamoja na changamoto ya maeneo rasmi ya TSAA kufanyia
mazoezi na mashindano badala ya kutegemea vilabu binafsi ambavyo wakati
mwingine vinakuwa na masharti magumu.
Upatikanaji
wa vifaa (boats) nimefahamishwa ni changamoto kubwa kwa viongozi wa TSAA kwani
hata vikipatikana bado ni ghali ambapo watanzania hawawezi kuvimudu.
Ninawasihi
na kuwashauri viongozi wa TSAA kuwa karibu na Shirikisho la Kimataifa cha
mchezo huu (ISAF) na Mtaalamu Rob Holden ambaye ndiye mhusika mkuu wa maendeleo
ya mchezo wa “Sailing” katika bara letu la Afrika.
Ninaamini
mmefaidika na elimu mliopata kutoka kwa mtaalamu wa Kimataifa Rob Holden ambaye
amekuwa wakiwaandalia masomo yote ya nadharia na vitendo kwa muda wote wa siku
11. Ni mategemeo yangu elimu mliyopata itawasaidia kuandaa timu katika vilabu
vyenu sambamba na kuwa wabunifu wa kutengeneza au kutumia vifaa (boats) za
kawaida bila kutegemea tu za kisasa ambazo hatuwezi kumudu kuzinunua.
Ni
ukweli usiopingika kwamba mmejiongezea
elimu ya kufundisha mchezo huu wa “saiing” kwa kiwango cha hali ya juu, mkilinganisha
uwezo na elimu mliyokuwa nayo awali.
Wakati
wote TOC imekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza taaluma ya ufundishaji na
mbinu za kisasa za kuboresha uwezo wa walimu na wachezaji wetu, ili waweze
kufikia viwango vinavyotakiwa na timu zetu zinaposhindana katika mashindano
mbalimbali ya Kimataifa.
Ningependa
kusisitizia sana kwenu walimu mnaomaliza mafunzo haya, kwamba mhakikishe mchezo
huu wa “sailing”
unapiga hatua kufikia kiwango ambacho wenzetu kama Afrika ya Kusini,
Tunisia, Algeria, Morocco wanayo.
Ningependa
kuwasihi walimu mnaomaliza mafunzo haya leo kuupeleka mchezo huu kwa wavuvi
ambao nina uhakika mkiwashirikisha na kuandaa mashindano ya mara kwa mara kwa
kushirikiana na TSAA mtapata washiriki wengi ambao inawezekana kabisa kuna siku
watakuwa wawakilishi wazuri katika michezo ya Kimataifa na kuachana na zana
kwamba washiriki wengi wa mchezo huu hapa Tanzania ni wageni kutoka nje ya
nchi.
Ni
matumaini yangu Wizara inayoshughulikia michezo hapa Tanzania imetayarisha
mipango kwa kushirikiana na vyama vya michezo kuendeleza michezo ya aina yote
ikiwa pamoja na “Sailing”. Kilio
kikubwa cha vyama/mashirikisho ya michezo ikiwa pamoja na TSAA kwa sasa ni eneo
maeneo ya mazoezi na mashindano. Ili kuondokana na masharti magumu wanayowekewa
na vilabu vyenye maeneo hayo. hususan “sailing”, ninaomba Serikali kutenga maeneo ya michezo hususani
kwa TSAA kwani pamoja na ISAF kuweka nguvu nyingi katika kutoa elimu kwa walimu
wetu bado TSAA inahitaji kumiliki eneo lake la bahari kwa ajili ya mafunzo,
mazoezi na mashindano.
Mchezo
huu bado haujatangazwa vizuri, na wanaoweza kuutangaza zaidi ni waandishi wa
habari ambao tuko nao hapa leo, tofauti na baadhi yao kukataliwa kufanya “coverage”
hivi karibuni baada ya kuombwa na TSAA.
Linalotakiwa
hivi sasa ndugu zangu walimu ni kutumia mafunzo haya katika kuendeleza mchezo
wa “sailing” nchini.
Napenda
nichukue nafasi hii kumpongeza na kumshukuru mtaalamu wa Kimatafa Rob Holden kwa
jitihada zake za kutoa mafunzo haya kwa ufanisi mkubwa, kwa sasa tuna walimu
ambao watatufundishia wanamichezo wetu wazalendo, lakini bila vifaa mafunzo
haya hayatakuwa na tija kwa TSAA.
Nitakuwa
mchoyo wa fadhila kama sitawashukuru waratibu wa TOC.TSAA kwa kufanikisha mafunzo
haya, Olimpiki Solidariti (OS) kwa kufadhili mafunzo haya, Shirikisho la
Kimataifa la “Sailing” (ISAF) kwa kumteua Mkufunzi niliyemtaja hapo juu kuendesha
mafunzo, TOC na TSAA kwa maandalizi mazuri.
Mwisho
kabisa nawashukuru wale wote waliohusika katika kufanikisha mafunzo haya kwa
namna moja au nyingine.
Kwa
haya machache sasa natamka kwamba mafunzo yenu ya ualimu wa mchezo wa “Sailing”
ninayafunga rasmi.
Ahsanteni kwa
kunisikiliza.
No comments:
Post a Comment