Monday, 14 May 2018

TAA Yawapiga Msasa Wanausalama Wake



Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Joseph Nyehende (aliyesimama) akifungua kozi ya Usalama wa vifurushi na mizigo iliyoanza leo kwenye Chuo cha Usafiri wa Anga kilichopo Jengo la Kwanza la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBI). (kulia) ni Bw. Sunday Mweemba wa Zambia na (kushoto) ni Bw. Ernest Bongane wa Afrika Kusini, ambao ni wakufunzi. (Picha Zote na Bahati Mollel wa TAA).

 Na Bahati Mollel, TAA
WANAUSALAMA 18 kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wametakiwa kuzingatia mafunzo ya Usalama wa vifurushi na mizigo vinavyosafirishwa kwa ndege za mizigo, yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Chuo cha Usafiri wa Anga kilichopo kwenye jengo la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBI) Jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Joseph Nyahende, ambapo amesema kuwa, mafunzo hayo yatasaidia zaidi kuongeza uelewa wa vifurushi na mizigo hiyo inatakiwa kusafirishwa bila abiria kuambatana nao.
Mkufunzi Sunday Mweemba kutoka Zambia akieleza jambo baada ya kozi ya Usalama wa Vifurushi na Mizigo kufunguliwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Joseph Nyehende (katikati), kushoto ni mkufunzi mwingine Bw. Ernest Bongane wa Afrika ya Kusini. Kozi hiyo itamalizika Mei 18, 2018. 
“Tunania njema ya kuwatengeneza wanausalama wetu na hili darasa ni muhimu sana kwa ajili yenu, hivyo tunahitaji mjifunze kwa faida yenu binafsi, taasisi na taifa kwa ujumla, kwani hamtaweza kuruhusu vitu visivyostahili kupita, kwani mtakuwa sasa mmepata mafunzo ya kuvitambua,” alisema Bw. Nyahende.

Naye mmoja wa wakufunzi Bw. Sunday Mweemba kutoka Zambia ameishukuru Menejimenti ya TAA ya kuomba kozi hiyo kupitia taasisis ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (ICAO), ambayo itawafanya wanausalama wake kutambua vitu vingi vinavyofanyika katika viwanja vingine Duniani.
 Kaimu Meneja wa Usalama wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Julius Misollow (aliyeipa kamera mgongo) akifafanua jambo mbele ya washiriki wa kozi ya mafunzo ya usalama wa vifurushi na mizigo inayosafirishwa na ndege za mizigo iliyoanza leo kwenye Chuo cha Usafiri wa Anga kilichopo kwenye Jengo la Kwanza la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBI). 
“Tumeona ni jinsi gani menejimenti yenu ilivyojitoa kwa ajili yenu, na hii inatolewa na ICAO na kupitia kazi yenu mnatakiwa kuwa makini zaidi na kuzijua sheria zote zinazohusika na mizigo, na tunamatumaini hadi mwisho mtakuwa mmeweza kujijengea uwezo,” alisema Bw. Mweemba.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Usalama wa Viwanja vya Ndege Tanzania, Bw. Julius Misollow alisema mafunzo hayo ni ya kwanza, ambayo yanalengo la kuwajengea uwezo wanausalama kukagua vifurushi na mizigo inayosafirishwa yenyewe bila abiria kwa kutumia ndege za mizigo.
Mkufunzi Bw. Ernest Bongane wa Afrika ya Kusini akisalimiana na washiriki wa kozi ya usalama wa vifurushi na mizigo inayosafirishwa na ndege za mizigo iliyoanza leo kwenye Chuo cha Usafiri wa Anga kilichopo jengo la Kwanza la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBI). 
“Magaidi wamekuwa wakitumia njia mbalimbali na wengine wanatumia mizigo au vifurushi kufanya hujuma, hivyo tunaimani kwa mafunzo haya tutawajengea uwezo wa kutambua mizigo, ambayo ni hatarishi, ingawa kwa Tanzania haijawahi kutokea tatizo hilo,” alisema Bw. Misollow.

