Ndege ya air Zimbabwe ikitua kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) baada ya miaka saba tangu ilipotua mara ya mwisho kwenye uwanaja huo. |
Na Mwandishi Wetu
USHIRIKIANO wa Tanzania na Zimbabwe katika utalii utaongezeka zaidi
baada ya ndege ya Air Zimbabwe kurejesha tena safari za kuja nchini baada ya
kuacha kuja kwa takribani miaka saba sasa.
Kwa mara ya mwisho ndege ya nchi hiyo ilikuja nchini mwaka 2009
huku ile ya Tanzania, Air Tanzania ilitua katika ardhi ya Zimbabwe kwa mara ya
mwisho mwaka 2004, ikiwa ni miaka 12 sasa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa
Faustine Kamuzora aliyemuwakilisha waziri wa wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa
aliipongeza Air Zimbabwe kwa kuanza tena safari zake huku ikiinua sekta ya
utalii.
Alisema ndege hiyo itasaidia wanaotaka kutembelea vivutio vya
utalii kama Maporomoko ya Victoria, Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro na Zimbawe
sasa wataweza kusafiri moja kwa moja kati ya nchi hizo mbili.
Ndege hiyo itakuwa inakuja nchini mara mbili kwa wiki, Jumanne na
Jumamosi.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa
Kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere (JNIA),Waziri wa Uchukuzi, Maendeleo ya
Miundombinu wa Zimbabwe, Dr Jorum Gumbo alisema kuanza tena safari za ndege
hiyo kutasaidia sana kukuza utalii na kuinua uchumi wan chi hiyo.
Kikundi cha Utamaduni cha Jeshi la Kujenga taifa (JKT) kikicheza ngoma wakati wa kuikaribisha ndege ya Air Zimbabwe kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. |
Alisema watalii wanaokuja Tanzania na Zanzibar sasa watakuwa na nafasi
ya kwenda moja kwa moja Zimbabwe kwa kutumia ndege, tofauti na huko nyuma
iliwabidi kupitia nchi zingine, kitu ambacho ni gharama kubwa.
Baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wa Zimbabwe wakishuhudia ndege ya nchi yao ilipozindua safari zake za kuja Tanzania juzi kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. |
Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Edzai Absalom Chimonyo alisema
kumekuwa ndege hiyo itasaidia sana kusafirish watalii, wafanyabiashara na watu
wa kawaida kusafiri kati ya nchi hizo mbili kwa shughuli mbalimbali.
Alisema Wazimbabwe wamekuwa wakitumia sana bandari ya Dar es
Salaam, ambapo mbali na shughuli zingine, pia wamekuwa wakiingiza magari zaidi
ya 300 kwa mwezi kupitia bandari hiyo.
"Karibu magari 300 yamekuwa yakichukuliwa kutoka bandari ya Dar es Salaam na kupelekwa Zimbabwe kila mwezi, “alisema akionesha umuhimu wa Air Zimbabwe kurejesha tena safari zake nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment