Sunday, 16 April 2017

Savio yaendelea kuchanja mbuga, ABC ikiidadabua Don Bosco 73-50 Ligi ya Kikapu RBA Dar es Salaam


Na Mwandishi Wetu

SAVIO imeendelea kuongoza katika Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam ya RBA inayoendelea kushika kasi.

Baada ya mechi za jana kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, ambapo ABC iliifunga Don Bosco kwa pointi 73-50 huku Oilers wakiitambia Chui kwa pointi 68-50, Savio wako kileleni kwa kujikusanyia jumla ya pointi 22.

Vijana au City Bulls wenyewe wako katika nafasi ya pili kwa pointi 21 huku Ukonga Kids wakifuatia katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 19 huku JKT wakiangukia katika nafasi ya nne.

Wakongwe Pazi wenyewe wako katika nafasi ya tano baada ya kujikusanyia poiti 17, Kurasini nao wana pointi 17 lakini wako katika nafasi ya sita, Mabibo Bullet wenyewe wako katika nafasi ya saba.

Mkurugenzi wa Ufundi na Mashindano wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam, Halleluya Kavalambi alisema kuwa ABC, Jogoo, UDSM Outsiders na Olilers wanashika nafasi ya nane hadi 10.

Wakati huohuo, Kavalambi alisema kuwa viporo vya baadhi ya mechi vitapigwa Jumatano, ambapo ABC watacheza na Tanzania Prisons saa 10:00 Jioni, huku Jogoo wataoneshana kazi na Mgulani kuanzia saa 12 jioni na Pazi atakwaruzana na Chui kuanzia sasa 2 usiku.

23 waunda timu ya taifa ya riadha ya vijana

Wachezaji wakike na kiume wanaounda timu ya taifa ya vijana ya Tanzania Bara wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Mwandishi Wetu
RIADHA Tanzania (RT) imetangaza majina 23 kwa ajili ya kuunda timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya Kanda ya Tano ya Afrika yatakayofanyika jijini Dar es Salaam mapema mwezi ujao.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa RT, Whilhem Gidabuday, timu hiyo itapiga kambi katika hosteli za Filbert Bayi zilizoko Mkuza Kibaha kuanzia Jumanne chini ya makocha Robert Kalyahe na Mwinga Mwanjala.
Timu hiyo inaundwa na wachezaji 12 wavulana wakatu wasichana katika timu hiyo wako 11 ma watashiriki katika michezo yam bio za meta 100, 200, 400, 800, 1500 na 3000 pamoja na miruko na mitupo.
Gidabuday alisema kuwa kambi hiyo itagharimu kiasi cha sh Milioni 20 kuanzia timu hiyo itakapokuwa kambini kwa karibu siku 20, wakati wa mashindano na huduma zingine.
Mbali na wenyeji Tanzania Bara, nchini zingine zitakazoshiriki ni pamoja na Zanzibar, Uganda, Kenya, Rwanda, Sudan, Sudan Kusini, Ethiopia, Eritrea na Djibout.
Timu hiyo ilichaguliwa jana mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya wazi ya taifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa na kuhudhuriwa na mikoa michache.
Baadhi ya wanariadha walioshiriki walitoka katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Arusha na Manyara, ambapo shule ya Filbert Bayi iliyopo mkoani Pwani, imeto wachezaji watano katika timu ya wasichana kutokana na umahiri wao.
Ukiondoa baadhi ya kasoro zilizokuwepo ikiwemo kutokuwa na huduma ya kwanza wala gari la wagonjwa, wachezaji wakishiriki bila ya kuwa na namba za kuwatambua na kuleta ugumu kwa waandishi wa habari kujua nani ni nani, mashindano yalienda vizuri.











Simba yamaliza mechi Kanda ya Ziwa kwa suluhu


Na Mwandishi Wetu, Mwanza
SIMBA ya Dar es Salaam imekamilisha mechi zake za Kanda ya Ziwa kwa kuondoka na pointi saba baada ya jana kushindwa kuifunga Toto Africans katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.
Pointi hizo saba ilizopata Simba ni baada ya kupewa zile tatu za mezani walizopewa na Kamati ya Saa 72 baada ya Wekundu hao wa Msimbazi kukata rufaa kupinga Kagera Sugar kumchezesha kumchezesha Mohamed Fakhi aliyekuwa na kadi tatu za njano.
Kwa matokeo ya mchezo dhidi ya Toto Africans, Simba wana pointi 62 huku ikishinda 3-2 katika mchezo wake wa kwanza Mwanza dhidi ya Mabao FC kwenye uwanja huo huo.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, timu hizo zilikuwa suluhu licha ya kushambuliana kwa zamu kila moja ikisaka bao la kuongoza.

