Monday, 23 October 2017
Mkurugenzi TAA ataka Tughe kutetea wafanyakazi
Na Mwandishi Wetu
KAIMU Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela
amewataka viongozi wa Chama cha Wafanyakazi kusikiliza malalamiko
ya wafanyakazi
bila kubagua.
Bw.Mayongela
alisema viongozi wa Wafanyakazi kupitia matawi mawili ya Chama cha Wafanyakazi,
TAA Makao Makuu na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),
kutenda haki kwa kusikiliza malalamiko ya wafanyakazi wote na kuyawasilisha kwa
wasilisha kwa mwajiri ili yafanyiwe kazi.
Alitoa kauli hiyo
juzi wakati viongozi wa matawi hayo walipokwenda kujitambulisha ofisi kwake TAA
Makao Makuu, ambapo alisisitiza kuwa wafanyakazi wa chini ndio wenye matatizo
makubwa, lakini hawasikilizwi na kutatuliwa matatizo yao kwa wakati.
“Ninashukuru
uongozi mmekuja kuonana nami, ninahitaji ushirikiano wenu kama Chama cha
Wafanyakazi, muwatumikie wafanyakazi kwa kutenda haki mkisikiliza matatizo ya
kila mmoja na kufikisha sehemu husika na ninawaahidi kuwa nanyi bega kwa bega
kutatua matatizo ya wafanyakazi kwani wao ndio wanafanya TAA iwepo, “alisema
Mayongela.
Alisema
wafanyakazi endapo wakifanya kazi bila manung’uniko wala makundi, mamlaka
itasonga mbele kwa kuwa na uongozi sio kupigana vita bali unatakiwa kujijenga
na kuwa kitu kimoja.
Hatahivyo alisema
kwa sasa yupo mbioni kuangalia namna ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupitia makusanyo yatakayotokana na
vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuongeza tija na ufanisi wa kazi ili kuongeza
ari kwa wafanyakazi.
Aliendelea kusema
kuwa inaonekana wafanyakazi wengi wa TAA wamekata tamaa kutokana na kufanya kazi
nyingi na wakati mwingine kupitiliza muda wa kazi wa kawaida bila kupata
stahiki yeyote.
“Kwa msaada wa
Mungu nina imani atanionyesha wapi fedha zilipo na jinsi ya kuzitumia ipasavyo
kwa masuala ya msingi, na ninakusudia hadi kufika Desemba mwaka huu niweze
kuboresha maslahi ya wafanyakazi.
Watu wanafanya
kazi sana lakini maslahi ni madogo, unaona kabisa jinsi mtu anavyoitumikia
taasisi kwa moyo, lakini sura inaonesha jinsi alivyokata tamaa, ninaamini kwa
kufanya hivi itaongeza tija na bidii ya kazi.” Alisema Bw. Mayongela.
Halikadhalika, Bw.
Mayongela amesema atahakikisha wafanyakazi wanapata vitendea kazi vya uhakika
kulingana na kazi zao, zikiwemo bajaji, pikipiki na magari kwa ajili ya doria
na shughuli za uendeshaji ndani ya Viwanja vya Ndege.
Pia amewataka
viongozi hao kuwa karibu na wafanyakazi ili kuhakikisha wanawahamasisha
wanafanya kazi kwa bidii, uaminifu na uadilifu ili kuondoa mianya na tabia za
upokeaji wa rushwa, kwa kuwa TUGHE ni daraja kati ya mwajiri na wafanyakazi.
Naye Mwenyekiti wa
TUGHE tawi la TAA Makao Makuu, Bw. Nasib Elias mbali na kumshukuru Kaimu
Mkurugenzi Mkuu kwa kuwapa fursa ya kukutana naye, lakini alimuomba kuendelea
kudumisha mahusiano baina ya mwajiri na Tughe.
Pia alimuomba
aitake menejimenti yake kuwa na utaratibu wa kuweka milango wazi kwa
wafanyakazi kama yeye ili waweze kusikiliza na kutoa majibu sahihi kwa baadhi
ya masuala ya kiofisi yanayowasilishwa na wafanyakazi kwao na sio kila jambo
liwasilishwe kwake.
