JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
MAMLAKA YA
VIWANJA VYA NDEGE
Simu: +255 22 2842402-3 S.L.P 18000,
Fax: +255 22 2844495 DAR
ES SALAAM
19/07/2016
E-mail:info@airports.go.tz
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Kassim M. Majaliwa kesho, tarehe 20/07/2016, anatarajiwa
kuweka jiwe la msingi la mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha ndege cha
Dodoma.
Ukarabati huo utajumuisha
urefushaji wa barabara ya kuruka na kutua ndege hadi kufikia urefu wa kilometa 2.5
kutoka Kilometa 2 za awali.
Kurefushwa kwa barabara
hiyo, sasa kutatoa fursa kwa ndege kubwa Bombardier Q400, Gulfstream 550, ATR
72 n.k zenye uwezo wa kubeba abiria 90.
Ukarabati huo unafanyika kwa
fedha za Serikali ya Tanzania na unasimamiwa na Wahandisi wa Mamlaka ya Viwanja
Vya Ndege Nchini kwa ushirikiano na Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS).
Ukarabati na upanuzi wa
Kiwanja cha Ndege cha Dodoma ni miongoni mwa Miradi mbali mbali inayotekelezwa na
Mamlaka ya viwanja Vya Ndege nchini kama vile Viwanja vya Tabora, Bukoba,
Kigoma na Mwanza ambayo imekwisha anza na miradi mipya ya viwanja vya ndege vya
Shinyanga na Sumbawanga itakayoanza hivi karibuni.
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA) ni wakala wa viwanja vya ndege iliyoanzishwa kwa Tangazo la
Serikali Namba 404 la mwaka 1999, chini ya Sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 ya
mwaka 1997.
Dira:
Kuwa mtoaji wa Huduma za Viwanja vya Ndege kwa
kiwango cha Kimataifa
Dhima:
Kutoa Huduma Bora na Viwezeshi katika Viwanja vya
Ndege kwa kuzingatia ufanisi katika matumizi ya rasilimali zilizopo
Imani kuu za Mamlaka:
·
Kuwajali
Wateja
·
Kuwaendeleza
Wafanyakazi wa Mamlaka
·
Ulinzi
na Usalama Viwanjani
·
Kufanya
kazi kwa pamoja
·
Kuwa
na Uongozi wa Mabadiliko
·
Uadilifu
IMETOLEWA NA KITENGO CHA SHERIA
NA MAHUSIANO TAA
No comments:
Post a Comment