Tuesday, 7 August 2018

Manchester United Yagoma Kumuachia Pogba


MANCHESTER, England
KLABU ya Manchester United imetupilia mbali ofa ya Barcelona ya kiasi cha pauni milioni 45  ya kutaka kumnunua Paul Pogba pamoja na kuwatoa Yerry Mina na Andre Gomes, kwa mujibu wa Sky nchini Italia.MANCHESTER, England

KLABU ya Manchester United imetupilia mbali ofa ya Barcelona ya kiasi cha pauni milioni 45  ya kutaka kumnunua Paul Pogba pamoja na kuwatoa Yerry Mina na Andre Gomes, kwa mujibu wa Sky nchini Italia.

Taarifa hizo zinafuatia ripoti ya awali kutoka kwa wakala wa Pogba, Mino Raiola, ambaye alisafiri hadi mjini hapa katika jaribio la kutaka kumchukua mchezaji huyo wa Man United ili kwenda kwa mabingwa hao wa Hispania kwa ajili kiungo huyo Mfaransa.

Lakini United kwa sasa haina mpango wa kuachana na Pogba, ambaye ndio kwanza amerejea katika mazoezi baada na kushinda taji la Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, alisajiliwa na Man United mwaka 2016 – kwa ada iliyokuwa rekodi ya dunia kwa wakati huo ya pauni milioni 93.25, na amebakisha miaka mitatu katika mkataba wake wa sasa.

Hata kama United itataka kumuuza mchezaji huyo, kesho Alhamisi ndio siku ya mwisho ya dirisha la usajili la Ligi Kuu ya England, ambapo wana siku mbili tu kumpata mchezaji atakayechukua nafasi yake.

Dirisha la usajili halitafungwa Hispania hadi Agosti 31, hiyo ikiwa na maana kuwa Barcelona wana nafasi hadi mwishoni mwa mwezi kujaribu kumsajili Pogba (pichani) katika kipindi hiki cha usajili.


Taarifa hizo zinafuatia ripoti ya awali kutoka kwa wakala wa Pogba, Mino Raiola, ambaye alisafiri hadi mjini hapa katika jaribio la kutaka kumchukua mchezaji huyo wa Man United ili kwenda kwa mabingwa hao wa Hispania kwa ajili kiungo huyo Mfaransa.

Lakini United kwa sasa haina mpango wa kuachana na Pogba, ambaye ndio kwanza amerejea katika mazoezi baada na kushinda taji la Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, alisajiliwa na Man United mwaka 2016 – kwa ada iliyokuwa rekodi ya dunia kwa wakati huo ya pauni milioni 93.25, na amebakisha miaka mitatu katika mkataba wake wa sasa.

Hata kama United itataka kumuuza mchezaji huyo, kesho Alhamisi ndio siku ya mwisho ya dirisha la usajili la Ligi Kuu ya England, ambapo wana siku mbili tu kumpata mchezaji atakayechukua nafasi yake.

Dirisha la usajili halitafungwa Hispania hadi Agosti 31, hiyo ikiwa na maana kuwa Barcelona wana nafasi hadi mwishoni mwa mwezi kujaribu kumsajili Pogba katika kipindi hiki cha usajili.

Kipa Chelsea Akaribia Kutua Real Madrid


LONDON, England
KIPA wa Chelsea, Thibaut Courtois, ambaye amekuwa akihusishwa na kutaka kuhamia Real Madrid, hajaripoti katika mazoezi ya timu hiyo ya Ligi Kuu ya England juzi.

Inaelezwa kuwa, the Blues hadi sasa hawajui lini kipa huyo wakimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 26, atarudi kundini katika kikosi hicho cha Chelsea.

Courtois amekuwa mchezaji wa Blues tangu mwaka 2011, wakati aliposajiliwa kutoka klabu ya Ubelgiji ya Genk na alichukuliwa kwa mkopo na Atletico Madrid.

Winga wa Chelsea, Eden Hazard naye pia amekuwa akihusishwa na Real, lakini Jumatatu hakuhudhuria mazoezi na klabu hiyo.