Hata hivyo, amesema mafunzo hayo yatakuwa na mitihani na watakaofaulu kwa alama 70 wataendelea na kozi ya ukufunzi, ambayo itaanza baadaye kuanzia Mei 19, 2018.
Washiriki, Wakufunzi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Joseph Nyahende (wa pili kushoto waliokaa) wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya usalama wa vifurushi na mizigo inayosafiri kwa ndege za mizigo iliyoanza leo kwenye Chuo cha Usafiri wa Anga kilichopo kwenye jengo la Kwanza la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBI). 
Washiriki wanaoshiriki na viwanja wanavyotoka ni pamoja na Philbert Lyimo, Ahmed Zomboko, Thawabu Njeni, Rehema Mlanzi, Nuhu Kisweswe, Martha Kilunga, Levina Valasa, Josephine Kahimba, Anna Myovela, Fatma Shomari na Stephen Ntambi (JNIA); Zalia Msangi na Stephen Magambo (Arusha).

Wengine ni   Mathias Gombo, Lilian Malero na Wenceslaus Sango (Mwanza); Bebedict Ole Laput (Songwe); na Felister Lutonja (Shinyanga).

Sunday, 13 May 2018

Ngorongoro Heroes Yajiweka Pabaya Afcon 2019


Na Mwandishi Wetu
PAMOJA na kufungwa mabao 2-1 na Mali, timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes bado inaweza kusonga mbele katika kufuzu kwa mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa umri huo, Afcon endapo itachanga vizuri karata zao katika mchezo wa marudiano.

Baada ya kufungwa 2-1 katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili wa kufuzu kwa Afcon leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Ngorongoro Heroes sasa inahitaji ushindi wa angalau mabao 2-0 ili kusonga mbele.

Timu hiyo iliitoa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa penalti 6-5 baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaama na baadae kupata matokeo kama hayo nchini Congo kabla ya kwenda katika matuta.

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, umeifanya Ngorongoro kuwa na kibarua kigumu katika mchezo wa marudinao kwani sasa inahitaji ushindi wa kuanzia mabao 2-0 ili kusonga mbele katika hatua inayofuata.

Mchezo huo ambao uliokuwa na ufundi mkubwa kwa timu zote mbili, timu ya Mali ilikuwa ya kwanza kuandika bao kupitia kwa kiungo Ousmane Diakite.

Wakati Ngorongoro ikicheza kwa juhudi zote kutafuta bao la kusawazisha,ndipo nshambuliaji Dianka wa Mali alipoipatia timu yake bao la pili kunako dakika ya 40.

Ngorongoro iliamka na kuanza kucheza kwa kasi ikitafuta bao,hata hivyo juhudi hizo zilianza kuzaa matunda baada ya mshambuliaji Paul Peter kufunga bao la kufutia machozi na kurudisha matumaini kwa Watanzania.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu na kujilinda zaidi ambapo mpaka dakika 90 zinamalizika matokeo yalibaki kwa Ngorongoro kupoteza kwa idadi hiyo ya mabao.

Liverpool Yashinda 4-0, Chelsea Yachapwa 3-0 EPL

Mohamed Salah

LONDON, England
MSIMU wa mwaka 2017/18 wa Ligi Kuu ya England ulimalizika jana kwa kishindi huku timu zingine zikicheka na zingine kulia kutokana na matokeo waliyoyapata.

Livepool ilitoka meno nne baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion, huku Chelsea ikipokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa New Castle United.

Ushindi huo umeifanya Liverpool kukata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu ujao, huku Chelsea akiikosa nafasi hiyo na kuambulia ile ya Ligi ya Ulaya msimu ujao.

