Friday, 23 February 2018
Mechi Kali za Premier League Wikiendi hii
Angalia mechi hii MUBASHARA kwenye DStv Bomba
kwa sh.19,000 tu, mechi itachezwa saa 12 jioni ,Supersport 10.
Mechi nyingine zitakazopigwa
wikiendi hii kwenye Premier League ni:
• Leicester
City dhidi Stoke City saa 9 alasiri kwenye Supersport 3
• Watford
vs Everton saa 2 usiku kwenye Supersport 3
• Burnely
vs Southampton saa 12 jioni Supersport 5
• Na
AFC Bournemouth itacheza dhidi ya Newcastle United saa 12 jioni a kurushwa LIVE
kwenye Supersport 10 iliyopo kwenye kifurushi Bomba kw ash.19,000 tu!
Jumapili ndio balaa lenyewe pale Manchester
United ambao kwasasa wanashika nafasi ya 2 kwenye msimamo wa EPL wakiwa na
pointi 56 wanawakaribisha Chelsea ambao wapo nafasi ya 4 wakiwa na utofauti wa
pointi 3 tu! Je, Man Utd atashinda au Chelsea itafunga pengo?
Usikose mechi hii, Jumapili saa 10 jioni
kwenye Supersport 3 ya kifurushi DStv Compact kwa sh.69, 000 tu!
Je hujajiunga na DStv? wahi sasa Ofa ya THE PUNGUZO, burudika na
miezi miwili bure kwa kununua Dekoda pamoja na Dish kwa sh.79, 000 tu!
Kujiunga piga 0659 070707, THE PUNGUZO na
DStv!!
Zabuni 163 za ujenzi wa hoteli ya nyota nne na maeneo ya biashara Termina 3 zafunguliwa leo

Tuesday, 20 February 2018
Marubani wa Kenya Waliotekwa Warejea
NAIROBI, Kenya
MARUBANI wawili wa Kenya ambao walikuwa
wakishikiliwa na kundi la magaidi Sudan Kusini kwa zaidi ya mwezi mmoja
wamerejea nyumbani.
Walitua kwenye Kiwanja cha Ndege Nairobi
kabla hawajakutana na ndugu zao.
![]() |
| Rubani Njoki akikutana tena na mtoto wake wakike mwenye umri wa miaka 12, Lucy Muthoni. |
Magaidi hao waliwakamata wawili hao mapema
mwezi uliopita wakati ndege ilipoanguka katika mkoa wa Upper Nil, ikiripotiwa kuuwa mwanamke mmoja na
baadhi ya mifugo.
Marubani hao wawili waliachiwa juzi kufuatia
mazungumzo mazito ya makubaliano yaliyowashirikisha viongozi wa serikali ya
Sudan Kusini na wenzao wa Kenya.
Sunday, 18 February 2018
Ndege Yaanguka na Kuuwa Abiria 66 Iran
TEHRAN, Iran
WATU 66 wamekufa baada ya ndege ya abiria kuanguka Iran,
maofisa wa ndege hiyo wamesema.
Ndege hiyo ya Shirika la Ndege la Aseman, ilikuwa
ikifanya safari yake kutoka Tehran kwenda katika jiji la kusini-magharibi la Yasuj,
ilianguka katika milima ya Zagros.
Shirika la Misaada la Mwezi Mwekundi liituma timu yake ya
waokoaji kwenda karibu na eneo la tukio karibu na jiji la Semirom katika jimbo
la Isfahan.
Ndege hiyo ilianguka katika Mlima wa Dena, ikiwa ni
kilometa 22 kutoka Yasuj, taarifa ya chaneli ya Irinn iliripoti.
Ndege hiyo ilikuwa na jumla ya abiria 60, wawili walinzi
wa usalama, wawili wafanyakazi wa ndege na rubani pamoja na msaidizi wake.
"Baada ya kuitafuta katika eneo hilo, bahati mbaya
tulitaarifiwa kuwa ndege hiyo imedondoka. Na kwa bahati mbaya abiria wetu
wapendwa wote wamepoteza maisha.”
DStv Media Bonanza Yafanyika kwa Kishindo Dar
Na Mwandishi Wetu
WAANDISHI wa Habari kutoka vyombo mbalimbali leo
walijumuika pamoja katika DStv Media Bonanza lililofanyika katika viwanja vya
Gymkana Club Jijini Dar es Salaam.
Katika Bonanza hilo, timu ya soka inayoundwa na
wafanyakazi wa DStv na ile inayopundwa na waandishi wa habari kutoka vyombo
mchanganyiko (Taswa FC) ziliumana na kutoa burudani safi kwa watu mbalimbali
waliofika hapo.
![]() |
| Johnson Mshana akiwa na wadau. |
Katika mchezo huo, timu ya Taswa FC iliibuka na
ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya wapinzani wao hao, ambao walitamba katika kipindi
cha kwanza na kushindwa kuendeleza cheche zao kipindi cha pili.
Katika bonanza hilo lililoanza majira ya saa 6:00
mchana hadi 12:00 jioni, washiriki waliburudika na burudani mbalimbali zikiwemo
muziki wa dansi `live’ na burudani nyingine.
