Tuesday 3 February 2015

Ronaldo auzwa kwa Pauni Milioni 300





LONDON, England
CRISTIANO Ronaldo atauzwa kwa kiasi cha pauni Milioni 300 endapo klabu ya Real Madrid itaamua hata kesho kumuchia mchezaji huyo kuondoka.

Hayo yalisemwa na wakala wa mchezaji huyo nyota wa Ureno alipozungumza leo na BBC Sport.

Wakala huyo Jorge Mendes alisema nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno ni mchezaji bora wa muda wote.

"Ni mchezaji bora wa muda wote duniani. Kamwe huwezi kumfananisha na mchezaji mwingine yeyote, alisema Mendes alipozungumza na muhariri wa michezo Dan Roan.

Ronaldo, mwenye umri wa miaka 29, mwezi uliopita alichaguliwa kwa mara ya tatu kuwa mchezaji bora wa dunia, akimbwaga Lionel Messi wa Barcelona katika tuzo hiyo.

Alipoulizwa mchezaji huyo ana thamani kiasi gani, Mendes alisema: 
"Cristano Ronaldo? Bilioni moja. Anakaribia Bilioni moja, hivyo ni bilioni moja. Kwa kweli haiwezekani kumpata mwingine anayefanana nay eye.

"Endapo kwa sabbau zozote zile klabu itaamua kumuuza hata kesho kwa Milioni 300, mtu atalazimika kulipa kiasi hicho cha pesa. "

Hatahivyo, Mendes aliaisisitiza kuwa raia huyo mwenzake wa Ureno ambaye alinunuliwa na Real Madrid kwa rekodi ya dunia ya ada ya dola za Marekani Milioni 80 mwaka 2009, ataendelea kubaki Bernabeu, licha ya mapenzi yake" kwa klabu yake ya zaman ya Manchester United.

Alipoulizwa kama atamalizia soka lake Real Madrid, Mendes alisema "na uhakika". "Hataondoka Real Madrid," aliongeza.

Mendes, aliyeripotiwa kuwa alipata zaidi na pauni bilioni 1 kwa ajili ya uhamisho tu, akielezewa kuwa ni mmoja wa watu wenye nguvu sana katika mchezo huo.

"Watu wana mtazamo tofauti kuhusu mawakala. Kuwa wakala kuna maana tofauti. Mimi ni mtu wa kawaida kabisa. Ninafanya kazi kwa bidii kila siku. Nina malengo na kusema ukweli ninatenda haki na hilo ndio muhimu zaidi.

Alielezea kuwa soka ni mchezo muhimu sana duniani na alitetea mishahara ya wachezaji, akisema wanastahili kiasi kikubwa kama inawezekana".

Mendes alifananisha kufanyakazi na wachezaji kwa mikataba ni sawa na familia.

"Ni kama vile unavyozungumza na mtoto wako, au familia yako wakati wote unajaribu kutafuta njia bora ya kuwasaidia."

Mendes, DJ wazamani na mmiliki wa klabu ya usiku, pia ni wakala wa Jose Mourinho, Luiz Felipe Scolari, Radamel Falcao, Angel Di Maria, James Rodriguez, David De Gea, Victor Valdes na Diego Costa.

No comments:

Post a Comment