Katika mchezo mwingine uliofanyika kwenye Uwanja wa Liberty, Swansea City ilijikuta ikilambwa mabao 2-1 dhidi ya Stoke City, huku Crystal Palace ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya West Brom.

Katike mchezo mwingine, kwenye Uwanja wa Turf Moor, Burnley ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa AFC Bournemouth huku Huddersfield Town ikichapwa 1-0 dhidi ya Arsenal na Manchester United wakiikandamiza Watford kwa bao 1-0.

Kwenye Uwanja wa St. Mary, Southampton ilichapwa bao 1-0 na mabingwa wapya Manchester City, ambao walifikisha bao la 100 na kuweka historia huku Tottenham Hotspur ikishinda 5-4 dhidi ya Leicester City.

Yanga Mwaka wa Kukosa, Yachapwa na Mtibwa


Na Mwandishi Wetu
UPEPO mbaya umeendelea kuikumba klabu ya Yanga,baada ya leo na kupoteza mchezo mwingine wa Ligi Kuu Bara baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri,Morogoro.

Mchezo huo unakuwa ni watatu mfululizo kwa timu hiyo kupoteza, ikiwa kwenye viwanja tofauti baada ya ule wa Simba uliofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na Tanzania Prison, uliofanyika Mbeya.

Katika mchezo huo ambao timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu, huku Mtibwa ikijlinda zaidi kuepuka kupoteza mchezo huo.

Yanga ilijitahidi kufanya mashambulizi ya kushtukiza. lakini umakini mdogo wa washambuliaji, Yohana Nkomola na Matheo Anthony ulifanya mchezo huo kwenda mapumziko ukiwa sare ya bila kufungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa Mtibwa kushambulia kwa mpira mirefu ambayo hata hivyo ilizimwa vizuri na walinzi wa pembeni Juma Abdul na Salum Hassan.

Dakika ya 62  ilifanya mabadiliko ya kumtoa Juma Abdul ambaye aliumia na kuingia Yusufu Suleiman, ambaye hata hivyo alionekana kuwa na uzoefu mdogo wa Ligi.

Yanga ilicharuka na kuanza kupeleka mashambulizi kwa kutumia mipira mirefu, ambayo dakika ya 65 nusura wapate bao baada ya Thaban Kamusoko kugongesha mwamba, kabla ya dakika nne baadaye Matheo Anthony kufanya hivyo pia.

Mtibwa ilionekana kudhamiria kuifunga Yanga,baada ya kufanya mabadiliko ya kumtoa Salum Kihimbwa na kuingia Haruna Chanongo ambaye alibadilisha taswira nzima ya mchezo huo kwa timu yake.

Wakati mchezo ukielekea ukingoni kiungo Thabani Kamusoko alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Festo Simon, ambapo dakika moja baadaye mchezaji Hassan Dilunga aliipatia Mtibwa bao ambalo lilidumu hadi dakika 90 ya mchezo.

Baada ya mchezo huo, Yanga itaingia kambini kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports utakaopigwa Mei 16 wiki hii, kwenye dimba la Taifa,Dar es Ssalaa.

Kwa matokeo hayo, Yanga imendelea kushika nafasi ya tatu kwa pointi 48, ikiwa nyuma ya Azam FC wenye pointi 52.

Yanga katika mchezo wa kwanza wa makundi wa Kombe la Shirikisho, ilifungwa mabao 4-0 na Alger Usm ya Algeria.