“Tunakuombea kwa
Mungu akutie nguvu kwa haya unayotaka kufanya likiwemo la kuboresha maslahi ya
wafanyakazi kwa kuwa litasaidia kuamsha morali ya kazi kwa wafanyakazi, lakini
hii sera yako ya kuwacha milango wazi, tunaomba nayo itekelezwe katika ngazi ya
menejimenti yako kwani kuna mambo ambayo yanaweza kumalizwa na Wakurugenzi na
Mameneja wenyewe na sio lazima yafike kwako, “ alisema Bw. Elias.
Katika kuboresha
maslahi ya wafanyakazi ambacho kimeonekana ni kipaumbele cha Kaimu Mkurugenzi
mkuu kwa wafanyakazi, Bw. Elias amemuomba kuangalia namna bora ya kusimamia
maslahi hayo ikiwemo kuuasili mkataba wa hali bora (SBA) kama inavyotekelezwa
na taasisi nyingine za serikali.
Thursday, 19 October 2017
Naibu Waziri amtaka mkandarasi haraka
Na
Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Ujenzi), Mhe. Elius Kwandikwa, amemtaka Mkandarasi wa
kampuni ya ujenzi ya China ya CHICO aliyepewa zabuni ya ujenzi wa Kiwanja cha
ndege cha Shinyanga kuanza ujenzi huo haraka.
Akizungumza mara
baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho katika eneo la Ibadakuli
leo, mkoani Shinyanga, Mhe. Kwandikwa, amesema kuwa haoni sababu ya mkandarasi
huyo kuchelewa kuleta vifaa vyake katika eneo la mradi hadi sasa wakati tayari
mkataba wa kuanza kazi hiyo umeshasainiwa.
"Mkandarasi
hana sababu ya kuchelewa kuanza kazi wakati fedha zipo na zimeshatengwa kwa
ajili ya mradi huu na mkataba umeshasainiwa,
sasa namwagiza kuleta vifaa vyake na kuanza kazi mara moja",
amesema Mhe. Kwandikwa.
Aidha, Mhe.
Kwandikwa amemtaka Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Msollow kuhakikisha
anakuwa bega kwa bega na kutoa ushirikiano kwa kumsimamia mkandarasi huyo, ili
kuhakikisha kiwanja hicho kinakamilika mapema na kwa viwango vinavyotakiwa.
"Naamini
tukimsimamia vizuri mkandarasi huyu tutapata kiwanja kizuri na imara hapa
Shinyanga na tutafungua fursa mbalimbali za kiuchumi katika mkoa huu",
amesisitiza Mhe. Kwandikwa.
Kwa upande wake,
Meneja wa kiwanja cha ndege cha Shinyanga, Bw. Msollow, amemhakikishia na
kuahidi kuwa atatoa ushirikiano kwa mkandarasi huyo atakapowasili eneo la
mradi.
Bw. Msollow
amesema kuwa mradi huo utahusisha ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege,
jengo la abiria, maeneo ya maegesho ya ndege na mnara wa kuongozea ndege.
Amesema barabara
ya kutua na kupaa kwa ndege inarefushwa kwa urefu wa Kilometa mbili na itakuwa
kwa kiwango cha lami, ikigharimu zaidi ya shilingi Bilioni 49.
Wakati huohuo,
Naibu Waziri Kwandikwa, amekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwigumbi -
Maswa (KM 50.3), mkoani Simiyu na kumsisitiza mkandarasi anayejenga barabara
hiyo kuikamilisha kwa wakati na kwa viwango.
Amesisitiza kuwa
kukamilika kwa barabara hiyo ambayo ni kiungo kwa wananchi wa Maswa, Bariadi,
Lamadi na Mwanza, kutarahisisha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo
katika maeneo hayo.
Naye, Meneja wa
Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani Simiyu, Mhandisi Albert Kent, amesema
kuwa mradi upo katika hatua nzuri na unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka
miwili kutoka sasa.
Naibu Waziri
Kwandikwa amefanya ziara ya kikazi katika mkoa wa Shinyanga na Simiyu ambapo
amekagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake.
Multichoice Yatimiza miaka 20 kwa Mbwembwe.. Ofa kabambe kwa watakaohudhuria maonesho Mlimani City!
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Multichoice Tanzania inatimiza miaka 20 toka kuanza kutoa huduma katika soko la Tanzania.
