MELBOURNE, Australia
MCHEZAJI Angelique
Kerber huku akishangiliwa na mashabiki kwenye Uwanja wa Rod Laver Arena leo
Jumamosi usiku ikiwa ni zaidi ya saa mbili alikiangusha kigogo Serena Williams
na kutwaa taji la micbuano ya tenisi ya Australian Open.
Kerber alimchapa
Serena ambaye ni bingwa namba moja kwa ubora katika mchezo huo duniani kwa
upande wa wanawake kwa 6-4, 3-6, 6-3. Ni taji la kwanza kubwa kwa Kerber, na ni
la kwanza kwa mchezaji wa Ujerumani katika karne hii.
Kerber, ambaye
ana umri wa miaka 28 na ni mwaka wake wa 14 katika katika mchezo huo, alikuwa
akicheza fainali yake ya kwanza ya mashindano makubwa, ambapo alianza mmchezo
huo kwa kuokoa mpira uliopigwa na bingwa huyo mara 21, kabla hajafanya matokeo
ya kuongoza kwa 2-0.
Bingwa
huyo alijikuta mipira mingi aliyoipiga iliishia kwa Kerber, na Kerber alifanya
kweli na kuendelea kumsambaratisha mpizani wake.
Williams lionesha
kuzinduka katika seti ya pili baada ya kucheza vizuri na kumuwezesha kufikia
hatua hiyo bila ya kupoteza seti hiyo. Mchezo huo uliendelea na mshindi
kuamriwa katika seti ya tatu.
Mashabiki
walipagawa baada ya Kerber akipomsambaratisha Williams katika mchezo wa kwanza.
Ilikuwa
ni kawaida kwa mashabiki uwanjani hapo kulipuka kwa furaha kwa kumshangilia Kerber.
Mashabiki wa mchezo wa tenisi wa Australia mi kawaida yao kumshangilia mchezaji
asiyepewa nafasi ya kushinda, lakini Williams alisema kuwa huo ni uwanja anbo
amekuwa akihisi kupendwa sana.
Williams aliwaambia
waandishi wa habari Alhamisi kuwa, ilikuwa miujiza kucheza fainali hapa. Baada
ya kushinda hii na mataji mengine mawli makubwa
mwaka jana. Alitarajia kuanza taratibu mashindano hayo. Alikuwa nje ya
uwanja kwa miezi minne akiuguza maumivu ya kufungwa katika nusu fainali ya
mashindano ya U.S. Open. Alitarajia kuanza taratibu, alisema.
No comments:
Post a Comment