Courtois alitajwa kuwa kipa bora katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Urusi mwaka huu, ambako Ubelgiji iliifunga England katika mchezo wa kusaka mshindi watatu.

Ameichezea Chelsea mechi 154, akicheza mara 58 bila kufungwa.

Akizungumza juzi, kocha mpya wa Blues Maurizio Sarri alisema hana uhakika kama Courtois ataendelea kuwepo katika klabu hiyo.

Alisema: "Kwa sasa Courtois ni kipa wa Chelsea. Sijui huko mbele. Itategemea na klabu, hasa itamtegemea yeye mwenyewe ana msimamo gani na anataka nini, lakini ninategemea Courtois ataendelea kuwa kipa wetu.”

Taarifa zingine zinasema kuwa, Chelsea wako tayari kutoa kiasi cha pauni milioni 89 ili kumnasa kipa wa Atletico Madrid, Jan Oblak kama mbadala wa Thibaut Courtois kama kipa huyo ataondoka kwenda Real Madrid.

Kampuni ya Mawasiliano Yaahidi Gawio Zaid 2019


1.  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (mwenye suti nyeusi) hivi karibuni akiongea na Kamati ya maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane alipotembelea banda la Mamlaka kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.


Na Mwandishi Wetu, Simiyu
SHIRIKA la Mawasiliano nchini (TTCL), limeahidi kutoa gawio kubwa zaidi kwa serikali mwakani, ili fedha hizo zikasaidie katika kazi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege vya serikali.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba ambaye alitembelea banda la maonesho ya Kilimo la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, amesema wingi huo wa fedha utatokana na mashirika na taasisi za umma kuwaunga mkono kwa kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo.


1.    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Ofisa Mipango na Takwimu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Edward Kimaro alipotembelea banda la Maonesho ya Kilimo na sherehe za Nanenane la Mamlaka, yanafanyika kwenye Uwanja wa Nyakabidni mkoani Simiyu.

“Mwaka huu tulitoa gawio la sh. Bil 5.1 kwa serikali, lakini ninaimani mwakani tutatoa zaidi endapo tutapata ushirikiano wa kutumiwa kwa huduma zetu kutoka kwenye taasisi nyingine za serikali, ambapo fedha hizo zinasambazwa na serikali kwenye kazi mbalimbali ukiwemo wa ujenzi wa viwanja vya ndege,” amesema Bw. Kindamba.

Bw. Kindamba ameishukuru TAA kwa kuanza kutumia huduma ya mawasiliano ya simu kutoka kwenye shirika hilo, ambapo itasaidia kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi. 

Amesema anaahidi kuimarisha ushirikiano na TAA, na wapo tayari kutumia huduma zinazotolewa na mamlaka kwa maslahi ya nchini, ili kuimarisha na kukuza uchumi wa nchi.

1.        Baadhi ya wanakamati ya maonesho ya Kilimo na sherehe za Nanenane ya Mamlaka ya Viwanja wa Ndege Tanzania (TAA), wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) (mwenye suti).

“Ushirikiano wetu utasaidia kuongeza mapato, ambapo kila taasisi moja itaweza kutumia huduma na bidhaa za taasisi nyingine, kwa lengo la kuzifanya ziendelee kukua na kuimarika kiuchumi, kwani taasisi za umma zinategemeana zenyewe kwa zenyewe,” amesema.

Pia ameipongeza TAA kwa jitihada zake za kujitangaza kwa wananchi, ambapo ameitaka kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege.
Ofisa Biashara na Masoko wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi. Herieth Nyalusi (kulia) akitoa maelezo ya ujenzi wa kiwanja kipya cha ndege cha Mkoa wa Simiyu kwa Bi. Grace Kenedy (kulia) na Bi.Magreth Lend wakazi wa Bariadi, walipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa Nyakabindi.
“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kujitangaza, naomba muendelee kuboresha viwanja vya ndege kwa maslahi ya Watanzania wote, kwa kweli najivunia sana uwepo wenu katika Nanenane “I am proud of your success’ na kweli mna iunganisha Tanzania kwa Ulimwengu,” amesema Bw. Kindamba.

