Sunday, 19 July 2015

Majura arejesha fomu ya Ubunge na kuahidi kuendeleza michezo Kawe



Na Mwandishi Wetu
Mwandishi wa habari na mtangazaji maarufu nchini, Abdallah Idrissa Majura leo ameahidi kufanya mapinduzi ya michezo katika Jimbo la Kawe ambao utakuwa ni mfano kwa maeneo mengine na taifa kwa ujumla.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kurejesha fomu za kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema endapo atapendekezwa na kisha kuchaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo, ataanza na michezo mitano ambayo ni soka, mpira wa kikapu, netiboli, wavu na mpira wa mikono.

"Mungu akinijaalia nikatimiza ndoto yangu ya miaka mingi nitaanza na michezo hii ambapo tutaunda timu moja yenye wachezaji mahiri katika kila mchezo na zote zitajulikana kwa jina moja tu Kawe United," alisema mtangazaji huyo ambaye pia ni mwanamichezo maarufu.

Alisema amekuwa akishangazwa kuona michezo kama mpira wa kikapu, netiboli, wavu na mpira wa mikono haipigi hatua wakati haina gharama kubwa za uendeshaji kulinganisha na soka, ambayo licha ya kuhitaji fedha nyingi pia kuna ubabaishaji mkubwa ambapo viongozi wengi wanaoungoza mchezo nia yao ni kujinufaisha wenyewe binafsi.
 
Alisema kwa sasa hawezi kuweka wazi mikakati atakayotumia kuiinua michezo hiyo kwakuwa wakati wa kampeni haujawadia.Hata hivyo  amesema ameamua kuanza na michache kwa sababu kipindi cha miaka mitano ni kidogo hivyo kama atabeba mzigo wa mambo mengi atashindwa kutimiza ahadi zake.

Mtangazaji huyo ambaye anamiliki kituo cha ABM FM RADIO cha mkoani Dodoma amesema dhaimira yake ya kuinua michezo ilianza tangu mwaka 2010 alipoanzisha kituo hicho ambacho kinaongoza nchini kwakuwa na vipindi vingi vya michezo kulinganisha na radio nyingine.ABM ina kipindi cha michezo kila baada ya saa moja.

Kuhusiana na changamoto ya viwanja, mtangazaji huyo ambaye ameweka rekodi ya kushinda tuzo za michezo za Baraza la Habari Tanzania (Ejat) kwa miaka mitatu mfululizo huku mwandishi wake akishinda tuzo zilizopita, amesema anao mkakati wa kuandaa uwanja mmoja ambao utatumia na timu zote za jimbo la Kawe kwa ajili ya kufanyia mashindano.

"Kama nitapendekezwa na kisha kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Kawe nimekusudia kuwashirikisha viongozi wenzangu jimboni tuuzungushie maduka uwanja wa Tegeta Nyuki kisha tuuwekee majukwaa kama Azam Complex, naamini utakuwa ni chanzo kizuri cha mapato ya jimbo na pia wanamichezo kuutumia.

Mgombea huyo amesema ameuchagua uwanja huo wa Tegeta Nyuki kwakuwa ni mkubwa na pia ni rahisi kufikiwa na wanamichezo kutoka sehemu mbali mbali kwani mabasi ya dalala dala yanaanzia hapo kwenda maeneo ya Kariakoo na Ubungo.

Majura ambaye pia amewahi kushinda tuzo ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (Taswa) 1997/98 zipo njia rahisi za kupata fedha za kujenga maduka ya kuzunguka uwanja huo pia kutengeneza majukwaa na kuahidi mbinu hizo kuziweka hadharani pindi kampeni zitakapoanza rasmi.

Mtangazaji huyo maarufu wa vipindi vya michezo ambaye amewahi kufanyakazi radio Tanzania,radio one/itv na BBC licha ya kuwa na diploma ya uandishi wa habari kutoka Chuo cha Uandishi wa Habari Tanzania (TSJ), pia anayo shahada ya kwanza ya Sayansi ya Jamii kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

 

Tuesday, 14 July 2015

Raheem Sterling kuvaa jezi namba 7 Manchester City



Mchezaji Raheem Sterling akionesha jezi namba saba atakayovaa Manchester City baada ya kukamilisha vipimo vya afya na kusaini mkataba wa kuanza kuitumikia timu hiyo, ambayo itamlipa mshahara wa pauni 180,000 kwa wiki.
LONDON, England
RAHEEM Sterling amekamilisha uhamisho wake kwenda Manchester City wa kitita cha pauni milioni 49 huku yeye akiondoka na pauni 180,000 kwa wiki kama mshahara wake.

Mchezaji huyo ambaye alipokuwa Liverpool alikuwa akilipwa chini ya pauni 80,000 na baadae kuahidiwa kuongezwa hadi 100,000 kama angeendelea kuitumikia timu hiyo, aligoma kubaki Anfield.
Raheem Sterlin akiwa na timu ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano ya Man City.
Mwakilishi wa Sterling, Aidy Ward alizungumza hadharani kuwa mchezaji huyo hakuwa na furaha hapo Anfield wakati wakielekea mwishoni mwa msimu uliopita, ambapo alisema kuwa mcheaji wake hata akiongezwa pauni 900,000 kwa wiki, hatabaki Liverpool.