Wataalam Wawasilisha Usanifu wa Awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, Dodoma

  Wahandisi Kamel Fazhani (kulia) na Marrarchi Walis (kushoto) wa Kampuni ya Studi ya Tunisia wakiwasilisha usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma leo katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), mbele ya wadau mbalimbali wa masuala ya usafiri wa anga. (Picha na Bahati Mollel wa TAA).
Meneja Mipango na Usanifu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mohamed Millanga (wa kwanza kushoto), akiangalia moja ya picha (hazionekani pichani) za usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliowasilishwa leo na Wahandisi Marrarchi Walis na Kamel Fazhani wa Kampuni ya Studi ya Tunisia kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo uliudhuriwa na wataalam mbalimbali wa usafiri wa anga. (Picha: Bahati Mollel – TAA).
Mhandisi Bernard Kavishe (aliyesimama) wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), akichangia hoja katika mkutano uliofanyika leo wa uwasilishaji wa usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo umewasilishwa na wataalam kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia. 
 Bw. Said Mpwili wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) (nyuma aliyenyanyua mkono), akiwasilisha mapendekezo ya ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege kwa wataalam kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia, ambao leo katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wamewasilisha usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma. (Picha na Bahati Mollel wa TAA).

Mwonekano wa Jengo la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliowasilishwa leo katika usanifu wa awali kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na wataalamu kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia.

Wednesday, 9 May 2018

Dar es Salaam Charity Goat Races Will Continue 2018

PRESS RELEASE

Dar es Salaam, 09th April 2018

The popular Charity Goat Races in Dar es Salaam will continue. After last year’s announcement by the former organizing committee to discontinue the popular charity and family event the Rotary Club of Dar es Salaam Oysterbay decided to carry on with the organization of the races in future. The new organizers will keep the structure of the event, but hope to attract new fans in addition to existing goat race enthusiasts.
The Rotary Goat Races Board Chairman, Amish Shah speaks to reporters in Dar es Salaam today during a media briefing to announce the club’s intention to continue with the organization of the Goat Races in 2018. Left is President of Rotary Club Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels  and the head of Goat Races Organizing Committee, Mathew Helela (right).
In the past 17 years the Dar es Salaam Charity Goat Races were a staple in the annual event-calendar and one of the premier charity events in the city. The decision by the former organizing committee not to continue with the organization of the event left many fans disappointed. After intensive discussions with the predecessors, the Rotary Club of Dar es Salaam (DSM) Oysterbay decided to carry on with the races. Under the new brand “The Rotary Goat Races” this year’s event will take place on June 23rd at the Green in Oysterbay banking on the previous assets of the races: a fun family-event with proceeds going to charitable projects.

Other than in the past, however, the proceeds of the Rotary Goat Races will not be given to various charity organizations but are going to be used for own service projects of the Rotary Club of DSM Oysterbay. 

Those projects will focus primarily on different aspects of education benefitting the local community. “Rotary International and its member clubs have the reputation of very efficiently carrying out projects via its member volunteers, directing almost one hundred percent of project funds to the beneficiaries”, said current President of Rotary Club DSM Oysterbay, Anne Saels. “We believe that with the planned education projects we can make a huge difference in the lives of the people in our community and we are happy that the Rotary Goat Races will play an important role in this”.

The Rotary Goat Races Board Chairman, Amish Shah, is convinced that the Rotary Goat Races 2018 will not disappoint. “With the Motto ‘Wakanda Goat Are You’, we give reminiscence of the year’s most successful movie ‘Black Panther’, hoping to attract new fans and previous Goat Race enthusiast likewise”. As in previous years, says Shah, the Rotary Goat Races 2018 were able to attract large sponsors such as Toyota, Swiss International Airlines and Coca Cola. “We are thankful for the trust in our organizational capacity that our sponsors have given us and we are confident that the Rotary Goat Races 2018 will be a fun event for everyone”.