Simba ndio walikuwa wa kwanza kulifikia lango la Toto Africans katika dakika ya pili, lakini Shiza Kichuya alishindwa kufunga, alipaisha juu ya goli.

Dakika ya 37, Hamimu Abdul alipiga mpira katika lango la Simba, lakini James Agyei akaicheza.

Kocha wa Simba, Joseph Omog alifanya mabadiliko kadhaa akiwatoa kiungo Mohammed Ibrahim na mshambuliaji Laudit Mavugo na kuwaingiza Mwinyi Kazimoto na mshambuliaji Ibrahim Hajib.

Pamoja na mabadiliko hayo, mchezo uliendelea kuwa mgumu na Omog akaamua kumtoa na winga Shiza Kichuya na kumuingiza mshambuliaji Juma Luizio, wakati kocha wa Toto, Furgence Novatus alimtoa Jamal Mtengeta na kumuingiza Hamad Nathaniel Mbumba.

Kosa kosa ziliendelea huku Simba wakilishambulia zaidi lango la wapinzani wao, lakini walishindwa kupata bao na kulazimishwa suluhu.

Yanga ambayo haikushuka dimbani katika Ligi Kuu, wenyewe walicheza Algeria katika mchezo wa mchujo wa kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Afrika.

Friday, 14 April 2017

VURUGU ZA MASHABIKI ZACHELEWESHA KUANZA PAMBANO LA LYON NA Besiktas

LYON, Ufaransa
VURUGU jukwaani zilisababisha baadhi ya mashabiki kukimbilia sehemu ya kuchezea na kuchelewesha kuanza kwa mchezo wa kwanza wa robo fainali wa Ligi ya Ulaya kati ya Lyon na Besiktas.

Hatahivyo, wenyeji ndio walikuja kuibuka na ushindi wa bao 2-1 katika mchezo huo.
Vurugu zilitokea na kusababisha polisi kuingilia kati nje ya uwanja kabla ya kuibukia nyuma ya goli ambako wachezaji walikuwa wakipasha.

"Vitu ukiwemo moto vilirushwa kutoka jukwaani nakusababisha baadhi ya wapenzi kuwa wakimbizi kwa muda uwanjani ili kuokoa maisha yao, “ Lyon walitweete.

Mchezo huo ulianza baada ya dakika 45 huku Lyon ikifunga mara mbili katika dakika 10 za mwisho nan aibuka na ushindi wa mabao 2-1.


Mamlaka walitenaga maeneo yenye riski kubwa, ambapo askari 500 walimwagwa kwenye Uwanja wa Parc Olympique Lyonnais ikiwa ni zaidi ya idadi ya kawaida.

Mourinho aponda kiwango cha wachezaji wake baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Anderlecht

BRUSSELS, Ubelgiji
KOCHA wa Manchester United Jose Mourinho amekilaumu kikosi chake kwa washambuliaji `kuchemka’ baada ya Anderlecht kufanikiwa kuifunga bao la kusawazisha katika mchezo wa kwanza wa robo fainali Ligi ya Ulaya.

Man United ilikuwa mbele kwa bao 1-0 katika mchezo huo uliopigwa nchini Ubelgiji hadi pale katika dakika ya 86 wakati wenyeji waliposawazisha baada ya kulifikia lango hilo mara moja.
“Kama ningekuwa beki wa Manchester United ningeshangazwa sana na washambuliaji, “alisema Mourinho.

Henrikh Mkhitaryan alipata nafasi nzuri ya kuifungia Manchester United katika dakika ya 36, lakini hayo ndio yalikuwa mafanikio mazuri zaidi katika mashuti 16 yatimu hiyo waliyopiga kwa mpinzani wake.

Wageni wako pointi nne nyuma ya wapinzani wao Man City waliopo katika nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi Kuu ya England,ambapo wamefunga mabao 46.

Chelsea, Tottenham, Liverpool, Manchester City na  Arsenal wote kila mmoja tayari imefunga mabao zaidi ya 60.

Zlatan Ibrahimovic ndiye mchezaji anayeongoza kwa kufunga mabao katika timu hiyo baada ya kufunga mabao 28 katika mashindano yote, lakini Mkhitaryan na Juan Mata wanamfikia endapo ukilinganisha mabao yao yote.

"Ni matatizo hay ohayo, “aliongeza Mourinho. "Tulitawala mchezo, na tulipata nafasi, lakini tlishindwa kufunga mabao ya kutosha.


