Na Mwandishi Wetu
BAADA ya kusibiri kwa muda mrefu, hatimaye Africa Magic kwa kushirikiana na Kampuni ya Multi-Choice Africa, imetangaza rasmi kupokea maombi ya kushiriki kwenye msimu wa saba wa tuzo za kimataifa za Africa Magic Viewers’ Choice Awards 2019 maarufu kama AMVCA Awards.
BAADA ya kusibiri kwa muda mrefu, hatimaye Africa Magic kwa kushirikiana na Kampuni ya Multi-Choice Africa, imetangaza rasmi kupokea maombi ya kushiriki kwenye msimu wa saba wa tuzo za kimataifa za Africa Magic Viewers’ Choice Awards 2019 maarufu kama AMVCA Awards.
Akizungumza katika semina maalum kwa ajili ya tuzo
hizo za awamu ya saba na wadau wa tasnia ya filamu hapa nchini, Ofisa Uhusiano
wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania Bi. Grace Mgaya amesema kuwa baada ya muda
mrefu hatimaye tuzo hizo zimerejea tena.
Tuzo hizo ni mahususi kwa ajili ya filamu za Afrika na
hufanyika kila mwaka ili kutambua jitihada kubwa za watengenezaji filamu,
waigizaji pamoja na mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika sekta hii ndani ya
mwaka husika.
Naye Ofisa Maendeleo ya filamu , Bodi ya Filamu
Tanzania, Clarence Chelesi aliongeza: “Kampuni ya MultiChoice imekuwa mstari wa
mbele kuunga mkono juhudi za wazalishaji wa filamu hapa nchini kwetu, hivyo
nitoe rai yangu kwa magwiji wote wa filamu hapa Tanzania kuweza kutumia fursa
hii adimu kwa kushiriki katika mchakato huu ambao utawawezesha kujitangaza na
kuzitangaza kazi zinazotengenezwa hapa nyumbani katika Nyanja za kimataifa
kupitia tuzo hizi”, alieleza Chelesi.
Maandalizi kwa ajili ya msimu huu wa saba yanaendelea
na tuzo hizi zitafanyika Machi mwakani ili kuwapata vinara mbalimbali wa filamu
kutoka barani Afrika.
Maombi yanayokaribishwa kwa ajili ya kushiriki ni ya
kazi za filamu na televisheni ambazo zilitayarishwa na kuoneshwa kuanzia April
1, 2018 hadi Novemba 30, 2019.
Ufuatao ni mwongozo wa jinsi ya kutuma kazi kwa ajili
ya kushiriki:
Hatua
ya 1: Andaa clip ya dakika 5 (reel) kwa ajili ya online
submission.
Hatua
ya 2: Ingia kwenye tovuti ya Africa Magic kupitia www.africamagic.tv/AMVCA. na click
kwenye banner ya AMVCA Seventh edition itakayokupelekea
kwenye ukurasa wa kutuma maombi
STEP
3:
Jaza fomu za kuomba kushiriki halafu upload clip yako. Kila online submission
iliyokamilika itapewa namba ya kumbukumbu kuthibitisha
STEP
4:
Hakikisha video ya kazi yako ina uzito usiozidi mb 300
STEP
5:
Weka namba yako ya kumbukumbu , kisha tuma hard drive ya kazi uliyoiwasilisha
mtandaoni kwenda:
Margaret Mathore
2 nd floor, MNET offices
Local Production Studio
Jamhuri Grounds off Ngong road
Nairobi Kenya
No comments:
Post a Comment