Pia walipata vinywaji na msosi huku wakibadilishana
mawazo baada ya wengine kutoonana kwa
muda mrefu, ambapo hafla hiyo iliwakutanisha waandishi wa vyombo mbalimbali
huku DStv ikiahisi kuendelea kushirikiana nao.
![]() |
| Kikosi cha DStv kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya Taswa FC. |
![]() |
| Vikosi vya DStv (wenye jezi bluu) na Taswa FC (nyeupe) kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafki. |
![]() |
| Kikosi cha Taswa FC |
![]() |
| Mhariri wa gazeti la Dailynews na Sundaynews, Nasongelya Kiyinga akisalimia na mfanyakazi wa DStv, Levina wakati wa hafla hiyo. |
![]() |
| Mtangazaji wa SuperSport na mwandishi mkongwe nchini, Aboubakary Liongo akisalimiana na mwandishi wa Mtanzania, Mwani Nyangasa. |
![]() |
| Kikundi cha ushangiliaji cha DStv wakati timu yao ilipocheza dhidi ya Taswa FC. Taswa ilishinda 4-2. |
![]() |
| Baadhi ya waandishi wakichukua msosi wakati wa bonanza hilo. |
Mchezaji wa Taswa FC, Majuto Omary `Bonge' akitafuta njia ya kuwatoka wachezaji wa DStv wakati wa mchezo wa kirafiki wa DStv Media Day Bonanza mapema leo Gymkana Club Jijini Dar es Salaam. Taswa ilishinda 6-2.
Thursday, 15 February 2018
DStv Media Day Bonanza Kufanyika Kesho
Na Mwandishi Wetu
BONANZA kubwa la Waandishi wa Habari lintarajia
kufanyika kesho Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam,
imeelezwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shumbana Walwa
wa DStv, bonanza hilo litashirikisha Waandishi wa Habari kutoka vyombo
mbalimbali vya habari nchini.
Katika bonanza hilo kutakuwa na michezo mbalimbali,
ambapo timu ya wafanyakazi wa DStv watatoana jasho na timu ngumu ya soka ya Chama cha
Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Taswa.
Mbali na mchezo huo na mingine, pia kutakuwa na
burudani live ya muziki wa dansi, ambapo wageni waalikwa wataburudika kwa
muziki huo kabambe.
Pia waandishi pamoja na wadau wengine wa habari,
watapata chakula cha mchana pamoja kuhitimisha shughuli hiyo, ambayo hufanyika
kila mwaka.
DStv wafungua tawi jipya, watoa ofa kabambe
Na Mwandishi Wetu
MULTCHOICE Tanzania leo Ijumaa itazindua tawi lake
jipya katika eneo la bishara la Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo,
inasema kuwa hatua hiyo ya kufungua tawi eneo hilo maarufu ni kwa ajili ya
kuwasogezea huduma ya DStv wateja wao wa maeneo mbalimbali wanaofika maeneo
hayo kupata huduma zingine.
Katika kusheherekea Msimu huu wa Valentine, DStv
hawajakusahau, wanakuletea huduma zao karibu zaidi na kukupa zawadi Kabambe ya
Valentine.
Taarifa hiyo imezidi kueleza kuwa, tawi hilo limesheheni
huduma zote na wafanyakazi wacheshi na wakarimu wako tayari kabisa kukuhudumia.
Ili kuzidi kuleta msisimko kwenye valentine hii, DStv
wanakuletea Ofa maalum kwa wateja wa tawi lao la Mlimani City pekee, fika
tawini kuanzia tarehe 13 hadi 18 February upate kununua Dikoda, Dishi na Vifaa
vyote kwa sh.69,000 tu pamoja na miezi
miwili buree!!
Ofa hii haishii hapo ndugu yangu, DStv watakupatia Na
ufundi buree. Yaani hii ni The Punguzo Valentine Special!
Wahi sasa kwenye ofisi zao mpya zilizopo Mlimani City
opposite na zamani Nakumat Supermarket.
Wednesday, 14 February 2018
Maisha Magic Bongo Kufadhili Harusi ya Aina Yake
Na
Mwandishi Wetu
WAKAZI wawili wa jijini Dar es Salaam ambao ni
wachumba, Solomon Mwaigwisa na Magreth Richard wameibuka washindi wa shindano
la Harusi ya Ndoto Yako lililokuwa likiendeshwa na chaneli ya Maisha Magic
Bongo Dstv chaneli 160.
Wapenzi hao wameshinda zawadi ya ufadhili wa harusi
yao ya kifahari itakayofanyika jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa April mwaka
huu. Pamoja na kushinda Harusi ya Ndoto
Yao, wawili hawa pia watapewa zawadi ya fungate kwa hisani ya hoteli ya kitalii
ya Voyager Beach iliyopo jijini Mombasa nchini Kenya.
