Na Waandishi Wetu
MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga jana ilipoteza mchezo wa kwanza katika ligi hiyo baada ya kufungwa mabao 2-0 na Costal Union, huku watani zao Simba wakiondoka na pointi zote tatu dhidi ya African Sports kwa ushindi wa mabao 4-0.
Simba iliyocheza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ilipata bao lake la kwanza dakika ya 14 kupitia
kwa mshambuliaji Mganda, Hamisi Kiiza aliyefumua shuti kali kwa mguu wa kushoto
baada ya pasi ya beki Hassan Kessy.
Kessy mwenyewe akafunga dakika ya 30 kuipatia Simba
SC bao la pili kwa shuti la mguu wa kulia akimalizia pasi ya mshambuliaji
Ibrahim Hajib na kumchambua vizuri kipa Zakaria Mwaluko.
Kiiza akamlamba chenga kipa Mwaluko baada ya kupata
pasi ya kiungo Mwinyi Kazimoto kuifungia Simba SC bao la tatu dakika ya 42.
Hajji Ugando akaifungia Simba SC bao la nne dakika ya
75 baada ya kupokea nzuri ya kiungo aliyekuwa katika kiwango kizuri.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Hassan
Kessy, Abdi Banda, Juuko Murshid, Hassan Isihaka, Justice Majabvi, Mwinyi
Kazimoto/Mussa Mgosi dk86, Jonas Mkude,
Haji Ugando/Said Ndemla dk76, Ibrahim Hajib na Hamisi Kizza/Brian Majwega dk67.
African Sports; Zakaria Mwaluko, Mwaita Gereza,
Halfan Twenye, Juma Shemvuni, Rahim Juma, Mussa Chambega/Hussein Amir dk51,
Ally Ramadhani, Pera Ramadhani, Hamad Mbumba, Rajab Isihaka na James
Mendy/Mohammed Issa dk56.
KWA UPANDE WA YANGA:
Yanga imefungwa mabao 2-0 na Coastal Union Uwanja
wa Mkwakwani, Tanga na matokeo hayo yanawafanya wabaki na pointi zao 39 baada
ya kucheza mechi 16, sawa na Azam FC iliyocheza mechi 15.
Coastal Union walipata bao lao la kwanza dakika ya 27
kupitia kwa beki wa zamani wa Simba, Miraj Adam aliyefunga kwa shuti la
mpira wa adhabu lililomparaza mikononi kipa Deo Munishi ‘Dida’ kabla ya kutinga
nyavuni.
Refa Andrew Shamba wa Pwani aliwapa nafasi ya kupiga
faulo Coastal Union, baada Miraj Adam mwenyewe kuangushwa na beki wa Yanga,
Kelvin Yondan nje kidogo ya boksi.
Mshambuliaji chipukizi, Juma Mahadhi aliifungia bao
la pili Coastal Union dakika ya 62 baada ya pasi nzuri ya Hamad Juma.
Bao hilo liliwavunja nguvu kabisa wachezaji wa Yanga
SC na kujikuta wanacheza bila malengo. Refa Andrew Shamba alimtoa kwa kadi
nyekundu beki wa Yanga, Kevin Yondan dakika ya 100.
Awali, dakika ya 97 Shamba alijichanganya kwa
kumuonyesha kadi nyekundu Said Jeilan badala ya njano.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deogratias Munishi,
Juma Abdul, Oscar Joshua, Kelvin Yondan, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon
Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Paul Nonga dk76, Donald Ngoma na Deus
Kaseke/Issoufou Boubacar dk80.
Coastal Union; Fikirini Bakari, Hamad Juma, Adeyoum
Ahmed, Said Jeilan, Miraji Adam, Sabo Youssouf, Juma Mahadhi/Omar Wayne dk86,
Ayoub Yahya/Mtenge Juma dk97, Chidiebele Abasarim, Ally Ahmed na Ismail Mohammed.
No comments:
Post a Comment