Na
Mwandishi Wetu
JENGO
la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA-TB III) litaongeza chachu ya kukua kwa uchumi wa nchi, imeelezwa.
Hayo
yamesemwa leo na Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania alipozindua jengo hilo, ambalo sasa limeanza kutumika kwa safari za nje
ya nchi baada ya kukamilika kwake.
Rais
Magufuli amesema mbali na jengo hilo litatoa ajira mbalimbali kwa wazawa, pia
litaruhusu wananchi kuwekeza katika huduma mbalimbali ndani na nje ya jengo
hilo, ambapo ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuhakikisha
Wazawa wanapewa kipaumbele katika uwekezaji katika jengo hilo.
“Serikali
inaimarisha usafiri wa anga kwa kununua ndege pamoja na kuimarisha miundombinu
ya viwanja vya ndege, ambapo serikali inampango wa kukarabati na kujenga
viwanja 15 nchini kikiwepo cha Kimataifga cha Msalato Dodoma, ili kuendelea
kuufanya usafiri huu uendelee kuwa wa haraka na salama, ambapo utachangia
kukuza pato la taifa kwa watumiaji wake, ambao kwa sasa abiria wameongezeka kwa
asilimia 12 kwa mwaka,” amesema Mhe. Rais.
Amesema
anaimani idadi ya abiria wa ndege wataongezeka zaidi kutokana na utalii
unakwenca sambamba na usafiri wa anga, kutokana na Watalii wengi huja nchini
kwa kutumia usafiri wa anga.
Hatahivyo,
ameipongeza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, pamoja na Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kwa
kufanikisha kukamilika kwa mradi huo mkubwa wa jengo hilo, ambao mwaka 2016
ulisuasua kutokana na kukosekana kwa fedha za kuendelea na mradi.
Amewataka
Watanzania kulipa kodi ili serikali iweze kukamilisha mapema kwa wakati miradi
mikubwa, ambayo itakuja kuwanufaisha na kuwapa heshima kubwa.
“Miradi
inawezekana kwani fedha nyingi zilikuwa zikitumiwa na mafisadi, hivyo nawataka
tulipe kodi ili kufanikisha miradi yote, na tuachane na dhana ya wafadhili
ambao wamekuwa na masharti,” amesema Mhe. Rais.
Hatahivyo,
amewataka watumiaji wote wa Jengo hili kuhakikisha wanalitunza na wasiliharibu
kutokana na kujengwa kwa fedha nyingi za Watanzania.
Katika
hatua nyingine amempongeza Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Kikwete
aliyeanzisha ujenzi wa mradi wa Jengo la Tatu la abiria, na pia amewashukuru
viongozi wa Dini nchini kuendelea kuliombea taifa.
Naye
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema
kutokana na ongezeko la mara kwa mara la abiria, sasa Jengo la pili la abiria
(JNIA-TBII) linaboreshwa na kukarabatiwa ili liweze kuhudumia abiria mara mbili
ya sasa ambao ni Milioni 1.5 kwa mwaka.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi Julius Ndyamukama amesema TAA wapo tayari
kuendesha huduma kwenye jengo hilo, ambapo wamefanya majaribio kadhaa ya ndege,
ambapo tarehe 17 Julai, 2019 walianza na ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania
(ATCL), iliyokuwa ikizindua safari yake ya kwanza kwenda nchini India.
Kwa
upande wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai
amesema jengo hili la kisasa linaitoa Tanzania kimasomaso, kutokana na ukubwa
na ubora wake.
“Nipo
hapa kuwawakilisha Wabunge, ambapo tunaona fedha tunazopitisha zinatumika
kihalali na tutaendelea kumuunga mkono Mhe. Rais katika jitihada zake za
kuendeleza na kuanzisha miradi mbalimbali,” amesema Mhe. Spika.
Naye
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma ame wataka wananchi kuhakikisha
wanatatua migogoro yao ya ardhi inayohusisha ujenzi wa miradi mbalimbali nje ya
mahakama, ili kufanikisha miradi hiyo kumalizika kwa wakati.
No comments:
Post a Comment