![]() |
| Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice-Tanzania, Maharage Chande. |
Washindi hao walitangazwa leo asubuhi katika kilele
cha Siku ya Wapendanao katika hafla iliyofanyika makao makuu ya MultiChoice
Tanzania jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na washindi hao.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa
MultiChoice Tanzania Maharage Chande amesema channel ya Maisha Magic Bongo
imeamua kuwatunuku watazamaji wake zawadi hiyo kupitia kipindi chake maarufu
cha Harusi Yetu kinachorushwa na channel hiyo ambacho huonyesha harusi
mbalimbali.
Kipindi cha Harusi Yetu kilianza kuruka Novemba 2016,
ambapo msimu wa pili wa kipindi hicho ulianza mwezi Julai mwaka 2017. Kipindi
hicho hurusha harusi mbamlimbali huku kikiangazia walikotoka wanandoa, hatua
wanazopitia katika mahusiano yao na hatimaye tukio la kufunga ndoa.
Kuanzia ilipoanza awamu ya pili Maisha Magic Bongo
ilianzisha shindano maalum lililojulikana kama Harusi ya Ndoto Yako ambapo
washiriki walikuwa wakijibu kuhusiana na kipindi cha harusi yetu ambapo kila
wiki kulikuwa na swali moja.
![]() |
| Waandishi wa habari wakifuatilia hafla hiyo. |
Baada ya usaili huu, Solomon mkazi wa Dar es Salaam
pamoja na mchumba wake Magreth waliibuka washindi na hivyo kupata zawadi ya
kugharimiwa harusi yao itakayofanyika jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 28
mwezi April mwaka huu.
![]() |
| Mfanyakazi wa DSTV, Shumbana. |
Akifafanua kuhusu zawadi hiyo, Maharage alisema
zawadi hiyo inamaanisha maharusi hao watarajiwa watagharimiwa kila kitu kuanzia
ukumbi, mavazi, chakula, vinywaji, burudani, pamoja na fungate la kukata na
shoka katika moja ya hoteli za kitalii Voyager Beach Hotel katika ufukwe wa
Mombasa nchini Kenya.
Wakizungumza katika hafla hiyo, Solomon pamoja na
mchumba wake Magreth wamesema wamefurahi sana kushinda na kutuzwa ufadhili wa
harusi yao. “Sote tunafahamu ni jinsi gani zoezi la harusi linavyokuwa na
patashika hususan kwenye suala la gharama.
![]() |
| Maharusi watarajiwa, Solomon na Magreth wakiingia stejini. |
“ Hivyo nafurahi sana na ninamshukuru Mungu kwa
kutuwezesha kushinda katika shindano la Harusi ya Ndoto Yangu kwani sasa sisi
kazi yetu ni kufikiria tu jinsi tutakavyoendesha maisha yetu kwani suala la
harusi limekamilika” alisema Solomon, ambaye ni Bwana Harusi mtarajiwa.
Ameipongeza Chaneli ya Maisha Magic Bongo kwa kubuni
shindano hilo ambalo lilileta msisimko mkubwa na kwamba anaamini kuwa channel
hiyo itaendelea kuimarika kwani kwa sasa imekuwa maarufu sana kwa kuwa ni
chaneli inayowafanya watanzania wajivunie vipaji vyao.
![]() |
| Bi Harusi Mtarajiwa, Magreth. |
DStv kupitia chaneli yake mahsusi ya maudhui ya
Kitanzania ya Maisha Magic Bongo imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha
kuwa tasnia ya Sanaa inakua na kuifanya iwe moja ya vyanzo muhimu vya mapato
kwa wasanii na hatimaye kuchangia katika uchumi wa nchi yetu.
Chanel ya Maisha Magic Bongo ilianzishwa tarehe 1
Octoba 2015, kwa lengo kuu la kuinua na kukuza vipaji na Sanaa hapa Tanzania na
pia kuongeza maudhui ya kitanzania kwa wateja wa DStv.
![]() |
| Maharusi watarajiwa wakati wa hafla hiyo. |
Kwa kipindi chote hiki Chaneli hii imekua kwa haraka
sana ambapo kwa sasa ni miongoni mwa Chaneli zenye watazamaji wengi zaidi
katika ukanda wa Afrika Mashariki. Chaneli hii imekuwa kitovu cha maendeleo ya
wasanii hapa nchini huku mamia ya wasanii wakipata fursa mbalimbali kutokana na
kazi zao kurushwa katika channel hii na pia kupata mafunzo na kipato kupitia
Sanaa.
Kwa upande wa tasnia ya filamu na uigizaji, Maisha
Magic Bongo imeleta mapinduzi makubwa na miongoni mwa filamu zinazotikisa
katika soko kwa sasa ni pamoja na Tamthila ya HUBA,ambayo ilipokelewa vizuri sana
na Watanzania, pia kuna filamu na vipindi vingine kama MWANTUMU, HARUSI YETU,
KITIMTIM pamoja na tamthilia mpya zilizoanza kuonyeshwa hivi karibuni za SARAFU
na KAPUNI ambazo zote zinazidi kuwa maarufu kila uchao.
![]() |
| Wedding Planner wa harusi hiyo. |
Subscribe to:
Posts (Atom)
















































