KIGALI, Rwanda
JAMHURI ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ilihitaji
muda wa ziada kuwaondosha wenyeji Rwanda katika mashindan ya Mataifa ya Afrika
kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani (Chan), baada ya kuibuka na ushindi
wa mabao 2-1 katika mchezo wa robo fainali jijini hapa.
Doxa Gikanji aliipatia Congo bao la kuongoza dakika
10 tangu kuanza kwa mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Amohoro.
Hatahivyo, wenyeji walisawazisha dakika 12 baada ya
mapumziko kwa bao lililowekwa kimiani na Ernest Sugira.
Padou Bompunga aliifungia Congo bao la ushindi katika
muda wa nyongez na hiyo ikiwa na maana kuwa washindi hao sasa watakutana ama na
Zambia au Guinea katika nusu fainali itakayopigwa Jumatano.
Congo, ambayo iliwahi kutwaa taji hilo mwaka 2009,
ilipata uongozi wa mchezo wakati Rwanda iliposhindwa kuokoa vizuri mpira na mpira
huo kuangukia kwa Gikanji aliyekuwa nje ya eneo la hatari na kupiga shuti kali
na kumuacha kipa wa Rwanda Eric Ndayishimiye akishindwa kuokoa shuti hilo.
Dakika tisa baadae, huku Chui hai wa Congo wakiwa
wametawala, Jonathan Bolingi alipiga shuti lililogonga mwamba.
Bao la kusawazisha la Rwanda la kipindi cha pili
lilipatikana kutoka kwa Sugira likiwa ni bao lake la tatu.
Mchezaji huyo alifunga bao hilo baada ya kufanikiwa kuwa
nyuma ya mabeki wa Congo, na kupiga shuti lililompita kipa Ley Matampi.
Muda mfupi baadae mchezaji huyo nusura afunge baada
ya kuitoka beki ya Congo na Matampi akiwa yeye na kipa, alipiga juu ya wavu wa
goli.
Timu zote zilishambuliana kwa zamu kabla ya filimbi
ya mwisho, lakini hadi dakika 90 za kawaida za mchezo zinamalizika, timu hizo
zilikuwa sare ya bao 1-1.
Wakati muda ukiendelea kuyoyoma watu wakitarajia timu
hizo zitapigiana penalty kumpata mshindi, Bompunga alipiga mpira wa kichwa cha
nyuma na mpira kumpita Ndayishimiye.
No comments:
Post a Comment