1.        Raia wa China wanaofundisha kwenye shule ya ya sekondari ya J.W.Bukanga Musoma, Bi. Jane Lee (wapili kushoto) na  Bi. Cary Zhang (watatu kushoto) wakimsikiliza Afisa Usalama Mwandamizi wa Mamlaka wa Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Bakari Mwalwisi alipokuwa akitoa maelezo kuhusu vimiminika kwenye banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la Mamlaka yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi, mkoani Simiyu. 



Sunday, 5 August 2018

RC Simiyu Afurahishwa na Maelezo ya Banda la TAA

      Mshauri wa Sera za Miundombinu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bi. Pudencia akimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela jana wakati akielezewa masuala mbalimbali alipotembelea banda la mamlaka hiyo katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Jumanne Sagini (wa pili kushoto) akipata taarifa ya ujenzi wa Kiwanja kipya cha Ndege cha mkoa huo kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Alex Kalumbete jana alipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto) jana akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (watatu kushoto) alipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la Mamlaka yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (aliyenyoosha mkono) jana akimwonyesha chati yenye viwanja 58 vya ndege Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la Mamlaka yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamati ya maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), jana alipotembelea banda la Mamlaka hilo katika Uwanja wa Nyakabindi. Kulia waliokaa ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela.

Rais Maduro wa Venezuela Anusurika Kuuawa


CARACAS, Venezuela
RAIS wa Venezuela, Nicolás Maduro anasema kuwa amenusurika kuuawa katika jaribio la mauaji yaliyohusisha ndege ndogo zisizo na rubani, ambazo zilibeba vilipuzi.

Maduro wakati huo alikuwa akihutubia katika hafla ya kijeshi jijini hapa wakati jaribio hilo la kumshambulia lilipotokea.

Rais Maduro na mkewe, Cilia Flores, ndio walilengwa katika shambulio hilo wakati akihutubia mamia ya askari jijini hapa.
 
Wawili hao, ghafla waliangalia juu kutoka stejini huku mamia ya askari wakikimbia kunusuru maisha yao baada ya kusikia sauti ya mlipuko na kutokea moshi mkubwa angani.

Picha zilionesha baadhi ya askari waliokuwepo katika eneo hilo wakivujwa damu.

“Matangazo mubashara `Live’ ya hotuba yake yanaonesha rais ghafla aliangalia juu, huku mamia ya askari wakikimbia kutoka katika mistari waliyokuwa wamejipanga wakisikiliza hutuba hiyo, “kilisema chanzo kimoja cha habari.

Bwana Maduro ameilaumu Colombia kwa shambulio hilo, dai ambalo limekanushwa na Bogota na kusema halina msingi wowote.

Askari saba waliumia, na watu kadhaa baadae walikamatwa, mamlaka ya Venezuela ilisema.

NINI KILITOKEA?
Tukio la shambulizi hilo, lilitokea wakati Bwana Maduro alikuwa akihutubia katika sherehe ya Kumbukumbu ya Jeshi kutimiza miaka 81.
 
Ndege mbili zisizo na rubani zikiwa na vilipuzi ziliruka jirani na jukwaa alikokuwa rais huyo akihutubia, alisema Waziri wa Mawasiliano Jorge Rodriguez.

Rais Maduro baadae akilihutubia taifa alisema: "Kuna kitu kilichokuwa kikiruka angani, kililipuka karibu yangu, mlipuko mkubwa. Dakika chache baadae kulikuwa na mlipuko wa pili.”
 
Picha katika mitandao ya kijamii zilionesha walinzi wakimlinda Bwana Maduro, huku wakiwa na ngao zisizopitisha risasi `bulletproof shields’ baada ya tukio hilo la uvamizi.

Rais huyo aliwatuhumu majirani zake Colombia na wapinzani wenye msimamo mkali wanaoungwa mkono na Marekani, kuwa ndio walitaka kumuua.

Aliongeza kuwa hana ‘wasiwasi’ Rais wa Colombia Juan Manuel Santos “alihusika katika jaribio hilo”.

