Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya kuifunga Kakamega Home Boyz kwa penalti 5-4. |
Na Mwandishi Wetu, Nakuru
TIMU ya soka ya Simba leo imekata tiketi ya kucheza
fainali ya mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Kakamega Home
Boyz kwa penalti 5-4, katika mchezo ulipigwa kwenye Uwanja wa Afraha mjini
hapa.
Ushindi wa mabingwa hao wapya wa Tanzania Bara,
haukuwa rahisi kwani walihitaji kutoka jasho na damu baada ya vijana wa
Kakamega kuwang’ang’ania na kulazimisha suluhu hadi dakika 90 za kawaida
zinamalizika na kufanya mchezo hu kwenda katika matatu.
Waliofunga penalti za Simba Sports jana ni Haruna
Niyonzima, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, Shiza Kichuya na Jonas Mkude, wakati penalti
ya mwisho ya Kakamega iliota mbawa baada ya mpigaji kupaisha.
Simba SC sasa Jumapili katika fainali na bingwa wa
Kenya na mshindi wa mwaka jana wa SportPesa Super Cup, Gor Mahia baada ya jana
kuifunga Singida United 2-0.
Ikumbukwe mchezo wa kwanza pia Simba ilipenya kwa
matuta, ikishinda kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Kariobangi Sharks
nayo ya Kenya, kabla ya kuendeleza ushindi wa staili hiyo mbele ya Kakamega
iliyowatoa Yanga ya Tanzania pia kwa
kuwachapa 3-1.
Fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup 2018
itafanyika Jumapili na mshindi pamoja na kupata dola za Marekani 30,000 pia
atapata nafasi ya kwenda kucheza na klabu ya Everton kwenye Uwanja wa Goodison
Park mjini Liverpool, England.
Mshindi wa pili atajipatia dola za Marekani 10,000,
wa tatu dola 7, 500 na wa nne dola za Marekani 5,000 wakati timu nyingine
zitapewa kifuta jasho cha dola 2,500.
Bingwa mtetezi ni Gor Mahia ambayo mwaka jana
iliifunga AFC Leopards 2-1 katika fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na
mbali na dola na Kombe, pia ilipata nafasi ya kucheza na Everton kwenye uwanja
huo.
No comments:
Post a Comment