Multichoice inajivunia mafanikio yake katika soko la Tanzania toka
kuanzishwa kwake mwaka 1997, katika kipindi cha miaka 20, tumelihudumia soko la
Tanzania Kwa kutoa burudani za kiwango cha juu na ambazo hazipatikani sehemu
yeyote ile.
Katika kipindi cha
miaka 20 tumewaletea watanzania michuano ya mpira (World Cup, Euro Champions
League, Europa League, EPL, La Liga, AFCON na makombe mengine mengi), pia
tumeweza kuwaletea maudhui mengi kupitia chaneli yetu ya MNET, Africa Magic na
nyingine nyingi.
Multichoice
tumekua mstari wa mbele katika kukuza tasnia ya Burudani nchini kwa kipindi
chote cha miaka 20 wote mnakumbuka mchango wetu katika mziki kupitia chanel “O”
Trace, MTV Base na sasa Trace Mziki. Tasnia ya Filamu tumechangia ukuaji wake
kupitia Africa Magic na baadae Maisha Magic East na sasa Maisha Magic Bongo
(MMB) ambayo ni maalum kwa kazi za Kitanzania. Tumekuza michezo kupitia
uwekezaji wetu kwenye riadha na michezo mingineyo.
Katika Kusheherekea maadhimisho ya miaka 20, Multichoice imeandaa maonesho ya siku 2 yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City kuanzia leo Alhamis Oktoba 19 hadi kesho Ijumaa kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 11:00 jioni.
Katika maonesho haya utapata kushuhudia maendeleo ya Teknolojia
yetu ya tangu 1997 mpaka sasa na huduma mbali mbali zitolewazo na Multichoice. Kutakuwa na
mabanda kadhaa likiwemo la Supersport, MNET, Maisha Magic Bongo, Fashion, Banda
la watoto na mengine mengi.
Kutakua na Ofa
kabambe ndani ya siku 2 za Maonesho, ambapo Mteja atajipatia full set ya DStv
kwa sh. 59,000 tu hii ikijumlisha
kifurushi cha mwezi mmoja BURE kwa king’amuzi cha HD cha Zappa.
Kwa King’amuzi cha
Explora Mteja atapata Kwa sh. 240,000 pamoja na kifurushi cha Compact cha mwezi
mmoja BURE…
Ofa hii ni kwa
siku za maonesho tu, ambazo ni Alhamisi na Ijumaa hii tu, Hii si ya kukosa!!!
#20YearsOfAwesomeness!!!!!
Ukarabati KIA kukamilika Desemba 2017
![]() |
Mafundi
wakiendelea na ukarabati katika jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege wa Kimataifa
cha Kilimanjaro (KIA). Ukarabati huo unatarajiwa kukamilika Desemba 2017.
|
Na Mwandishi Wetu
KIWANJA
cha ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA) kinafanyiwa ukarabati mkubwa
unaohusisha miundombinu mbalimbali, ambapo unaotarajiwa kukamilika Desemba
2017.
Maeneo
yanayofanyiwa ukarabati ni pamoja na jengo la kupumzikia abiria, upanuzi wa
maegesho ya ndege na mifumo ya maji taka.
Akizungumza
baada ya kukagua maendeleo ya ukarabati huo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Mhe. Elius Kwandikwa amesema ameridhika na hatua iliyofikia,
ikiwa ni zaidi ya asilimia 90.
"Nimeridhishwa
na ukarabati unaoendelea katika kiwanja hiki na nafikiri mmejionea wenyewe kazi
inaendelea vizuri, hivyo naamini kutokana na hali hii kazi itakamilika hivi
karibuni, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.
Aidha,
Mhe Naibu Waziri amefafanua kuwa ukarabati huo ambao pia umehusisha maboresho
ya mfumo wa maji taka unalenga kuleta tija kwa mkoa huo na Taifa kwa ujumla
kutokana na kuwepo ongezeko la abiria, huduma za kijamii na kibiashara.
Amesisitiza
kuwa Serikali itaendelea kukarabati na kujenga viwanja vya ndege nchini ili
kurahisisha huduma za usafiri wa anga kwa wananchi wake lengo likiwa ni
kuchochea fursa za kiuchumi ambazo zitasaidia kulipeleka Taifa katika uchumi wa
kati.
