Saturday, 23 January 2016

Balozi wa Kuwait azindua kisima katika shamba la Mrisho Mpoto katika kijiji cha Kibogolwa, Mkuranga



Balozi wa kuwait nchini Tanzania, Jasem Alnajem (wa pili kushoto), akizindua kisima walichomjengea msanii mahiri wa mashahiri, Mrisho Mpoto kushoto) katika kijiji chake huko Mkuranga leo Jumamosi

Na Mwandishi Wetu, Mkuranga
SERIKALI ya Kuwait imeahidi kuwasaidia wananchi wa kijiji cha Kibogolwa kitongoji cha Kibamba Mkuranga mkoani Pwani, ili kuharakisha maendeleo katika eneo hilo.

Hayo yalisemwa leo na Balozi wa nchi hiyo nchini Tanzania, Jasem Alnajem wakati akizindua kisima kirefu kilichojengwa
 katika shamba la msanii nguli wa mashahiri, Mrisho Mpoto ``Mjombakijijini hapo.
Mrisho Mpoto akizungumza katika kijiji cha Kibogolwa, Kibamba Mkuranga leo wakati balozi wa Kuwait akizindua kisima katika mradi wa msanii huyo wa Kutoka Shambani.
Kisima hicho ni sehemu ya mradi wa Kutoka Shambani wa Mjomba uliopo katika zaidi ya hekali 40 akiwa na lengo la kuanzisha shughuli kubwa za kilimo kwa vijana wasio na mbele wa nyuma.

Balozi Alnajem akijibu risala ya mwenyekiti wa kijiji hicho, Salima Mussa aliyesema wanakabiliwa na matatizo kibao yakiwemo ya watoto wao kusoma mbali, kutokuwa na msikiti, zahanati na barabara mbovu.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem alnajem akifungua maji na watoto wakati wa kuzindua kisima Mkuranga leo.
Alnajem alisema suala la zahati watalidajili ili kuona jinsi gabi watakavyo lishughulikia wakati lile la madrasa na msikiti alisema hilo hakina shaka watapajengewa mara moja.

Karibu kaya 150 zitanufaika na maji hayo, ambayo kisima chake kimegharimu kiasi cha zaidi y ash. Milioni 12.

Mratibu wa Mpoto Foundation, Mwalimu Steph (kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhiwa kisima na balozi wa Kuwait, Jasem alnajem (kulia) katika kijiji cha Kibogolwa leo Jumamosi.
Naye mratibu wa mradi huo uliopo chini ya Mpoto Foundation, Mwalimu Steph aliushukuru ubalozi wa Kuwait kwa kuwachimbia kisima hicho na kukubali kutatua matatizo mbalimbali ya taasisi hiyo pamoja na yake ya wanakijiji.

Alisema kuwa mradi huo utasaidia kukomboa vijana wengi ambao hawana cha kufanya mitaani na kubaki kujiingiza katika masuala ya dawa za kulevya na ulevi mwingine.

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania baada ya kumtwisha ndoo ya maji mwanakijiji mmoja wa kibogolwa leo Jumamosi baada ya kuzindua kisiwa kilichojengwa kwa msaada wa nchini yake.
Nao wananchi wa eneo hilo wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti waliishukuru Kuwait na kusema maji hayo yatawapunguzia sana na matatizo ya kwenda mbali kuchota majia, ambayo pia hayakuwa salama.

Mussa alisema kuwa walikuwa wakitumia muda mwingi kwenda kusaka maji na kushindwa kufanya kazi zingine za kimaendeleo.
 
Katika mradi wa Kutoka Shambani, Mpoto kwa kuanzia ataanza na vijana 50, ambapo tayari kuna maombi ya vijana 3,500 wanaotaka kuingia katika mradi huo, utakaowawezesha kujifunza kilimo na sanaa.

 
 
 
 

 

No comments:

Post a Comment