"Katika lugha yangu dhaifu ya Kiingereza neno zuri la kusema sio zaidi ya kuchemka. Tunatakiwa kuwa makini

Uchukuzi Sports Club watamba kutoa kichapo kwa kila watakayekutana naye Mei Mosi Moshi

Wachezaji wa timu ya Uchukuzi Sports Club wa timu ya Kuvuta Kamba wakijifua kwa ajili ya mashindano ya Mei Mosi.
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Uchukuzi Sports imetamba kutetea mataji yake na kuongeza mengine katika mashindano ya Mei Mosi yatakayofanyika kuanzia wiki ijayo mjini Moshi.

Katibu wa Michezo wa Uchukuzi Sports Club, Alex Temba alisema juzi wakati wa mazoezi ya timu hiyo kuwa, wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanatetea mataji waliyonayo na kuongeza mengine.
Timu ya soka ya Uchukuzi wakati wa mapumziko walipocheza jana dhidi ya Kitunda FC na kutoka sare ya bila kufungana.
Akifafanua, Temba alisema kuwa Uchukuzi Sports ndio mabingwa wa jumla wa mashindano hayo ya wafanyakazi, ambao waliutwaa mwaka jana mjini Dodoma na kukabidhia Kombe na Rais Dk John Pombe Magufuli.

Alisema wanakwenda Moshi kutetea mataji ya soka, kuvuta kamba kwa wanawake na wanaume, mbio ndefu kwa wanaume na wanawake, baiskeli kwa pande zote mbili pamoja na michezo ya jadi ya bao, karata na drafti.
Timu ya netiboli wakijfua.
Alisema kuwa maandalizi yao ambayo walianza muda mrefu, yanaendelea vizuri na wanatarajia kuondoka wiki ijayo kwenda Moshi tayari kwa mashindano hayo.

Timu ya Uchukuzi Sports inaundwa na wachezaji kutoka taasisi zilizochini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Naye nahodha wa timu hiyo, Toba Ally alisema kuwa hawana wasiwasi, kwani wana uhakika maandalizi yao mazuri kuwanyoa wapinzani wao katika michezo yote.


Alisema mwaka jana walitwaa vikombe vitano, lakini mwaka huu watabeba mataji zaidi, kwani maandalizi yao ndio yanawafanya kujiamini kiasi hicho.

Ndondi wajichuja Michezo ya Jumuiya ya Madola Gold Coast, Australia 2018 kutokana na ukata

Kocha wa timu ya taifa, Mzonge Hassan akifuatilia  mazoezi ya mabondia wa timu hiyo kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa.

Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Ngumi Tanzania (BFT) huenda likashindwa kupeleka mabondia katika Michezo ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika Gold Coast mwakani kutokana na ukata, imeelezwa.

Akizungumza jana Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema kuwa wahawa uhakika wa kupeleka mabondia katika mashindano ya ndondi ya Afrika yatakayofanyika Brazzaville, Congo kuanzia Mei 27 hadi Juni 4.

Alisema kuwa wanakabiliwa na ukata, hivyo hawatapeleka mabondia katika mashindano hayo na hivyo kushindwa kufuzukwa mashindano ya dunia yatakayofanyika Hamburg, Ujerumani Agosti 25 hadi Septemba 3 mwaka huu.

Endapo watashindwa kufuzu kushiriki mashindano ya dunia, moja kwa moja mabondia wa Tanzania hawatakuwa na vigezo vya kushiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola pamoja na ile ya Olimpiki Japan 2020.

Mashaga alisema wamekata tamaa ya kusaka fedha, kwani kila wanakopiga hodi wanaambiwa kuwa hakuna fedha licha ya kupeleka maombi mapema.

Alipoulizwa kama anajua kuwa kushindwa kupeleka timu katika mashindano ya Afrika pamoja ya yale ya dunia kama kutawafanya kushindwa kupeleka timu katika Jumuiya ya Madola na Olimpiki, Mashaga alisema analijua hilo vizuri.

Juzi Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi alisema kuwa ngumi hawana viwango vya kushiriki Jumuiya ya Madola, lakini lazima kwanza washiriki mashindano ya Dunia.
Alisema mchezaji hataruhusiwa kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola kama hajashiriki mashindano ya dunia ya mchezo wake.


Timu ya ndondi ilishindwa kushiriki michezo iliyopita ya Olimpiki iliyofanyika Rio de Janeiro, Brazil mwaka jana baada ya mabondia wake kutoshiriki mashindano ya dunia.