Kiongozi huyo wa Venezuela, ambaye awali alikuwa akiituhumu Marekani kumpinga, hakuwa na ushahidi wowote kudhihirisha madai yake.

Hatahivyo, serikali ya Colombia imekanusha kujihusisha kokote na tukio hilo, ikisema kuwa madai hayo ya Bwana Maduro hayana msingi wowote.

Friday, 3 August 2018

Wakazi wa Simiyu Wapata Maelezo ya Ujenzi wa Kiwanja Kipya cha Ndege cha Mkoa Wao Kutoka Kwenye Banda la Maonesho ya 88 la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

Bi. Elizabeth Manoti mkazi wa Simiyu akisikiliza kwa makini maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa leo na Ofisa Tehama Mwandamizi, Bw. Geofrey Youze katika banda la maonesho ya Kilimo na sherehe za Nanenane la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayofanyika kwenye Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Mhandisi Alexander Kalumbete (mwenye kofia)  wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), akiwaeleza wakazi wa Mkoa wa Simiyu kwa kuwaonesha picha za Kiwanja kipya cha ndege kinachotarajiwa kujengwa eneo la Igegu mkoani hapa, leo walipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nyakabindi.

Wanafunzi kutoka shule ya Sekondari ya Ngulyati ya Bariadi mkoani Simiyu wakipata maelezo ya viwanja vya ndege kutoka kwa Mwanasheria Mwandamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi. Janet Mugini leo.

Ofisa Biashara na Masoko Mwandamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi. Herieth Nyalusi, akiwaeleza wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ngulyati ya Bariadi leo walipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la TAA, yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi.
Mtangazaji Fred Mwanjala wa Kituo cha televisheni cha Channel 10 akimhoji  Ofisa Mipango na Takwimu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Edward Kimaro leo alipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyakabindi.
Wananchi mbalimbali wakipata maelezo ndani ya banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu  leo. 
Ofisa Usalama Mwandamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Bakari Mwalwisi akielezea Bw. Geronimo Gelle wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) juu ya ubebaji wa vimiminika kwenye mizigo inayowekwa kwenye begi la mkononi.       

Mnangagwa Ashinda Kiti cha Urais Zimbabwe

HARARE, Zimbabwe
EMMERSON Mnangagwa (pichani) ameshinda Uchaguzi wa Rais, kwa mujibu wa Kamisheni ya Uchaguzi nchini Zimbabwe, imeelezwa.

Huku majimbo yote 10 yametangaza, Bwana Mnangagwa ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 50.3 dhidi ya mpinzani wake, Nelson Chamisa.

Polisi iliwaondoa viongozi wa wapinzani kutoka katika steji ya Kamisheni ya Uchaguzi wakati wakipiga matokeo.

Mwenyekiti wa Chama cha Bwana Chamisa cha MDC Alliance alisema kuwa kura hizo zilizotangazwa hazikuwa halali.

Rais huyo alishinda kwa asilimia ndogo ya 50 ya kura zote, na kumfanya Mnangangwa amefanikiwa kukwepa kufanyika kwa duru la pili la uchaguzi dhidi ya Chamisa.

Rais huyo alisema kuwa "amefurahi" alisema katika Twitter, na kusema kuwa matokeo hayo ndio mwanzo.

Bwana Chamisa alisisitiza ameshinda uchaguzi huo, aliwaambia waandishi wa habari mapema jana kuwa Chama Tawala cha Zanu-PF kilijaribu kubadili matokeo, kitu ambacho kamwe hawatakikubali.

Lakini Kamisheni ya Uchaguzi ya Zambabwe (Zec) ilisema hakukuwa na udanganyifu yoyote na uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Waandamanaji wa upande wa upinzani walifurika jijini Harare wakipinga matokeo hayo, ambapo watu sita wanadai kufa kutokana na vurugu hizo.

Uchaguzi huo ni wa kwanza kufanyika tangu mtawala wa muda mrefu Robert Mugabe, 94, kutolewa madarakani Novemba mwaka jana.

