Mkurugenzi wa Kiwanja cha Kimataifa cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo. |
Na Mwandishi Wetu
UONGOZI wa Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam umesema kuwa
umejipanga mathubuti kiusalama.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa
JNIA, Paul Rwegasha wakati akitoa ufafanuzi kuhusu madai ya abiria kuchukua
muda mrefu katika jengo la pili la abiria wakati wakiwasili kiwanjani hapo
kabla ya kutoka nje ya jengo hilo.
Mbali na madai hayo, pia Rwegasha
alitolea ufafanuzi madai ya msanii maarufu nchini Ray Kigosi kuwa aliibiwa raba
na perfume kiwanjani hapo kutoka katika begi lake wakati akisafiri kwenda Dubai
akitokea JNIA tarehe 3 Jan, 2019.
Alisema kuwa mtangazaji wa Radio
Clouds, Ephahimu Kibonde alilalamika katika kipindi cha Jahazi kuwa, alitumia saa
mbili kabla ya kutoka nje ya Kiwanja hicho baada ya kuwasili akitokea Afrika
Kusini.
Kibonde alishangaa abiria raia wa
Tanzania kuchukua muda mrefu Kiwanjani hapo wakati alitakiwa kutumia muda
mfupi kwa kuwa hana mambo mengi ya kukaguliwa, tofauti na wale wanaotoka nje ya nchi.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji JNIA, Kanankira Mbise (kuhoto) akizungumza huku Mkurugenzi wa kiwanja hicho, Paul Rwegasha akimsikiliza. |
Rwegasha alisema kuwa JNIA imefungwa
kamera za usalama za CCTV katika maeneo yote ili kuhakikisha usalama wa abiria
na mali zao wakati wakiwasili au kuondoka nchini kupitia kiwanjani hapo.
Alisema kuwa mbali na mifumo
mathubuti ya ulinzi na usalama, pia uongozi wa kiwanja hicho unasera ya kutotoa
msamaha kwa Mtumishi yeyote atakayefanya udokozi na uwizi wa mali za abiria,
ambapo akibainika anapelekwa kwenye vyombo vya sheria na kufukuzwa kazi moja
kwa moja.
“Kamwe hatutamvumilia mfanyakazi yeyote
mwenye tabia za kidokozi, ambaye atabainika kuiba mzigo wa abiria, kwani
tutamtimua mara moja, na hilo kila mfanyakazi analijua ipo katika sera yetu,,
“alisema Rwegasha.
Damas Temba (kushoto), ambaye ni Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kiwanjani hapo akizungumza sula la usalama. |
Aliomba watu wanapopata matatizo au
changamoto kiwanjani hapo, kwanza wawasiliane na uongozi wa kiwanja ili kupata
ufafanuzi na utatuzi wa matatizo yao kwa haraka, ambapo mwenendo wake
utaangaliwa kwenye kamera za usalama ambazo zipo tangu abiria akiingia
kiwanjani hadi anapopanda ndege, badala ya kukimbilia kuandika kwenye mitandao
ya kijamii, kwani kufanya hivyo sio tu kunadhalilisha kiwanja, bali na nchi
nzima kwa ujumla.
Akizungumzia Jengo la tatu la abiria
linalojengwa maeneo ya Kipawa, Rwegasha alisema kuwa wanatarajia kuanza
kulitumia mara baada ya kukamilika kwani kwa sasa kuna maeneo yanaendelea na
ujenzi, licha ya nje kuonekana kama jengo hilo limekamilka. Jengo hili
linatarajiwa kukabidhiwa kwa serikali Mei 2019.
Naye Kanankira Mbise, ambaye ni Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji kiwanjani hapo alisema kuwa, idara
yake imekuwa ikihakikisha inafanya shughuli zake kwa haraka na kufuata taratibu
ili kuondoa msongamano wa abiria wanaowasili kutoka nje ya nchi.
Kwa upande mwingine, naye Damas
Temba, ambaye ni Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kiwanjani
hapo alisema wananchi wanatakiwa kupata elimu zaidi ya kodi, kwani kuna vitu
vikiingizwa nchini lazima vilipiwe kodi, hata kama ni zawadi, ambazo zikiwa ni
nyingi.
“Abiria wanaosafiri na usafiri wa
ndege wasione eneo la Forodha kama ni adui watoe ushirikiano kwa kuwa wakweli
wa vitu walivyobeba, kwani hata zawadi zinalipiwa ushuru, mfano mtu anaweza
akawa na begi lililojaa nguo na kudai ni zawadi, au saa za mkononi zaidi ya
tatu, zipo sheria kabisa zenye kuonesha na kuzungumzia hili,” amesisitiza
Temba.
Pia alisema mizigo lazima ikaguliwe
kwa ajili ya usalama na mambo mengine, lakini wanajitahidi kufanya mambo kwa
haraka ili kuepusha msongamano wa watu katika eneo la Forodha.
Hatahivyo, katika kipindi cha jana
Jumatano cha Jahazi katika Radio ya Clouds, Kibonde alionekana kushangazwa tena
na maelezo ya Temba kuwa hata zawadi zinatozwa kodi.
No comments:
Post a Comment