Naye Meneja
Miradi wa KIA, Mhandisi Mathew Ndossi,
amesema kuwa maegesho yatakapokamilika yatakuwa na uwezo wa kuegesha
jumla ya ndege kubwa 11 kwa wakati mmoja badala ya 6 zinazoegeshwa sasa.
Ameongeza
kuwa abiria wanatarajiwa kuongezeka kutoka 800,000 kwa mwaka hadi kufikia 1.2
milioni mara baada ya kukamilika kwa ukarabati huo.
Hivi
karibuni KIA imeandaa mbio za marathoni zitakazofanyika Novemba 19 kwa
kushirikisha raia mbalimbali wa nadani na nje ya nchi, ili kuvutia zaidi
watalii na watumiaji wa usafiri wa anga kwa ujumla.
Kia
pamoja na Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) ni milango
ya kuingia nchini kwa usafiri wa anga kwa watalii wanaotoka nchi mbalimbali
duniani, kuja kutembelea mbuga za wanyama na
vivutio vinavyopatikana kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na
Zanzibar.
Wakati
huo huo, Naibu Waziri Kwandikwa amekagua barabara ya Sakina - Tengeru (km 14.1)
na barabara ya mchepuko ya Arusha (Arusha Bypass km 42.4) ambapo amesema kuwa
kukamilika kwa barabara ya Sakina - Tengeru
ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na wageni wanaoingia
katika mkoa huo kwani kumepelekea
kupungua kwa ajali na msongamano
wa magari katika eneo hilo.
Ametoa
wito kwa wananchi kuzitunza barabara na
kutunza mazingira yanayozunguka barabara hizo ili ziweze kudumu kwa muda mrefu
kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Naye,
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Arusha Mhandisi, Johny
Kalupale, amemhakikishia Naibu Waziri
huyo kufanya kazi kwa ubora na kwa weledi ili kutimiza malengo ya Serikali ya
kuwajengea wananchi miundombinu bora na ya kisasa.
Awamu ya
pili ya mradi huo sehemu ya barabara ya mchepuo ya Arusha (Arusha Bypass),
inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), inatarajiwa kukamilika
mwakani na kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 67.
Naibu
Waziri Kwandikwa amemaliza ziara ya kikazi katika mkoa wa Kilimanjaro na Arusha
ambapo amekagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake.
Tuesday, 17 October 2017
Kocha Napoli aipa City ubingwa wa Ulaya
MANCHESTER,
England
KOCHA wa timu ya Napoli
Maurizio Sarri anasema kuwa Manchester City sasa iko viwango sawa kama Barcelona
na Real Madrid na inaweza kuendelea kufanya vizuri hadikutwaa ubingwa wa Ligi
ya Mabingwa wa Ulaya.
Man City iliyocheza
kandanda safi na kushambulia kwa dakika 20 na kufanikiwa jkupata mabao mawili
ya kuongoza dhidi ya Napoli katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Etihad juzi
lakini Waitalia hao ambao bado hawajapoteza pointi katika Ligi Kuu ya Italia ya
Serie A, iling’ang’ania na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Alipoulizwa baada
ya mchezo huo kama Man City sasa iko katika kiwango sawa na vigogo vya Hispania
na kama inaweza kutwaa taji hilo la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, Sarri alisema:
"Ndio, Nafikiri hivyo.
"Mana City
wana kikosi kisicho cha kawaida. Wako vizuri katika kila idara na wanaweza
kufanya vizuri kutokana na ubora wao, “aliongeza kocha huyo.
Kwa ushindi huo
Man City inaoongoza katika Kundi F ikiwa na pointi tisa baada ya kucheza mechi
tatu na pia inaongoza katika Ligi Kuu ya England baada ya kushinda mara saba
kutoka katika mechi nane.
Kikosi cha Guardiola
sasa hakijafungwa katika mechi 18 katika mashindano yote, ambapo imeshinda
mechi 14 kati ya hizo, tangu walipofungwa 2-1 na Arsenal katika nusu fainali ya
Kombe la FA.
Mabao kutoka kwa Raheem
Sterling na Gabriel Jesus katika dakika 13 za kwanza yalionekana kufungua
mlango kwa Man City kuibuka na ushindi lakini Napoli walijipanga upya na Sarri alisema
kuwa amefurahishwa na jinsi walivyojibu.