Sita Wauawa Vurugu za Uchaguzi nchini Zimbabwe

Mtu akipita katika moja ya mitaa mjini Zimbabwe pembeni ya duka lililovunjwa vioo na waandamanaji.

HARARE, Zimbabwe
MJI Mkuu wa Zimbabwe, Harare uligeuka mji wa vurugu, chini ya saa 24 baada ya watu sita kuuawa katika mapambano ya wapinzani na watu wa usalama kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumatatu.

Askari walitumia jana asubuhi kuondoa shughuli zote na kuwaonya watu kuondoka haraka hadi ifikapo mchana siku hiyo. Magari iliweka misururu mirefu, ambayo kila mmoja alikuwa akijaribu kupita.
Vijana wakileta vurugu baada ya Uchaguzi Mkuu wa Zimbabwe.

Maduka yalifungwa, huku polisi wa kuzuia ghasia waliizungua makao makuu ya chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change na kuzuia mitaani yote ua jirani.

Polisi iliwakamata watu 18 wakati walipoiweka chini ya ulinzi Makao Makuu ya MDC, ambapo msemaji wa Jeshi la Polisi la Zimbabwe, Charity Charamba alisema, bado mashtaka hayajawa tayari, lakini Charamba alisema tayari watu 26 wametiwa mbaroni wakituhumiwa kuleta virugu wakati wa maandamano juzi.
Askari akitokea kisago kwa raia mmoja aliyedaiwa kuleta vurugu.

Wakati wakitangaza idadi mpya ya watu waliokufa, ibidi wanajeshi kuingia mitaani baada ya hali kutokuwa nzuri na hivyo kuhitajika nguvu zaidi kutumika ili kuleta amani.


Thursday, 2 August 2018

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) watoa huduma kwenye maonesho ya Kilimo 88 mkoani Simiyu


Ramadhani Mawazo (kushoto) akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa maafisa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kutoka kulia Geofrey Youze, Mhandisi Alexander Kalumbete na Bakari Mwalwisi kwenye maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu. 
      Ofisa Usalama Mwandamizi wa Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bakari Mwalwisi (kushoto) akitoa maelezo yanayohusiana na ulinzi na usalama kwenye viwanja vya ndege kwa wakazi wa Simiyu waliotembelea banda la maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi.


   Mwanasheria Mwandamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi. Janeth Mugini (kulia) akimfafanulia mambo mbalimbali Bi. Grace Mgombera mkazi wa Simiyu alipotembelea banda la maonesho ya Kilimo Nanenane la TAA.
 Kikosi kazi cha maonesho ya Kilimo kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakiwa kwenye picha ya pamoja katika banda lao maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyakabindi.
Bw. Masaga Malika (kulia) akimsikiliza Mhandisi Alexander Kalumbete akimpa maelezo ya ujenzi wa Kiwanja kipya cha Ndege cha mkoa wa Simiyu, katika banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) katika maonesho ya Kilimo Nanenane.


Mhandisi Alexander Kalumbele (kulia) akitoa maelezo mbalimbali yanayohusu Viwanja vya Ndege Tanzania kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA), Bi. Vumilia Zikankub (wa pili kulia) aliyeongozana na Bw. Mikalu Mapunda, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara (kushoto) na Bw. Chambua Majuto (wa pili kushoto).   
 Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA), Bw. Mohamed Ally (mwenye miwani kushoto), alipotembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwenye viwanja vya maonesho ya Kilimo Nanenane, yanayofanyika Nyakabindi mkoani Simiyu.


Tuesday, 31 July 2018

Waziri Kamwelwe akagua ujenzi Terminal 3 JNIA na kumtaka Mkandarasi Kiwanja cha Msarato kuwasilisha nyaraka Tanroads

Sehemu ya Jengo jipya la Kiwanja cha Kimataifa cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA) Terminal 3 linavyoonekana kwa mbele.

Na Mwandishi Wetu
WAZIRI  wa Ujenzi, chukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe ametoa siku saba kwa Mhandisi mshauri katika ujenzi wa kiwanja kipya cha ndege cha Msalato Jijini Dodoma, kuwasilisha kwa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) nyaraka zote zinazohusu mradi huo kabla ya kuianza kazi aliyopewa.

