Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania imeanza maadhimisho
ya wiki ya wateja, ambapo itaendesha shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa zawadi
kwa wafanyakazi na wateja kwa muda wa mwezi mzima.
Mkuu wa huduma kwa wateja Ngwitika Mwakihesya amesema
kuwa katika kipindi hicho, MultiChoice Tanzania itakuwa na matukio mbalimbali
yenye lengo la kuiwezesha kuwasogelea wateja karibu zaidi na kufahamu kwa kina
uzoefu wao wa kupata huduma za DStv.
‘MultiChoice inaamini kuwa wafanyakazi na wateja wetu
ndiyo nguzo ya ustawi wetu hivyo katika kipindi hiki tutahakikisha tunawafikia
na kuwasikiliza maoni yao na hili tunalifanya ili tuweze kuboresha zaidi huduma
zetu na kumfanya mteja ajisikie kuwa yeye kweli ni mfalme,” alisema Ngwitika.
Aliongeza kuwa zoezi hilo litahusisha kuwazawadia
wafanyakazi mbalimbali pamoja na wateja na pia kuwatembelea wateja wao maeneo
mbalimblai ili kuwasikiliza na kupata maoni yao.
Amesisitiza kuwa kutokana na uzito huo, zoezi la
kutembelea wateja litafanywa kwa kushirikiana na uogozi wa kampuni hiyo “Zoezi
hili la kuwatembelea wateja litafanywa kwa kushirikiana na viongozi hivyo hata
mkurugenzi mwenyewe na timu yake ya Menejimenti wataenda kuwatembelea wateja”
alisisitiza Ngwitika.
No comments:
Post a Comment