The Rotary Club of DSM Oysterbay was founded in 2009 and has currently about 70 members. It is the largest of the eight Rotary Clubs in Dar es Salaam and supports the community with a wide range of projects including a Community Health Initiative that organizes biannual medical camps in rural and urban Tanzania, the Vijana Poa project to help young university students find employment, the Rotary Dar Marathon to assist the work of CCBRT-Hospital, and Rotary Mission Green, a district effort to plant trees. Furthermore, the Rotary Club of Oyster Bay is currently building various Rotary Community Corps in order to deliver direct community support to beneficiaries.
For media enquiries:
·         Angelika El-Noshokaty (The Rotary Goat Races PR-Committee)​
angelika@el-noshokaty.com,  +255689619930
·         Abdulrahman Hussein (2018 Organizing Committee)
akhussein@gmail.com, +255 715 361 300
·         Mathew Hellela (2018 Organizing Committee)
mhellela@gmail.com, +255 758 178 850

Rotary Club Kuandaa Mbio za Mbuzi 2018

Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza dhumuni la klabu hiyo kuendeleza mashindano ya mbio za mbuzi kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya mbio za mbuzi,  Amish Shah.
Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya mbio za mbuzi mwaka huu yanatarajia kufanyika Juni 23 kwenye viwanja vya The Green Oysterbay jijini Dar esSalaam,imeelezwa.

Mbio hizo zinafanyika chini ya muandaaji mpya, ambaye ni Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oysterbay baada ya muandaaji wa awali kusitisha shughuli hiyo baada ya kuiandaa kwa takribani miaka 17.
Methew Hellela; Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Mbio za Mbuzi 2018 akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya mbio hizo leo. Kushoto ni Rais wa Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saeels na kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Mbio za Mbuzi, Amish Shah.
Rais wa Rotary Dar es Salaam Oysterbay, Anne Saeels  alisema jana kuwa, waandaaji wapya wataendelea na utaratibu ule ule wa kuendesha mashindano hayo kama ilivyokuwa huko nyuma.

Alisema kuwa tofauti na miaka ya nyuma, mapato yote yatakayotokana na mashindano ya mwaka huu, hayatapelekwa katika mashirika mbalimbali yanayopokea misaada na badala yake fedha hizo zitatumika kwa ajili ya miradi binafsi ya hutoaji huduma ya klabu ya Rotary Dar es Salaam Oysterbay.
Mjumbe wa Bodi ya Mbio za Mbuzi za Rotary 2018, Amish Shah akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu mbio hizo. Kushoto ni Rais wa Rotary Dar es Salaam, Oysterbay Anne Saels na kulia ni Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Methew Hellela.
Alisema miradi hiyo itazingatia hasa masuala mbalimbali ya elimu kwa manufaa ya jamii.

“Tunaamini kwamba kupitia miradi ya elimu iliyopangwa tunaweza kuleta tofauti kubwa kwenye maisha ya watu katika jamii na tunafuraha mashindano yam bio za mbuzi ya Rotary yatakuwa na jukumu katika kukamilisha hili, “alisema Saels.

Naye mwenyekiti wa Bodi ya Mbio za Mbuzi za Rotary, Amish Shah alisema kuwa anaamini mashindano hayo yatakuwa mazuri sana na hayatawaangusha mashabiki, ambapo anaamini yatavutia mashabiki wengi.
Rais wa Rotary Club Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels akifurahia jambo na mwenyekiti wa Bodi ya Mbio za Mbuzi 2018, Amish Shah wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. 
Alisema kuwa mashindano hayo mwaka huu yamedhaminiwa na Coca Cola, Toyota na Swiss International Airlines.

Alisema kuwa ni matarajio yao kuwa huo ni mwanzo na anaamini kuwa kila mwaka watajitahidi kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika tena kwa ufanisi wa hali ya juu na kuvutia watu wengi.
Mwenyekiti wa Bodi ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza mbio hizo zitakazofanyika Juni 23. Katikati ni Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels na Mkuu wa Kamati ya Maandalizi, Abdulrahman Hussein .