Kamwelwe aliyasema hayo wakati alipotembelea alipotembelea ujenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA), Terminal 3 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya mafunzo tangu alipoteuliwa na Rais John Magufuli siku 11 zilizopita.
WAZIRI  wa Ujenzi, chukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe (kushoto) akisalimiana na Mhandisi Simba Bogohe wakati alipofanya ziara katika Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Kimataifa cha Ndege cha Juliue Nyerere. Kulia ni kaimu mkurugenzi wa JNIA, Paul Rwegasha.

Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais aliyetaka Tanroads kupewa usimamizi katika majukumu yote yanayohusu ujenzi.

Alisema hatua hiyo pia imelenga kwenda haraka na agizo jingine la juzi kutaka ujenzi wa kiwanja hicho kuanza mara moja, ili kuharakisha maendeleo ya Jiji hilo la Makao Makuu ya nchi, linaloanza kukua kwa kasi baada ya Serikali kuhamia huko rasmi hivi karibuni.

“Nina taarifa kuwa tayari TAA (Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania) mmeingia mkataba na mhandisi mshauri wa ujenzi wa kiwanja cha Msalato, hivyo natoa siku saba nyaraka zinazohusu ziwe zimepelekwa Tanroads kama mtu mwenye dhamana katika ujenzi wa uwanja huo,” alisema.
WAZIRI  wa Ujenzi, chukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Kimataifa cha Ndege cha Julius Nyerere, Paul Rwegasha.

Pia aliipongeza Tanroads kwa kusimamia vizuri ujenzi wa jengo hilo la abiria la Terminal 3, hatua aliyoitaja kuwa ni moja ya mipango ya Serikali kuona taasisi zake zinasimamia kikamilifu miradi ya maendeleo inayotekelezwa nchini ili kuendana na kasi ya maendeleo kuelekea nchi ya uchumi wa kati wa viwanda ifikapo 2025.

Aidha, Waziri Kamwelwe alisema Serikali imeridhishwa na ujenzi wa uwanja huo ambao ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Mei mwakani na kutoa fursa ya utatuzi wa changamoto ya muda mrefu la ufinyu na uhaba wa sehemu ya kiwanja cha ndege cha JNIA.
WAZIRI  wa Ujenzi, chukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe akitaniana na Meneja Mradi wa ujenzi wa jengo hilo la Terminal 3, Wolfgan Marschick.

“Tunampongeza mkandarasi anayejenga mradi huu, anafanya kazi nzuri nasi kama Serikali tumekuwa macho kufuatilia usiku na mchana bila hata ya kuchoka ili tuweze kufikia malengo, aliongeza.
Meneja wa Tanroads mkoa wa Dar es Salaam, Julius Ndyamukama akimuonesha mchoro wa Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Kimataifa cha Ndege cha Julius Nyerere Waziri Kamwelwe.

Alisema ujenzi wa uwanja huo ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuwahudumia abiria zaidi ya 2800 kwa saa na Milioni 6 kwa mwaka na hivyo kutatua changamoto iliyokuwepo kwa kiasi kikubwa.
WAZIRI  wa Ujenzi, chukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe (katikati mstari wa mbele) baada ya kumaliza ziara ya kutembelea Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Kimataifa cha Ndege cha Julius Nyerere.
 Awali, Mkurugenzi wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo, Wolfgang Marschick  mbali na mambo mengine  alimueleza Waziri kuwa moja ya changamoto anayokabiliana nao katika kutekeleza majukumu yake kuwa ni  kukwama kwa baadhi ya vifaa vya ujenzi katika Bandari ya Dar es Salaam,

Waziri alianza kulishughulikia suala hilo pale pale, ambapo alipiga simu kwa wahusika ili kuhakikisha vifaa hivyo, ambavyo alisema ni vidogo dogo lakini muhimu katika kukamilisha ujenzi huo vinatoka haraka ili kazi imalizike kwa wakati.