Arsenal yavunja benki kumbakisha Alexis Sanchez sasa atalipwa sh Milioni 838 kwa wiki

LONDON, England
KLABU ya Arsenal hatimaye imeufyata baada ya kuamua kuvunja benki na kuahidi kumlipa Alexis Sanchez kiasi cha pauni 300,000 (sawa na sh Milioni 838) kama mshahara wa mchezaji huyo kwa wiki.

Gazeti la Standard Sport lilibainisha Desemba kuwa, mchezaji huyo mwenye uimri wa miaka 28, alikuwa akitikisa kiberiti ili alipwe mshahara mnono kama ule wa Mfaransa wa Manchester United, Paul Pogba wa pauni 290,000 (sawa na sh Milioni 810) kwa wiki.

Habari zilizopatikana kutoka Arsenal zinasema kuwa kwa sasa the Gunners imeonesha dalili za kutaka kutoa kiasi hicho cha fedha ili kumbakisha mchezaji huyo katika klabu hiyo.

Manchester City, Chelsea na Paris St Germain wanatarajia kuweka mezani ofa kwa ajili ya kumtaka mchezaji huyo mwishoni mwa msimu huku Arsenal ikitaka ilipwe kiasi cha pauni Milioni 50 kama itashindwa kufikia makubaliano na mchezaji huyo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile katika wiki za hivi karibuni amechanganyikiwa zaidi wakati Arsenal ikipoteza mechi saba kati ya 12 katika mashindano yote huku mashabiki wakimtaka kocha Arsene Wenger kuachia ngazi mara moja mwishoni mwa msimu.


Mesut Ozil ndiye anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kwa sasa Arsenal akiweka kibindoni kiasi cha pauni 140,000 — Sanchez anapata pauni 130,000 — lakini klabu inajua madhara ya kuwapoteza wachezaji bora kwa wapinzani wao wakubwa.

Saturday, 8 April 2017

Wanafunzi shule ya Filbert Bayi wakonga nyoyo wakati wa kukipokea Kifimbo cha malkia jijini Dar es Salaam leo



Wanafunzi wa shule ya msingi ya Filbert Bayi wakiwa katika picha ya pamoja na wakimbiza Kifimbo cha Malkia mara kilipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyererea (JNA) eneo la VIP leo.
Na Mwandishi Wetu

KIFIMBO cha Malkia wa Uingereza kimetua jijini Dar es Salaam leo huku wanafunzi wa shule ya Msini ya Filbert Bayi waking'ara na ngoma yao ya Mganda wakati wa kukipokea kifimbo hicho kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere  (JNIA).
Kifimbo hich kesho kitakimbizwa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Ikulu, ambako litapokewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Wanafunzi hao wa shule ya Filbert Bayi walikonganyoyo za wakimbiza kifimbo hicho pamoja na wageni waalikwa waliofika uwanjani hapo kukipokea, ambapo walichenua kwa `atep zao bila kukosea, mbali na mavazi yao meupe na vitambaa vyekundu vichwani mwao.
Ndege ya Kenya Airways ndiyo iliyokibeba Kifimbo hicho kutoka Kenya na kupokewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na watu mbalimbali wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Coke na Balozi wa Australia nchini Kenya, John Feakes.

Kifimbo hicho kilipotua nchini kilibebwa na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Michezo ya Jumuiya ya Madola Afrika, Gideon Sam pamoja na Rais wa TOC, Gulam Rashid na kuingia nacho katika jengo la kuwasilia na kuondokea abiria maarufu la VIP la JNIA.

 Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akizungumza kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) leo. Kushoto ni Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Coke na Rais wa TOC, Gulan Rashid.
Akizungumza uwanjani hapo Sam alisema kuwa kifimbo hicho ni ishara ya kukaribia kufanyika kwa Michezo ya 21 ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika Gold Coast, Australia Aprili mwakani.

Alisema kifimbo hicho kimetokea Kenya, ambao walikipokea kutoka nchini Nigeria.

Naye Feakes  alisema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuelimisha kuhusu kifimbo hicho, ambacho kinakimbizwa kila kabla ya michezo inayokuja ya Jumuiya ya Madola.

Rais wa TOC, Rashid alisema wanafurahi kukipokea kifimbo hicho , ambapo kesho watakikimbiza hadi Ikulu.

Bayi akitaja ratiba ya kifimbo hicho kesho asubuhi kitaanzia Azam TV kabla ya kwenda katika daraja la Nyerere na baadae kwenye Uwanja wa Taifa, ambako kutakuwa na shughuli mbalimbali zikiwemo za burudani kutoka African Stars `Twanga Pepeta’, JKT, Polisi na vikundi vingine, kabla ya kuanza mbio kwenda Ikulu.