"Unatakiwa
kuugawa mchezo katika dakika 25 za kwanza na baadae zilizobaki. Wanastahili
sifa kubwa kwa jinsi walivyoanza mchezo, mbinu za kiufundi, kasi na jinsi
movement yao, lakini na sisi hatukuwapa shinikizo kubwa, “alisema.
Wachezaji Munich wakabidhia magari ya anasa
![]() |
Gari aina ya Uudi, ambayo wachezaji wa Bayern Munich wamekabidhiwa. |
MUNICH, Ujerumani
NYOTA wa timu ya
soka ya Bayern Munich wamekabidhiwa magari yao mapya ya anasa aina ya Audi AB.
Wachezaji hao kama
akina Robert Lewandowksi, Mats Hummels na Javi Martinez wote walipokea `michuma’
yao mipya wakati wacheaji wa kikosi hicho wakisaini autographs wakati wa hafla
ya kila mwaka ya kuabidhi magari huko Ingolstadt.
Hatahivyo,
wachezaji wengi wa timu hiyo hawakuwepo kwani walikuwa na timu zao za taifa
katika mechi mbalimbali za kimataifa.
Audi ni wadhamini
wa kuu wa klabu ya Bayern Munich, ambapo imekuwa ikitoa gari kwa kila mchezaji
wa timu hiyo tangu mwaka 2002, mwaka ambao walianza kuwa mhisa na vigogo hao wa
soka wa Ujerumani.
Sehemu ya mkataba
wao ni kuwa kampuni hiyo ya magari kila mwaka itakuwa ikitoa gari kwa kila
mchezaji, ambapo wachezaji hao Jumatatu ya wiki iliyopita walikabidhiwa
`michuma’ yao.
Karibu wachezaji
wa kikosi hicho kila mwaka wamekuwa wakipata mamilioni, walikabidhiwa seti mpya
ya matairi, ambapo sio kitu kigeni kwa wachezaji wa mabingwa hao wa Ujerumani.
Lakini gari hizo
aina ya Audi zililetwa zikiwa tayari zina majina ya wachezaji hao katika vibao
vya namba zikijulikana kama gari rasmi za Bayern. Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani wanajua kuwa gari hizo zenye namba zinaoanzia na M-DM zitakuwa zikiendeshwa na
wachezaji au viongozi wa kikosi hicho chenye maskani yake Allianz Arena.
Herufi 'M' inasimama badala ya 'Munich', wakati ‘'DM'
inasimama badala ya 'Deutscher Meister', au Mabingwa wa Ujerumani, kufuatia
ubingwa wa Bayern Munich walioupata msimu uliopita.
Wakati Bayern sio
mabingwa wa Ujerumani, kitu ambacho hakijatokea kwa miaka ya hivi karibuni- 'DM'
inakuwa 'RM', ambayo inasimama kama 'Rekordmeister', au mabingwa wa kihistoria.
Wachezaji wa Bayern
walichukua magari yao huku wakiwa na mashabiki kibao wa timu hiyo waliohudhuria
hafla hiyo, ambapo iliwachukua muda kupiga picha na mashabiki hao.
Kikosi hicho
kiliungana na kocha mpya Jupp Heynckes, ambaye wiki iliyopita alitangazwa kama mbadala wa Carlo
Ancelott.
Kocha huyo
atatimiza miaka 72 wakati akiifundisha klabu hiyo kwa mara ya nne, ambapo
walishinda taji la Bundesliga mwaka 1989, 1990 na 2013 na lile la Ligi ya
Mabingwa mwaka 2013.
Monday, 16 October 2017
Waegesha ndege 10 wa JNIA wapigwa msasa
Na Mwandishi Wetu
WAEGESHA ndege 10
wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), leo walianza
mafunzo ya siku saba ya uegeshaji ndege kutoka kwa wakufunzi wa Kiwanja cha
Ndege cha Hague cha Uholanzi yanayofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga
(CATS) jijini Dar es Salaam.
Akifungua mafunzo
hayo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela amesema kuwa mafunzo
hayo ni muhimu kwani yatazidi kuwajengea uwezo na uzoefu washiriki hao.
Bw. Mayongela
amewasisitiza washiriki hao kuzingatia kila wanachofundishwa ili waweze kuwa
mahiri na weledi katika uongozaji wa ndege za ndani na nje ya nchi zinazotumia
kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
“Waongoza ndege ni
moja ya kazi inayohusisha mawasiliano ya moja kwa moja kati ya watoa huduma
ndani ya kiwanja cha ndege, hivyo ni lazima tufikie viwango vinavyotakiwa kwa
mujibu wa sheria kimataifa,” amesema Bw. Mayongela.