Friday, 4 May 2018

NMB Yakabidhi Jeshi Vifaa vya Michezo vya Mil 10


Mlezi wa timu za Jeshi, Luten Kanal, David Mziray akipokea vifaa vua michezo kutoka kwa Meneja Mwandamizi wa NMB, Mahususi kwa wateja, Gibson  Mlaseko kwa ajili ya michezo ya Mkuu wa Majeshi itakayofanyika jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB leo imetoa vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 10 kwa timu za Majeshi, ambazo zinajiandaa na mashindano ya Majeshi yanayotarajia kuanza Mei 8 hadi 20, mwaka huu kwenye viwanja vya Uhuru na Twalipo Jijini Dar es Salaam.

Michezo mbalimbali ikiwemo soka, netiboli, riadha, ngumi, kulenga shaba, mpira wa mikono inatarajiwa kuwepo na washindi watazawadiwa zawadi mbalimbali.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhia vifaa hivyo Makao Makuu ya Meneja Mwandamizi na mahusiano kwa wateja wa NMB, Gibson Mlaseko alisema kuwa sababu ya kutoa msaada huo ni kutokana na mahusiano mazuri waliyokuwa nayo na JWTZ, katika mambo ya michezo.

“Nashukuru kwa mahusiano mazuri kati yetu na JWTZ kwani hii ni mara ya tatu tunasaidiana nao katika maswala mbalimbali ya michezo, pia lengo la msaada huu ni kutambua umuhimu wa michezo kuwa ni kuibua vipaji kujenga Afya na ajira hivyo tuna imani wenzetu watavitumia vifaa hivi vizuri na kufikia malengo,” alisema Mlaseko.

Kwa upande wake, Luteni Kanali David Mziray aliishukuru NMB, kwa msaada huo na kusema watahakikisha wanavitumia vizuri ili kutimiza malengo ambayo wamejiwekea katika mashindano hayo.

“Tunawashukuru NMB kwa msaada huu vifaa hivi vitaongeza chachu ya mashindano yetu ambayo hufanyika kila mwaka tunaomba na kampuni zingine ziige mfano wao ili kuinua michezo nchini,” alisema Mziray.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mipira ya michezo yote, Jezi za michezo yote, michezo mingine ambayo itashindaniwa katika michuano hiyo ambayo hufanyika kila mwaka.

Tuesday, 1 May 2018

Serena Williams Kupanda Chati Wimbledon 2018


NEW YORK, Marekani
BINGWA mara saba Serena Williams bado anaweza kuwa namba moja katika mashindano ya Wimbledon mwaka huu, hata kama Mmarekani huyo hajarejea ndani ya nafasi 32 bora duniani kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.

Williams, 36, aliporomoka kwa viwango hadi kufikia nafasi ya 449 duniani tangu alipojifungua mwaka jana.

Anaamini wachezaji wanaotoka kujifungua wanatakiwa kulindwa katika upangaji wa ratiba pamoja nakulindwa katika viwango.

Richard Lewis, mtendaji mkuu wa klabu ziote za England, alisema kuwa huo ni “uamuzi mkubwa”.

Lewis alisema kuwa anfikiri hilo klitatokea kwa Williams kwani anaweza kupangwa katika mashindano hayo, licha ya kuwa nje ya 32 bora, mashindano hayo yataanza Julai 2.

Hatahivyo, klabu baadae ilitoa taarifa kuwa ni ubaguzi kuwapanga wachezaji katika mashindano kwa kuzingatia viwango vyao.

Mkutano wa upangaji ratiba unatarajia kufanyika Juni 26.

Williams, ambaye alijifungua mtoto wakike anayeitwa Alexis Olympia Ohanian Jr Septemba, amecheza mechi nne za mchezaji mmoja mmoja tangu aliporejea katika mchezo huo, ambapo alifikia katika hatua ya 32 bora katika mashindano ya Indian Wells kabla hajapoteza kwa dada yake Venus na baadae alitolewa na nyota Mjapan anayeinukia Naomi Osaka katika raundi ya kwanza huko Miami.

Nyota ya Mohamed Salah Yaendelea Kung'ara


LONDON, England
MSHAMBULIAJI wa Liverpool Mohamed Salah (pichani) ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Soka.