Kifimbo hicho jioni kitakwenda Arusha katika shule ya St Judy na baadae kurudi jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Filbert Bayi wakicheza ngoma ya Mganda ya Manda mkoani Ruvuma wakati wa kukipokea Kifimbo cha Malkia ya Uingereza leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere, JNIA.
 

Wednesday, 22 March 2017

Kamati ya Bunge ya Miundombinu yataka fedha za TB III zitolewe kwa wakati


Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dk.Leonard Chamriho akitoa taarifa fupi ya wizara kuhusiana na ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea kuona ujenzi wa jengo hilo.
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeitaka serikali kuhakikisha inatoa kwa wakati fedha za mradi wa ujenzi wa Mradi wa jengo la tatu la abiria (TB III) la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, ili mradi huo uweze kukamilika Disemba 2017 kama ilivyopangwa.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Norman Sigalla alitoa kauli hiyo leo wakati wa kufanya majumuisho baada ya kutembelea na kuona maendeleo ya ujenzi huo, ambapo ukikamilika jengo hilo litakuwa na uwezo wa kupokeo abiria milioni 6 kwa mwaka.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB), Mhandisi Prof. Ninatubu Lema akielezea masuala mbalimbali ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipofanya ziara kwenye jengo hilo linaloendelea kujengwa na linatarajiwa kumalizika Desemba 2017.
Prof. Sigalla alisema kukamilika kwa jengo hilo kwa wakati utapunguza msongamano wa abiria ambao sasa wanahudumiwa kwenye jengo la pili la abiria la JNIA (TBII).

 uliopangwa utawapa heshima Watanzania lakini pia kupunguza msongamano katika jengo la sasa la Terminal II.
“Ninawapongeza sana ten asana kwa ujenzi wa jengo hili ikimalizika ninaimani kubwa litatupa heshima kubwa, hivyo ili likamilike kwa haraka tunaiomba serikali yetu itoe fedha kwa wakati kwani tumeona ndio moja ya changamoto zilizozungumziwa hapa,” alisema Prof. Sigalla.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi akisoma taarifa ya mradi wa jengo la tatu la abiria (TBIII), kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, ilipofanya ziara kuangalia maendeleo ya ujenzi huo.
Aliongeza kuwa … “pato la taifa litaongezeka kwa ndege nyingi za nje na kubwa zitakapokuja kutua kwenye kiwanja chetu,”.

Awali wakati akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa jengo hilo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi alisema, changamoto kubwa inayowakumba ni serikali kuchekewa kutoa fedha.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Prof. Norman Sigalla akiwaeleza jambo wajumbe wa kamati hiyo, wakati wakitembelea jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Prof. Norman Sigalla akiwaeleza jambo wajumbe wa kamati hiyo, wakati wakitembelea jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Bw. Msangi alisema changamoto nyingine ni sheria ya Mamlaka ya Mapato (TRA) ya kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ilipitishwa mwaka 2015, awali kabla ya sheria hiyo kupitishwa vifaa vya ujenzi wa jingo hilo vilikuwa na msamaha wa kodi, lakini baada ya kupitishwa msamaha huo uliondolewa na kusababisha baadhi ya vifaa kukaa kwa muda mrefu bandarini baada ya kuzuiwa.

Alisema kutokana na changamoto hiyo ya kuchelewa kwa fedha na vifaa kukwama bandarini, kumesababisha mradi huo uliokuwa umepangwa awali kumalizika Agosti 2016 kushindwa kukamilika kwa wakati na sasa unatarajiwa kukamilika Disemba 2017. 

Mhandisi Mwanaidi Mkwizu aliyenyoosha kidole kuwaonesha wajumbe wakati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, majenereta ya kisasa yaliyofungwa kwa ajili ya matumizi ya jengo la tatu la abiria (TBIII) la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, walipofanya ziara. Kushoto ni Prof. Anna Tibaijuka.
“Tunaiomba serikali itusaidie upatikanaji wa fedha hizi za mradi kwani hii ni moja ya changamoto kubwa inayotishia kuendelea kwa ujenzi huu,” alisema Bw. Msangi.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dk Leonard Chamriho alieleza juu ya notisi iliyotolewa na Mhandisi Mshauri ya kutaka kusitisha huduma kuanzia leo (Jumatano) hadi atakapiliwa fedha anazodai.

“Tayari serikali imeanza kufanyia kazi deni hili na sasa ipo kwenye hatua nzuri ya kuhakiki nyaraka za malipo kabla ya kumlipa,” alisema.

 

 IMETOLEWA NA BAHATI MOLLEL, OFISA UHUSIANO MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA).