Saturday, 17 September 2016

Kongamano la Michezo lajadili kwa kina kuporomoka kwa michezo hapa nchini na kuibuka na jibu zito



Vyeti vya wakongwe wa michezo hapa nchini, Chabanga Hassan Dyamwale na Khalfa Abdallah.

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema kuwa kunatakiwa uwekezaji mkubwa kuendeleza michezo hapa nchini  ili kuzalisha ajira na kuongeza pato la taifa, imeelezwa.

Hayo yamo katika hotuba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye iliyosomwa na Mkuruenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Petro Lyatuu.

Washiriki wa Kongamano la michezo nchini wakiwa katika picha ya pamoja baada ya konamalo hilo kufunuliwa katika shule za Filbert Bayi Mkuza, Kibaha mkoani Pwani.
Nape alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kuendeleza michezo hapa nchini na mpango wa maendeleo wa taifa wa miaka mitano (2016-2017-2020-2021) unatambua Tanzania bado iko nyuma katika michezo na hivyo kunahitajika uwekezaji wa makusudi ili kuinua kiwango cha michezo hapa nchini.

Alisema kuwa mafanikio ya michezo hapa nchini katika miaka ya nyuma hayakuja kimiujiza, kwani kulikuwa na programu maalumu zilizowezesha vijana kushiriki katika michezo kama mashindano ya Shule za Msingi na Sekondari ya   Umitashumta na Umisseta.

Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), Amir Mhando akichania mada wakati wa Konamano la Michezo lililofanyika katika shule za Filbert Bayi Mkuza, Kibaha mkoani Pwani. Kushoto ni mwanariadha wazamani, Gidamis Shahanga.
Alisema kuwa vionozi wazamani wa michezo hawakuwa na tamaa wakati wa uongozi wao hawakuwa na tamaa ya fedha au madaraka waliyopewa ya kusimamia michezo kama ilivyojitokeza sasa katika klabu na taasisi zinazojaribu kufufua michezo hapa nchini.



Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Gulam Rashid alisema kuwa michezo hapa nchini ilishuka kuanzia katika miaka ya 1990 ukilinganisha na miaka ya 1970-80 huenda ilitokana na mifumo ya Serikali kuwa tofauti katika kuchangia michezo kwa ujumla.

Gulam alisema kuwa wakati huo kulikuwa na taasisi mbalimbali kama Mamlaka ya Bandari, Kampuni za Mafuta kama Esso, Majeshi (JWTZ), Polisi, JKT, Magereza, Uhamiaji zilikuwa na timu za michezo mbalimbali, ambzo zilileta ushindani na kusababisha kuendelea kwa michezo hapa nchini.

Alisema wanamichezo huandaliwa kuanzia chini, ambapo hakuna ubishi kuwa nazi hizi ni shuleni, ambako kulikuwa na vipindi vya elimu ya viungo kwa wanafunzi wetu.

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Muchezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Akichangia mada katika kongamano hilo, kaimu katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa, BMT, Mohamed Kiganja alisema upatikanaji wa viongozi wa michezo hapa nchini ni mbovu sana kiasi cha kuingiza watu wasio na uzalendo au kuongoza licha ya kuwa na elimu ya kutosha.

Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), Amir Mhando alisema viongozi wengi wa vyama vya michezo hawana hasa nia ya kuendeleza michezo ila wengi wao lengo lao ni kutaka kutoka kimaisha kupitia michezo.
Alisema wengi wamekuwa wakiingia kuongoza michezo ili kujitafutia njia ya kuingia katika siasa katika ngazi tofauti tofauti.
Mkurugenzi wa kwanza wa michezo nchini, Khalfa Abdallah akitoa neno la shukrani wakati wa ufunguzi wa kongamano la michezo nchini lililofanyika katika shule za Filbert Bayi Kibaha.
Mkurugenzi wa kwanza wa michezo mzalendo, Khalfa Abdallah alitaka kongamano hilo liwe chachu kwa makongamano mengine ambayo yanatakiwa kuandaliwa na Serikali ili kupata jibu la kufanya vibaya katika michezo.

Abdallah aliongoza ofisi hiyo kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1990 alipostaafu.

Baadhi ya wadau wengine wa michezo walioshiriki kongamano hilo ni pamoja na Leonard Thadeo aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Michezo nchini, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Makoye Nkenyenge, mkurugenzi wa Chuo cha Michezo cha TOC Suleiman Jabir, mkimbiaji wazamani Gidamis Shahanga na Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Petro Lyatuu akifungua kongamano la michezo Mkuza, Kibaha jana.
 Kongamano hilo linatarajia kumalizika leo, ambapo suluhisho la nini kifanyike ili kuendeleza michezo hapa nchini baada ya michezo kuporomoka kwa miaka mingi.
 Mkurugenzi wa kwanza wa michezo nchini, Khalfa Abdallah (kushoto) na meneja wa kwanza wa Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru), Chabanga Hassan Dyamwale wakiteta wakati wa mapumziko ya Kongamano la Michezo katika Shule za Filbert Bayi Kibaha jana.
 Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Mwenyekiti wazamani wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Anna Bayi akizungumza na mwanamichezo wazamani, Chabanga Hassan Dyamwale. Kushoto ni Mkurugenzi wa kwanza wa Michezo, Khalfa Abdallah.


Sunday, 11 September 2016

Bingwa wa Olimpiki Mo Farah abaguliwa na mfanyakazi wa Shirika la Ndege la Delta wakati akitoka Rio



LONDON, England
BINGWA wa Olimpiki wa mbio za meta 5,000 na 10,000 Mo Farah alijikuta katika wakati mgumu baada ya kubaguliwa na mfanyakazi wa ndege na kurudisha nyuma katika mstari kabla ya kupanda ndege kwenda Marekani, alisema mke wake.

Tania Farah alisema mfanyakazi wa Shirika la Ndege la Delta alimtilia ngumu bingwa huyo mara nne wa medali za dhahabu za Olimpiki na kugoma kabisa kuamini kama mwanariadha huyo ana tiketi ya daraja la pili (business class).

Hatahivyo, taarifa zingine zilisema kuwa Farah na familia yake hiyo walichelewa kupanda ndege wakati abiria wa daraja la kwanza walipokuwa wakiingia katika ndege.

Msemaji wa Delta Airlines alisema baadae kuwa wanachunguza madai hayo na "watalifanyia kazi moja kwa moja kwa kushirikiana na familia hiyo ya Farah".

Tukio hilo inadaiwa lilitokea Agosti 22 wakati wawili hao pamoja na watoto wao wanne wakirejea kutoka katika Olimpiki ya Rio 2016, ambako Farah alitetea mataji yake yam bio za meta 5,000 na 10,000.

Farah na familia yake walikuwa katika hatua za mwisho za safari yao kutoka Atlanta kurudi kwao Portland, Oregon.

"Najua alikuwa na tatizo na yeye, alisema.Tania Farah katika gazeti la Jumapili la Telegraph, akimnukuu mfnayakazi huyo wa Delta Airlines.

"Huyu manamke alimdharirisha hadi watu walipokuja na kusema: 'Huyi ni Mo Farah, ni bingwa wa Olimpiki,alisema mke wake.

Farah, 33, alitarajia kuwa mtu wa kwanza kushinda mara tatu mfululizo mbio za Great North Run wakati wa mbio hizo Newcastle leo Jumapili.

Angelique Kerber adhihirisha makali yake kwa kutwaa taji la US Open 2016 kwa kumfunga Karolina Pliskoya



 
NEW YORK, Marekani
MJERUMANI Angelique Kerber (pichani), aliendeleza makali yake kama bingwa namba moja kwa ubora duniani baada ya jana kuchapa Mczech Karolina Pliskova katika mchezo wa fainali ya mashindano ya US Open.

Kerber, 28, alishinda kwa 6-3 4-6 6-4 katika mchezo huo uliofanyika jijini hapa akiongezea taji la US Open katika taji lake la Australian Open alilolitwaa Januari.

Ushindi wa Pliskova katika nusu fainali dhidi ya Serena Williams tayari uimhakikishia Mjerumani huyo namba moja katika viwango vipya vya ubou zote zimekuwa kweli leo (jana) na ninachojaribu sasa ni kufurahia mafanikio yangu sasa, alisema Kerber.

Kerber hiyo ilikuwa ni fainali yake ya tatu ya mashindano makubwa mwaka huu, ambapo Mjerumani huyo alicheza huku akisubiri kutangazwa bingwa namba moja duniani katika viwango vya mchezo huo.

Wayne Rooney, Pep Guardiola nusura wazitwange kavu kavu wakati wa Manchester derby



Wayne Rooney.
MANCHESTER, England
NAHODHA wa Manchester United Wayne Rooney jana nusura azichape na kocha wa Man City Pep Guadiola wakati timu hizo zikipambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Huku Man United ikiwa nyuma kwa bao 1-0 mchezo huo ukielekea katika katika ya kipindi cha pili, Rooney alijaribu kuchukua mpira uliotoka baada ya kuchuana na mchezaji mmoja wa Man City.

Guardiola, akiwa katika eneo lake la ufundi, aliokota mpira huo na kuonekana kama alitaka kumpa mchezaji huyo.

Lakini Kocha huyo wa Man City alikataa kukabidhi mpira huo kwa Rooney na badala yake aliuweka nyuma ya mchezaji huyo ili asiuchukue haraka.

Rooney alijaribu kuuchukua mpira kwa nguvu, akionekana kupokonya mpira huo na kumsukuma Guardiola, kabla kocha huyo Mhispania kuwa mpole na kuuachia mpira huo.

Mwamuzi wa mchezo huo Mark Clattenburg, alikuwa mstaarabu pamoja na kushuhudia tukio hilo, kabla hajawashika mkono mmoja baada ya mwingine.

Man City ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Man United katika mpambano wa kwanza wa Manchester msimu huu, shukrani kwa mabao ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Kevin De Bruyne na Kelechi Iheanacho.

Zlatan Ibrahimovic aliipatia Man United bao la kufutia machozi muda Mfupi kabla ya mapumziko huku kikiwa hakia bao lolote.

Hicho ni kipigo cha kwanza kwa Man United chini ya kocha wao mpya Mreno Jose Mourinho.

Saturday, 10 September 2016

Bonanza la uzinduzi wa Mashindano ya Shimiwi 2016 lafana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Jumamosi



Washiriki wa Bonanza la uzinduzi wa mashindano ya Shimiwi wakipita katika barabara ya Mandera leo kuelekea Uwanja wa Uhuru.

Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu Kiongozi,  Balozi John Kijazi leo alikuwa mgeni rasmi katika Bonanza la uzinduzi wa mashindano ya 34 ya Shirikisho na Taasisi za Umma (Shimiwi), lililofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Utumishi, Lauriane Ndombaro akimkabidhi Kombe la ushindi wa kwanza Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva.
Kijazi ambaye hotuba yake ilisomwa na Katibu Mkuu wa Utumishi, Dkt Laurean Ndumbaro, ambayo iliwataka waajiri kuwatimizia mahitaji wafanyakazi wao ili waweze kujiandaa na kushiriki vizuri katika mashindano ya Shimiwi, ambayo mwaka huu yatafanyika Dodoma baadae mwezi ujao.

Alisema  kuwa waajiri wanatakiwa kuwa patia mahitaji muhimu kama vifaa vya michezo na mahitaji mengine ili wafanyakazi wao waweze kushiriki vizuri katika mashindano hayo, ambayo mwaka jana hayakufanyika ili kupisha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabune na Madiwani hapa nchini.
Dokta Mtaka akimchua mmoja wa washiriki katika bonanza hilo la ufunuzi wa Shimiwi leo Jumamosi.
 Kijazi pia alimpongeza Rais wa awamu ya tano wa Tanzania Dkt Pombe Maufuli kwa jitihada zake za kuliletea maendeleo ya haraka taifa la Tanzania, ambapo hadi sasa amefanya mambo mengi.
Pia aliwataka wafanyakazi hao wa umma kuwa na nidhamu wakati wote wa mashindano hayo ili kuonesha taswira nzuri kwa jamii.

Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakifanya mazoezi katika bonanza hilo leo.
Pia aliwataka wafanyakazi hao wa umma kufanaya mazoezi kila wakati sio kusubiri tu wakati wa bonanza hilo au mashindano ya Shimiwi kwani mazoezi uwajena kimiili na kiakili na kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
 
Aliwaambia kuwa michezo inawaepusha wafanyakazi hao wa Serikali na maonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu, kisukari, kupooza na mengine mengi.

Katika bonanza hilo viongozi mbalimbali wa wizara na taasisi mbalimbali za Serikali walishirriki katika bonanza hilo ambalo lilianza kwa washiriki zaidi ya 2,000 kukimbia katika mitaa mbalimbali ya jirani na Uwanja wa Uhuru na kurudi katika uwanja huo ambako walifanya mazoezi ya viungo kabla ya mgeni rasimu kuzungumza.
Mbali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Elisante Ole Gabriel, viongozi wengine waliokuwemo uwanjani hapo leo ni pamoja na katibu mkuu wa uchukuzi Dkt. Leornard Chamuriho (kulia) na katibu mkuu wa Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora.
 

Aidha, Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam (RAS) ndio ilitwaa ushindi wa kwanza katika shindano la taasisi iliyoshirikisha wafanyakazi wake wengi katika bonanza hilo la uzinduzi wa mashindano ya 34 ya Shimiwi baada ya kuwa na wafanyakazi 180 huku Kilimo walimaliza wa pili kwa kuwa na wafanyakazi 82.

Mwakilishi wa Kilimo (kulia) akipokea Kombe la ushindi wa pili kutoka kwa Katibu Mkuu Utumishi.
Washindi hao wa kwanza na pili walipewa zawadi ya makombe, ambayo yatakuwa yao kabisa.
Naye mwenyekiti wa Shimiwi Daniel Mwalusambi aliwashukuru viongozi wote waliowaruhusu wafanyakzi wao kushiriki bonanza hilo la uzinduzi wa mashindano ya Shimiwi.
 
Pia aliwataka kuwawezesha na kuwaruhusu kushiriki mashindano ya Shimiwi mkoani Dodoma mwaka huu.
Mwenyekiti wa Shimiwi, Daniel Mwalusambi akizungumza leo kwenye Uwanja wa Uhuru
MC wa Bonanza hilo la uzinduzi, ambalo lilifana, Joyce  Benjamin.