Wawakilishi wa
Matamasha ya JAMAFEST na URITHI FESTIVAL kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Hifadhi ya
Taifa ya Mlima Kilimanjaro pamoja na wa Wizara ya Maliasili na Utalii kabla ya kuanza
safari ya SIKU SITA kuelekea Kilele cha Uhuru Kama sehemu ya matukio ya
Matamasha hayo yaliyozinduliwa na Makamu wa Rais ,Mama Samia Suluhu Hassan.
(Na Mpigapicha Wetu).
Na
Mwandishi Wetu, Moshi
WAWAKILISHI
wanne kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika matamasha JAMAFEST na
URITHI FESTIVAL wanaendelea na safari ya siku sita ya kupanda Mlima Kilimanjaro
kuelekea kilele cha Uhuru ikiwa ni sehemu ya matamasha hayo yaliyozinduliwa
Jumapili na Makamu wa Rais, Samia Suluhu
Hassan.
Wanaopanda
Mlima Kilimanjaro kama sehemu ya matamasha hayo makubwa kwa nchi za Afrika
Mashariki ni pamoja na Joel Acana kutoka nchini Uganda, Luca Waiganja kutoka
nchini Kenya na Anita Brown wa Tanzania wakiwakilisha tamasha la JAMAFEST huku
Jocktan Makeke akiwakilisha tamasha la Urithi Festival.
Akizungumza
wakati wa hafla ya kuwaaga washiriki hao, Mwakilishi wa Katibu Mkuu waWizara ya
Maliasili na Utalii, William Mwita alisema chanzo cha tamasha la JAMAFEST ni
utekelezaji wa maelekezo ya sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya
kutaka Malikale na Utamaduni kutumika kama vivutio vya Utalii.
“Sekretarieti
ilizielekeza nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2012
zihakikishe Malikale na utamaduni unatumika kama kivutio cha utalii ili uweze
kutumika katika maendeleo ay nchi za afrika Mashariki,”alisema Mwita.
Alisema
baada ya maelekezo hayo, sekretarieti ilianzisha tamasha la Sanaa na Utamaduni
kwa nchi za Afrika Mashariki likiwa tayari limefanyika katika majiji
matatu; Kigali (Rwanda), Nairobi (Kenya), Kampala (Uganda) na sasa linafanyika
Dar es Salaam Tanzania.
Kwa
Tanzania, tamasha la JAMAFEST lilizinduliwa Jumapili sambamba na tamasha la
URITHI FESTIVAL, tamasha ambalo liko kwenye ngazi ya kitaifa likiwa na maudhui
kama ya tamasha la JAMAFEST.
Wakati
Jamafest inaunganisha wana Afrika Mashariki na kutumika kama kivutio cha Utalii
au zao la utalii, Urithi festival linafanya mambo hayo hayo kwa Tanzania, kamba
unaunganisha Watanzania na inatumika kama zao la Utalii.
Mapema
mwakilishi wa Kamishna Mkuu wa Uhifadhi wa shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA), Victor Kitansi aliwakapongeza waratibu wa matamasha hayo kufanya
uamuzi wa kutumia sehemu ya matukio kuwa ni kushiriki kupanda Mlima
Kilimanjaro.
Tamasha
la JAMAFEST ambalo hufanyika kila baada ya miaka miwili kuzunguka nchi
wanachama linafanyika kwa muda wa siku nane huku Tamasha la Urithi Festiva
likifanyika katika mikoa 12 ya Tanzania Bara kwa kila mkoa kuionesha kivutio
ambacho kitatumika kama zao la Utalii.
No comments:
Post a Comment