Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Isack Kamwelwe (Mwenye
suti ya bluu) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA)
Mhandisi Julius Ndyamukama mara baada ya
kuwasili kwa ajili
ya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi katika jengo la tatu la abiria (TB III) katika Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA)
jioni
ya leo.
Na Mwandishi Wetu
JENGO la Tatu la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Julius Nyerere (JNIA), Terminal 3,
litakabidhiwa mapema kwa wamiliki, imeelezwa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack
Kamwelwe amesema kuwa jengo hilo, ambalo litakuwa na uwezo wa kuchukua abiria
milioni 6 kwa mwaka, litakabidhiwa Mei 29, ikiwa ni siku moja kabla tarehe ile
ya awali iliyoahidiwa na mkandarasi kulikabidhi.
Awali, mkandarasi aliahidi kukabidhi jeingo hilo, Mei
30 kwa wamiliki, ambao ni Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa ajili
ya maandalizi ya mwisho kabla ya kuzinduliwa rasmi na Rais John Pombe Magufuli
baadae mwaka huu.
JENGO TAYARI
Tayari ujenzi wa jengo hilo umekamilika kwa asilimia
99.5 na sasa vitu vikubwa vinavyofanyika
ni kufunga vifaa mbalimbali, vikiwemo vile vya usalama, milango, vitu na vile
vya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TRA).
Alisema kuwa tayari ujenzi umeshakamilika na watu wa
TRA, TTCL, Fire na wengine wanaweka mifumo yao ya huduma ili kukamilisha ujenzi
huo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Isack Kamwelwe katikati akiwa anaelekea katika jengo la tatu la Abiria (TB III) kuona maendeleo ya mradi wa ujenzi, kulia kwake ni Mhandisi Msimamizi
wa Ujenzi wa jengo hilo Barton Komba na kushoto kwake ni Msimamizi wa miradi ya Viwanja
vyote vya Ndege Tanzania Mhandisi Godson Ngomuo.
“Mtendaji Mkuu kwa sasa anahangaika na watoa huduma
na wanaotakiwa ni wale wenye uwezo mkubsa na ambao hawafanyakazi kwa mazoea na ni
bora wakapata vijana wa kitanzania wenye uwezo mkubwa wa kutoa huduma katika jengo
hilo bora kabisa na la kisasa, “ alisema Kamwele baada ya kukagua jengo hilo.
MAJARIBIO
Alisema baada ya Mei 29 wataanza kufanya majaribio ya matumizi
mbalimbali katika jengo hilo, ambalo halina tofauti kabisa na majengo ya
viwanja vya Ulaya nan chi nyingine zilizoendelea.
Aidha, Kamwele alisema baada ya kukamilika kwa Jengo
l Terminal 3, ujenzi utahamia katika terminai 2, ambalo lenyewe litatumika kwa
ajili ya abiria wa hapa nchini ambao wanatoka na kuwasili kutoka mau kwenda
mikoani.
Terminal 3 ina madaraja 12, ambayo yana uwezo wa
kuegesha ndege kubwa za idadi hiyo kwa wakati mmoja pia kutakuwa na mageti 16
ya kuingilia na kutokea katika ndege.
Alisema kuwa katika kudhihirisha kuwa ujenzi wa
Terminal 3 tayari wafanyakazi wamebaki 1,000 kutoka 2,900 ambao walikuwa
wakifanya shuhghuli mbalimbali za ujenzi.
Tayari baadhi ya majengo yaliokuwa ofisi za muda
zilizojengwa na mkandarasi katika eneo hilo la Terminal 3 kwa ajili ya kutoa
huduma mbalimbali za ujenzi, zimeshavunjwa.
Waziri alisema ameridhishwa kabisa na maendeleo ya
ujenzi wa jingo hilo na baada ya Mei 29, TAA itakuwa ikiendesha mafunzo
mbalimbali kwa ajili ya watoa huduma uwanjani hapo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Isack Kamwelwe akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi Msimamizi wa
Ujenzi Barton Komba kutoka Wakala wa barabara (TANROADS) alienyoosha mkono juu kuhusu eneo la maegesho ya magari katika
Jengo la tatu la Abiria (TB III) wakati wa ziara yake
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jioni ya leo.
Alisema Mtendaji Mkuu tenda anayohangaika nayo ni
watoa huduma kwani wanataka wale wenye uwezo mkubwa, ambao wataendana na ubora
wa jingo hilo, hivyo hawataki wale wanaotoa huduma kwa mazoea.
Waziri alipotembelea jengo hilo alishuhudia watu wa
TRA, Uhamiaji na wengine wakifunga vifaa vyao, tayari kutoa huduma wakati
wowote kiwanja hicho kitapoanza kutumika.
Juni mosi wataanza kutoa huduma kwa majaribio
uwanjani hapo, hasa ,ujaribu mifumo mbalimbali kabla ya kutoa taarifa kwa Rais
Magufuli kuuzindua jengo hilo la tatu la abiria.
Awali, akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa
ujenzi wa TB III, Kaimu Mkurugenzi Mkuu TANROADS Mhandisi Crispin Akoo alisema kutokana
maendeleo mazuri ya ujenzi Mkandarasi anatarajia kukabidhi jengo mapema.
“Hadi kufikia
terehe 31 Julai 2018 maendeleo yalikua ni asilimia 78.33, lakini hadi kufikia
tarehe 18 Mei 2019 ujenzi wote ulikua umefikia asilimia 99.5, ” alisema.
Kuhusu maandalizi ya uendeshaji Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi Julius Ndyamukama alimweleza
Waziri kwamba majaribio na maandalizi ya uendeshaji yalianza tangu mwezi machi
mwaka 2018 na yapo katika hatua za mwisho.
“Majaribio ya kwanza ya kwanza ya mifumo na vifaa
vinavyotumia umeme yalianza mwezi Julai 2018 kwa sasa yamefikia asilimia 96 na
muda sio mrefu yatakamilika.”
Aidha Mhandisi Ndyamukama aliongeza kwamba majaribio
hayo yanatarajiwa kufanyika ndani ya miezi mitatu kuanzia mwezi Mei na ifikapo
mwezi Agosti yatakua yamekamilika.
Naye Mhandisi Barton Komba alimwambia mwandishi wetu
kuwa, kwa wakati mmoja jingo hilo linaweza kuhudumia hadi abiria 2800 bila
tatizo, huku kukiwa na checking counter 42, 37 zikitoa huduma kwa abiria wa
madaraja ya kawaida na wale wa business huku tano zikitoa huduma kwa Commecial
Important People (CIP).
No comments:
Post a Comment