Hata hivyo,
amesema TAA inajukumu kubwa la kuwaongezea uwezo watumishi wake kwa kuwapeleka
kwenye mafunzo mbalimbali ili kujijengea uwezo na maarifa.
Bw. Mayongela
amewashukuru waendeshaji wa mafunzo hayo yanayotolewa na mfuko wa Avi Assist wa
Uholanzi, ambapo amewahahakikishia kuendeleza ushirikiano waliouanzisha kwa
kushirikiana katika utoaji wa mafunzo ya kada mbalimbali.
Naye Mkuu wa
Kitengo cha Waongoza ndege cha JNIA, Bw. Lugano Mwinuka amesema mafunzo haya
yamekuja wakati muafaka, kwa kuwa walikuwa yakiyahitaji kwa muda mrefu, na sasa
anauhakika wa washiriki wataongeza ujuzi katika utendaji wao wa kazi.
Bw. Mwinuka
amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa nadharia na vitendo, ambapo washiriki hao
wamegawanywa katika makundi mawili ya watu watano, ambao ni Earisner Waihula,
Emmanuel Nyaulingo, Anunciatus Alex, Fadhili Meena na Oscar Kibiki.
Watakaoingia kundi
la pili ni pamoja na Denis Kinyaga, Zennobius Mwimba, Raynard Komba, Said Mussa
na Meshack Elisante.
Tuesday, 10 October 2017
Messi apiga hat-tric Argentina ikifuzu Kombe la Dunia
QUITO, Ecuador
QUITO, Ecuador
LIONEL Messi
amefunga hat-trick wakati Argentina ikitoka nyuma na kushinda ugenini 3-1 dhidi
ya Ecuador na kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Russia
mwakani.
Brazil wenyewe
tayari walishafuzu huku Luis Suarez akizifumania nyavu mara mbili wakati Uruguay
ikiichapa Bolivia 4-2 na kufuzu, pamoja na Colombia nayo pia ikifuzu licha ya
kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Peru.
Peru ilimaliza
mchakato huo ikiwa katika nafasi ya tano ya Kanda ya Amerika Kusini ya kufuzu
kwa Kombe la Dunia na sasa itakutana na New Zealand katika mechi mbili za
mchujo zitakazochzwa nyumbani na ugenini.
Lakini Alexis
Sanchez na Chile wametupwa nje baad aya kupokea kichapo cha mabao 3-0 ugenini
dhidi ya Brazil.
Argentina ilianza
siku ikiwa katika nafasi ya sita na kuwa katika hatari ya kuweza kushindwa
kufuzu kwa Kombela Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1970.
Timu hiyo ilianza
vibaya katika mchezo huo uliofanyika katika ukanda wa juu uliopo hapa na
wenyeji walikuwa mbele katika sekunde ya 38 kupitia kwa Romario Ibarra likiwa n
bao la mapema zaidi kufungwa Argentina katika Kombe la Dunia.
Hatahivyo, Argentina,
ambao ni washindi wa pili wa Kombe la Dunia mashindano yalipofanyikia nchini
Brazil 2014, walipambana huku Messi akiwa katika kiwango cha hali ya juu.
Messi, ambaye ni
bingwa mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa dunia, alisawazisha baada
ya dakika 12 baada ya kushirikiana vizuri na kiungo wazamani wa Manchester
United Angel di Maria.
Bao lake la pili
lilikuja dakika nane baadae kwa shuti kali ndani ya eneo la hatari kabla
hajafunga la tatu na kuiwezesha timu yake kufuzu kwa fainali za mwakani za
Kombe la Dunia.
MAJAGA
KWA CHILE
Chile,ambayo
ilitwaa taji la Copa America katika mashindano mawili yaliyopita, ilikuwa
nalengo la kufuzu kwa mara ya tatu mfululizo katika Kombe la Dunia baada ya mara
ya mwisho kucheza hatua ya 16 bora mwaka 2010 na 2014.
