Wateja kuendelea kushuhudia burudani kabambe kwa bei
‘mtelezo’!
DStv Tanzania imethibitisha rasmi kupunguza kwa kiasi kikubwa
ada ya mwezi ya vifurushi vyake kuanzia Septemba mosi mwaka huu.
Mabadiliko hayo yanakuja muda mfupi tu baada ya kuanza kwa msimu
wa soka, ambapo ligi kubwa maarufu diniani zimeanza, hivyo kuwawezesha wateja
wa DStv kushuhudia ligi hizo kwa bei nafuu kabisa.
Akithibisha punguzo hilo la bei, Mkurugenzi Mtendaji wa
MultiChoice Tanzania, Jacqueline Woiso amesema kuwa muda wote wamekuwa
wakisikiliza maoni ya wateja wao na moja ya mambo wateja waliyoshauri ni
kupunguzwa kwa bei za vifurushi.
“Wateja ndiyo moyo wa biashara yetu na muda wote tunawasikiliza
na kutekeleza maoni yao pale inapowezekana. Kwa msingi huu, tumeamua kupunguza
bei ili wateja wetu waendelee kufurahia burudani kabambe kwa bei nafuu zaidi, “
alisema Jacqueline.
Mchezaji wazamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Edibily Lunyamila akizungumza hivi karibuni. Kulia ni mchezaji mwenzake wazamani wa Yanga na timu ya taifa, Sekilojo Chambu. |
Amezitaja bei hizo mpya kuwa kifurushi cha DStv Premium kutakuwa
na punguzo la Sh 40,000 kutoka bei ya sasa ya Sh 169,000 hadi 129,000;
Kifurushi cha DStv Compact+ punguzo la Sh 25,000 kutoka 109,000 hadi
84,000; Kifurushi cha DStv Compact
punguzo la Sh 25,000 kutoka 69,000 hadi
44,000; na kifurushi cha DStv Family punguzo la Sh 10,000 kutoka 39,000
hadi 29,000.
Kuhusu vifurushi maalum, Jacqueline amesema kifurushi chenye
nyongeza maalum ya chaneli za Asia - DStv Premium+Asia Addon kitapungua kwa
shilingi 40,000 kutoka 220,050 hadi 170,050 wakati kile chenye chaneli za ziada
za Kifaransa DStv Premium+French addon nacho pia kitapungua kwa 40,000 kutoka
259,000 hadi 2019,000.
Mkurugenzi huyo amewahakikishia wateja wa DStv kuwa kushuka huko
kwa bei hakutasababisha mabadiliko wa chaneli katika vifurushi hivyo mteja
ataendelea kupata chaneli zile zile alizokuwa akipata awali ila sasa atakuwa
analipa bei ndogo zaidi.
No comments:
Post a Comment