Ward pia alidai kuwa kiungo huyo hakuwa na uhusiano mzuri na kocha wake Brendan Rodgers, lakini madai hayo yalikanushwa na kocha huyo wa Liverpool.
 
Lakini kufuatia vipimo vya afya katika klabu ya Man City, Sterling aliuambia mtandao wa klabu hiyo: ‘Napenda kuwashukuru watu wote wanaonizunguka, mama yangu na dada zangu, uongozi wa timu, na Aidy Ward kwa kunisaidia na kufika nilipo leo. 

Nimefurahi kwa mambo yote kukamilika.

Sterling mwenye umri wa miaka 20, aliweka wazi nusu ya pili ya msimu kuwa, hana mpango wa kuongeza mkataba Liverpool na katika mahojiano katika televisheni Aprili mwaka huu kuwa kinachomuondoa Liverpool sio pesa.

Laklini, baada ya kukamilisha kuondoka Liverpool, Sterling ametumia muda wake kumpongeza Rodgers.

‘Napenda kumshukuru Rafa Benitez kwa kunipeleka Liverpool wakati nikiwa na umri wa miaka 15 na Kenny Dalglish for kwa kuonesha imani kwangu wakati nikiwa na umri mdogo.
 
Mwisho napenda kumshukuru Brendan Rodgers kwa kunipatia nafasi ya kudumu katika timu ya kwanza na kukionesha duniani kipaji changu.

Sterling, atakayevalia jezi namba 7 katika timu hiyo yenye maskani yake kwenye uwanja wa Etihad na kufuzu vipimo vya afya kabla yakusaini mkataba mpya ambao utamuwezesha kuondoka na pauni 180,000 kwa wiki, alisema anaangalia mbele kukutana na wachezaji wenzake wapya.

Mchezaji huyo alikiri kuwa alizungumza na kipa Joe Hart kuhusu kuhamia katika klabu hiyo wakati walipokutana katika timu ya taifa ya England.

Monday, 13 July 2015

Casillas aaga akiondoka zake Real Madrid baada ya miaka 25

Kipa wazamani wa Real Madrid Iker Casillas, akiwa mbele ya mataji aliyotwaa na timu hiyo kwa vipindi tofauti alivyokuwa akiichezea timu hiyo, ambapo jana alikuwa na mkutano na waandishi wa habari kabla ya kwenda kujiunga na Porto ya Ureno. Casillas ameichezea Real kwa miaka 25 mfululizo.

Sunday, 12 July 2015

Serena Williams, Novak Djokovic katika bonge la pati la ushindi



Serena Williams akipozi na kivazi chake.


LONDON, England
BAADA ya kushinda mataji ya tenisi ya Wimbledon, bingwa kwa upande wa wanawake Sereina Williams na Novak Djokovic kwa wanaume, jioni ya jana walitinga katia pati wakiwa na vivazi tofauti na vile walivyozoeleka kuonekana navyo uwanjani.

Katika pati hiyo kubwa bingwa mtetezi Novak Djokovic aliyemshinda bingwa mara saba Roger Federer, alitinga akiwa amevali suti huku Williams gauli refu `maksilangi ya maziwa.

Hilo ni taji la tatu la mashindano ya Wimbledon na ni la tisa kubwa kwa Djokovic wakati Serena akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mkubwa kutwaa taji la mashindano makubwa kwa upande wa wanawake.

Williams alitimixza miaka 33 na takribani siku 289 Jumamosi wakati akimfunga Garbine Muguruza wa Hispania kwa seti 6-4, 6-4 na kukamilisha taj lake la 21 kwa mchezaji mmoja mmoja na kujiweka vizuri kumaliza kalenda ya mashindano makubwa vizuri wakati atakaposhiriki US Open.
Serena Williams.

Serena Williams (kushoto) na Novak Djokovic

Wakali hao wakiwa na mataji hayo wakati wa pati hiyo ya ushindi.
 
Serena Williams katika kivazi alichozoeleka kuonekana nacho.

Saturday, 11 July 2015

Hatimaye Van Persie aondoka Man United na kwenda Fenerbahce



LONDON, England
HATIMAYE mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Robin van Persie kwenda Fenerbahce umekamilika, kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Uturuki.

Mwenyekiti wa Fenerbahce Aziz Yildirim alisema kuwa makubaliano yalikamilika tangu Ijumaa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, leo Jumapili anatarajia kutua Istambul kwa ndege binafsi kwa ajili ya kukamilisha taratibu za mwisho za usajili wake.

"Tulifanya kazi kwa nguvu, hadi usiku wa manane. Hatima ye tumefanikiwa kumsajili mcheaji huyo," alisema Yildirim alipokaririwa na gazeti moja.

"Uhamisho wa van Persie umefanyika na nyota mmoja zaidi ametua katika timu ya Fenerbahce.

Van Persie Alhamisi alifanyiwa vipimo vya awali vya afya England na alitarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne wa kuitumikia klabu hiyo ya Uturiki, lakini uhamisho rasmi ulikuwa nado haujathibitishwa.