Walianza raundi
hiyo ya mwishi wakiwa katika nafasi ya tatu, lakini walishindwa baada
yakufungwa mabao mawili na Brazil ndani ya sekunde tatu yaliyofungwa na Paulinho
na Gabriel Jesus.
Wakati Peru
ikifunga bao la kusawazisha katika dakika za mwisho za mchezo huo dhidi ya
Colombia, Chili ilikuwa ikihitaji kufunga tu ili kucheza hatua ya mtoano.
Monday, 2 October 2017
Sunday, 1 October 2017
Chaneta waibuka na mikakati ya kuinua netiboli
Na Mwandishi Wetu
UONGOZI mpya wa
Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) umesema kuwa umejipanga kuhakikisha
unaleta maendeleo ya mchezo huo hapa nchini.
Akizungumza jana Katibu Mkuu mpya wa Chaneta, Judith Ilunda (pichani) alisema kuwa,
wanajua changamoto zilizopo katika chama hicho, lakini wamejipanga kukabiliana nazo ili kuleta maendeleo katika mchezo huo.
Ilunda ambaye ni
mchezaji wazamani wa timu ya Bandari Dar na timu ya taifa ya netiboli kwa muda
mrefu, alisema kuwa watahakikisha mchezo huo unachezwa katika shule za msingi,
sekondari na mitaani.
Alisema pia
watahakikisha wanaendesha mashindano ya mara kwa mara na timu zenye ubora
zinashiriki, ili kuhakikisha mchezo huo unarudi katika chati kama zamani
kitaifa na kimataifa.
Alisema kamati yao
mpya itakutana hivi karibuni mara baada ya kukabidhiwa ofisi na uongozi
uliopita na kutangaza zaidi mipango yao ya muda mrefu na mfupi.
Uchaguzi Mkuu wa
Chaneta ulifanyika mjini Dodoma juzi, ambapo Dk Devetha Marwa aliutwaa uenyekiti baada ya kupata kura 53
dhidi ya Damian Chonya aliyepata kura nne.
Makamu ni Anna
Gidaria aliyepata kuta 44 dhidi ya Winfrida Emmanue kura 10 na Pili Mogella
alipata kura tatu.
Nafasi ya Katibu
Mkuu ilikwenda kwa Ilunda aliyepata kura 50 dhidi ya makamu mwenyekiti
aliyepita Zainabu Mbiri aliyeambulia kura sita, huku katibu msaidizi ni Hilda
Mwakatobe aliyepata kura 30 dhidi ya 26 za Mwajuma Kisengo.
Nafasi ya mhazini
haijajazwa baada ya mgombea pekee, Grace Khatibu kupata kura nne za ndio na
hapana 49 na hivyo kutoweza kuchaguliwa kwa kuwa alikuwana kura nyingi za
hapana.
Wapiga kura walikuwa 57 kutoka mikoa 21 ya Tanzania Bara.
Pakacha Group laendesha kongamano la kujadili utatuzi wa changamoto za maji Kwembe, Kibamba, Msigani
![]() |
Viongozi wa asasi
ya Pakacha Group wakiwa na viongozi wa Kata ya Kwembe wilaya ya Ubungo mkoani
Dar es Salaam kabla ya kongamano la kujadili changamoto zinazokabili maji
katika kata hiyo jana.
|
Na Mwandishi Wetu
DIWANI wa Kata ya
Kwembe wilayani Ubungo, Dweza Kolimba amesema asasi za kiraia zina nafasi kubwa
ya kuleta maendeleo katika jamii kwa kushirikiana na wananchi na watendaji wa
serikali.
Akizungumza katika
kongamano lililoandaliwa na asasi ya Pakacha Group kwa wananchi wa kata hiyo
kwa ajili ya kujadili utatuzi wa changamoto ya maji, kuanzia ufuatiliaji wa
rasilimali fedha na utekelezaji wake, Kolimba alisema asasi hiyo itasaidia
kufanya watendaji na wananchi kufanya kazi kwa pamoja.
Alisema
ushirikiano huo utasaidia kuibua changamoto zinazokwamishwa na rasilimali fedha
au kutowajibika kwa baadhi ya watendaji.
Alisema asasi
zinaweza kuleta mabadiliko kwa kufuatilia miradi ya maji, ambayo inakwamishwa
kwa sababu mbalimbali na kuwaelimisha wananchi jinsi ya kulinda miundo mbinu ya
maji na ufuatiliaji wake.
