Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Dk Yussuf
Singo (kulia) akimkabidhi mpira msanii, Amisa Mobeto wakati wa hafla ya kuzindua
kampeni ya kuishangilia timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17,
Serengeti Boys, iliyoandaliwa na DStv kwenye hoteli ya Double Tree Masaki
jijini Dar es Salaam.
|
Na Mwandishi Wetu
WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kwa wingi
kuishangilia timu ya taifa ya vijana ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 17
itakayoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika ya Afcon 2019 itakayoanza jijini
Dar es Salaam Jumapili.
Serengeti Boys itafungua dimba kwenye Uwanja wa Taifa
kwa kucheza dhidi ya mabingwa mara mbili wa Afrika na mabingwa mara tano wa
dunia Nigeria.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Dk Singo
aliyasema jijini Dar e Salaam jana wakati wa hafla ya DStv ya kuhamasisha watu
kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu hiyo iliyopo katika Kundi A pamoja na
Nigeria, Angola na Uganda.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Dk Yussuf
Singo (wa pili kulia), Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania, Ronald
Shelukindo (watatu kulia), mchezaji wazamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Amri
Kiemba (kushoto) na Salum Salum wa DStv kulia kabisa.
Hafla hiyo iliwahusisha wachezaji wazamani, wasanii
na wadau wengine wa michezo kuhakikisha wanatumia nafasi au tasnia zao
kuwahamasisha watu kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja huo wa Taifa.
Singo alisema kuwa DStv ambayo imekuwa mstari wa
mbele kusaidia maendeleo ya michezo mbalimbali hapa nchini, imebuni kitu cha
maana kuhakikisha watoto wetu hao wanaungwa mkono kwa watazamaji kuingia kwa
wingi uwanjani na kuwashangilia.
Shumbana. |
Naye Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania , Ronald
Shelukindo alisema wakati akimkaribisha Singo kuwa ni jukumu la kila Mtanzania
kujitokeza kuishangilia Serengeti na wale ambao hawatakuwa na nafasi ya kwenda
uwanjani, basi wataziona mechi hizo kupitia DStv.
Alisema kuwa
DStv imeanzisha kampeni hiyo ya uhamasishaji inayojulikana kama ‘DStv Inogile’
na imehakikisha kuwa michuano mbalimbali ya kimataifa inarushwa mubashara tena
katika kifurushi cha chini kabisa cha DStv Bomba cha Sh. 19,000 tu.
Baadhi ya wachezaji wazamani walioudhuria hafla hiyo Double Tree Masaka, Dar es Salaam. |
Kwa upande wa michuano ya Afcon ya U-17, Shelukindo alisema
DStv itakuwa ikifanya kampeni kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa njia ya mitandao
na matangazo mbalimbali kuhamasisha na kuitia nguvu timu ya taifa ili iweze
kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Baadhi ya wachezaji wazamani waliodhuria hafla hiyo
ni pamoja na Sekilojo Chambua, Edibily Lunyamila, Magoso, Kiemba, Madata
Lubigisa na wengineo, wakati wasanii ni Mobeto, Nancy Sumari, John Makini na
wengine.
No comments:
Post a Comment