Na Mwandishi Wetu
Wateja wa DStv wanauanza mwaka kwa kicheko baada ya
kutangazwa rasmi kuwa DStv itaonyesha michuano maarufu ya ya Emirates FA Cup
kupitia chaneli za SuperSport kuanzia tarehe 4 Januari 2019. Hii inamaana kuwa
mechi za mzunguko wa tatu sasa zitaonekana katika kisimbuzi cha DStv.
Akizungumzia kurejea kwa michuano hiyo katika chaneli
za SuperSport, Mkurugenzi wa MutiChoice Tanzania, Jacqueline Woiso amesema
“Lengo letu ni kuwa mstari wa mbele katika kutoa burudani ya soka bora duniani
kwa wateja wetu wa DStv hivyo, kuanzia tarehe 4 Januari 2019, wateja wetu
wataweza kufurahia michuano ya Kombe la Emirates maarufu kama FA Cup kupitia
chaneli za SuperSport zizopatikana ndani ya vifurushi vya DStv".
Amesema kuwa
muda wote MultiChoice imahakikisha kuwa wateja wake wanapata burudani ya hali
ya juu na ndiyo sababu wamekuwa wakiongeza maudhui mapya kila uchao katika
vifurushi vya DStv.
Sambamba na mechi za michuano ya kombe la FA za
mzunguko wa tatu zitakazoanza Januari 4 2019, wateja wa DStv pia wataendelea
kuburudika na ligi kubwa za soka zinazotamba duniani ikiwemo ligi kuu ya
Uingereza maarafu kama PL, ligi kuu ya Italia Seria A, michuano ya ligi kuu ya
Hispania {La Liga} na ligi ya mabingwa Ulaya maarufu kama EUFA Champions League
bila kusahau maudhui mengineyo mengi zikiwamo filamu na tamthilia mpya
kutoka nje na ndani ya Tanzania na vipindi vya watoto.
Mechi hizi za michuano ya Kombe la FA zitakuwa zikipatikana
mubashara kupitia chaneli za Supersport ndani ya DStv. Idadi ya mechi
zitakazoonekana mubashara zinatofautiana kulingana na aina ya kifurushi huku
baadhi ya mechi hizo zikionekana katika kifurushi cha chini cha DStv Bomba kwa
Sh 19,000.
Kwa wateja wanaotaka kujiunga na DStv, bado wanaweza
kunufaika na ofa inayoendelea ya msimu wa sikukuu ambapo kwa gharama ya
Sh.79,000 tu! Mteja anapata seti kamili
ya DStv. Pia kupitia mtandao wa bongoshop.dstv.com mteja anaweza kupata
maelekezo ya ziada ya namna ya kujiunga na DStv, ikiwemo kuunganishwa na
mawakala na mafundi wa DStv popote alipo.
No comments:
Post a Comment