Kiungo wa Manchester City Kevin de Bruyne ameshika nafasi ya pili huku mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane akiibuka watatu.

Salah, mwenye umri wa miaka 25, amefunga mabao 31 katika mechi 34 za ligi alizoichezea timu hiyo msimu huu.

Nyota huyo wa Misri, ni mwanasoka wa kwanza wa Afrika kupewa tuzo hiyo, ambaye pia alitwaa tuzo kutoka kwa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa mwezi uliopita.

Mshambuliaji wa Chelsea na England Fran Kirby ameshinda tuzo ya uchezaji bora wa mwaka kwa wanawake (FWA).

Salah amefunga mabao 43 katika mashindano yote baada ya kusajiliwa na Liverpool kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 34 akitokea Roma ya Italia.

Mchezaji huyo wazamani wa Chelsea na Basel alifunga mara mbili katika mchezo wa kwanza wakati Liverpool ikiibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Roma katika mchezo wa nusu wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwenye Uwanja wa Anfield wiki iliyopita.

Kikosi cha kocha Jurgen Klopp tayari kiko Italia kwa mchezo wa Jumatano dhidi ya Roma utakaofanyika kwenye Uwanja wa Stadio Olimpico kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano.

MBIO ZA WACHEZAJI WAWILI

Salah na mchezaji mwenye umri wa miaka 26 Mbelgiji De Bruyne alipata zaidi ya asilimia 90 ya kura zilizopigwa na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Soka.

Mwenyekiti wa FWA Patrick Barclay alielezea mpambano wa wawili hao kama ni wa nguvu zaidi tangu mwaka 1968-69", wakati walipopambana kati ya Tony Book wa Manchester City na yule wa Derby, Dave Mackay.

Wachezaji wengine waliopigiwa kura na wanachama wa FWA walikuwa: Sergio Aguero (Man City), Christian Eriksen (Tottenham), Roberto Firmino (Liverpool), Nick Pope (Burnley), David Silva (Manchester City), Raheem Sterling (Man City) na Jan Vertonghen (Tottenham).

Zidane Aaanza Nyodo, Real Ikitinga Fainali Ulaya


MADRID, Hispania
ZINEDINE Zidane anasema kuwa mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya “ni vinasaba vya Real Madrid” baada ya kikosi chake kutinga kwa mara ya nne fainali ya mashindano hayo katika kipindi cha miaka mitano.

Real ilipata nafasi hiyo ya kucheza fainali ikisaka kushinda kwa mara ya tatu mfululizo taji hilo baada ya Karim Benzema kufunga mara mbili na kuwawezesha mabingwa hao watetezi kutoka sare ya 2-2 na kupata ushindi wa jumla wa 4-3 dhidi ya Wajerumani Bayern Munich.

Real Madrid tayari imeshuhudia wapinzani wao wakubwa Barcelona wakitwaa taji la La Liga ndhini Hispania msimu huu, lakini Zidane anasema mashindano hayo makubwa Ulaya mara nyingi timu yake inafanya vizuri, ambapo imeshatwaa taji hilo mara 12.

"Ni vinasaba vya klabu yetu. Kamwe hatuachi kupambana hadi katika dakika ya mwisho, kama walivyofanya Bayern usiku huu.”

Zidane alisema Benzema alikuwa zaidi ya kuanza katika mchezo huo baada ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa alitolewa katika kipindi cha kwanza katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliofanyika Jinini Munich.

"alistahili kufunga, alifanya kazi kwa bidii na kamwe huwa hana tabia ya kutojituma.

"Mchezo wake mara zote huwa ni sawa na amekuwa mchezaji mwenye msaada mkubwa ketu.”
Baada ya kushinda 2-1 katika mchezo wa kwanza nchini Ujerumani, Bayern Munich walikuwa wakihitaji ushindi katika mchezo huo wa marudiano uliofanyika kwenye Uwanja wa Bernabeu ili kutinga fainali lakini walijikuta wakimaliza mchezo huo kwa sare ya 2-2 na kupata ushindi wa jumla wa mabao4-3.