"Pia
zinasaidia kutoa msukumo kwa utelekezaji wa miradi kwa kuibua hoja kwa
wananchi, kwa lengo moja tu, kuleta maendeleo na sio malumbano yasiyo na
msingi”, alisema mheshimiwa Kolimba.
Ofisa Mtendaji wa
Kata ya Kwembe, Hamisi Moto alisema kuwa jitihada zinafanyika ile kuondoa adha
ya upatikanaji wa maji kwa wananchi.
Kongamano hilo
limefanyika kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society kwa ajili ya kutoa
elimu kwa wananchi kufuatilia fedha zinazotengwa kwa ajili ya utoaji wa huduma
ya Maji katika kata tatu za Kwembe, Kibamba na Msigani.
Diwani huyo
alisema wananchi wanaweza kufanya ufuatiliaji kupitia mfumo wa Pets ukiwa na
malengo ya kuboresha huduma za kijamii, kuhakiki utendaji wa serikali za mitaa
na kuwezesha uandaaji wa mipango shirikishi.
Pets ni mfumo
unaowezesha ufuatiliaji matumizi ya rasilimali za umma zinazotoka Serikali Kuu
au halmashauri kwa maendeleo ya wananchi kuanzia ngazi za mitaa hadi kata na
kuendelea.
Verisiyus Magoti,
mwakilishi wa mhandisi wa maji kutoka Manispaa ya Ubungo alisema wananchi
washirikiane na watendaji ili kutatua kero za maji na jitihada zinaendelea
kuhakikisha huduma hiyo muhimu inapatikana wakati wote.
Haroun Jongo,
katibu wa Pakacha Group alisema kongamano hilo ni moja kati ya matatu
yatakayofanyika katika Kata za Kibamba, Kwembe na Msigano kwa siku tofauti
tofauti.
Alisema
makongamano hayo hayana lengo la kuwagombanisha wananchi na viongozi, bali
yanaweka msukumo katika kuhakikisha miradi inasimamiwa vizuri na inatekelezwa.
Tigo Fiesta yatikisa Ali Hassan Mwinyi Tabora
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akifungua Tamasha la Tigo Fiesta kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora juzi. |
Tamasha la Tigo
fiesta limeendelea tena usiku wa kuamkia jumamosi mkoani Tabora.
Akifungua tamasha hilo mkoani humo, mkuu wa mkoa Aggrey Mwanri alisema hii nafasi nyingine kwa mkoa wetu kuletewa fursa kwa wakazi wetu, nawapongeza sana Tigo na Clouds Media. Pia nawasihi vijana kuondokana na mimba za utotoni na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Nandy
Naye meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Gwamaka Mwakilembe amesema, mwaka huu tumeamua kudhamini tamasha
hili kubwa kwa lengo la kuwapa burudani wateja wetu na kuendeleza muziki wetu
wa ndani, hii itasaidia kuwapatia kipato wasanii wetu na kuendeleza vipaji vyao.
Kwa wateja wetu ndani ya msimu huu wataweza kujipatia ofa mbalimbali wanunuapo
tiketi kwa tigopesa.
Kwa upande wa
burudani yenyewe, jumla ya wasanii 13 walipanda jukwaani kwa nyakati tofauti
lakini msanii Ben pol aliingia kivingine alipowashilikisha kikundi cha ngoma za
utamaduni wa kinyamwezi cha mapambano na kuimba nao nyimbo tofauti tofauti za
kinyamwezi na za Ben ikiwemo wimbo 'Tatu'na kutengeneza 'remix' ya aina yake
Nao kundi la
Rostam kama ilivyoada walifunga tamasha kwa kuamsha mashabiki kwa shangwe
walipoimba wimbo wao wa 'huku ama kule'.
Wasanii waliopanda
jukwaani ni
1.Rostam
2.Ney wa Mitego
3.Darassa
4.Chege
5.Mr Blue
6.Nandy
7.Maua
8.Young Dee
9.Aslay
10.Jux
11.Msami
12.Ben Pol
13.Ommy Dimpoz
Tamasha hilo
linaendelea jumapili hii mkoani Kigoma kwenye uwanja wa Tanganyika.
Subscribe to:
Posts (Atom)


