Joshua Kimmich aliifungia Bayern mapema kwa mkwaju wa umbali wa meta sita, kabla Karim Benzema hajafunga kwa kichwa akiisawazishia Real Madrid akiunganisha wavuni krosi ya Marcelo dakika nane baadae.

Liverpool Yapata Pigo Ikicheza na Roma Ulaya


LONDON, England
JURGEN Klopp amepata pigo kubwa kuelekea mchezo wao wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Roma baada ya msaidizi wake muhimu Zeljko Buvac kuachia ngazi kutokana na sababu za kibinafsi.

Huku Liverpool ikiwa mbioni kukabiliana na Roma katika mji mkuu wa Italia Jumatano usiku, klabu hiyo imethibitisha juzi kuwa Buvas atakuwa nje ya timu hiyo hadi mwishoni mwa msimu.

Klopp alimuelezea Buvas kama "kichwa" katika suala zima la ukocha na kutokuwepo kwake ni pigo kubwa kwa Liverpool ambayo inaangalia kuendelea ushindi wake wa awali wa mabao 5-2 dhidi ys Roma.

Tetesi zilianza kusambaa tangu Jumapili kuwa Bosnian anaachia ngazi, lakini Liverpool ilikanusha taarifa hizo kwa kusisitiza kuwa Buvac bado ni muajiriwa wa klabu hiyo na pengo lake halitaathiri kitu.

Buvac, ambaye alikuwa katika benchi pamoja na Klopp katika mchezo wa Jumamosi ambao timu hiyo ilitoka suluhu dhidi ya Stoke, alikuwa msaidizi wa karibu kabisa wa kocha huyo Mjerumani katika kipindi cha miaka 17 iliyopita.

Wawili hao walikuwa pamoja huko Mainz katika miaka ya 1990 na waliungana tena wakati Klopp alipomfanya kuwa msaidizi wake wakati alipokuwa kocha mwaka 2001.

Wakati alivyopanda pamoja wawili hao walienda Borussia Dortmund mwaka 2008 ambako walishinda mfululizio taji la Bundesliga na kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kabla hawajahamia Liverpool.

Wakati huohuo, leo inashuka nchini Italia kucheza dhidi ya Roma katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Kikosi cha Klopp kiko mbioni kutinga fainali baada ya kuwa na faida ya mabao mengi iliyopata katika mchezo wa kwanza ilipoifunga Roma mabao 5-2, ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 2007 walipofikia hatua ya juu ya mashindano makubwa Ulaya.

Lakini nje ya uwanja presha ni kubwa wakati shabiki wa Liverpool Sean Cox lyuko katika koma baada ya kushambuliwa kabla ya mchezo wa wili iliyopita uliofanyika kwenye Uwanja wa  Anfield.

Mashabiki wawili wa Roma walikamatwa kuhusiana na jaribio hilo la kutaka kuuwa na gwiji wa klabu hiyo Francesco Totti ametaka kuwepo kwa mchezo wa kiungwana, na kuheshimiwa kwa wapinzani.

Mshambuliaji wazamani wa Roma Mohamed Salah alifunga mara mbili na kutengeneza mengine mawili wakati Liverpoo; ikizifumania nyavu mara tano kwenye Uwanja wa Anfield kabla ya mawili yaliyofungwa katika dakika za mwisho.

Kikosi cha Klopp kitashuka uwanjani bila ya kiungo Alex Oxlade-Chamberlain, ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima kutokana na maumivu ya goti, pamoja na Georginio Wijnaldum ambaye alibadilishwa katika mchezo wa kwanza.

Emre Can (mgongo) na Adam Lallana (maumivu ya nyama za paja) nayo pia wanapambana na maumivu.