Tuesday, 6 September 2016

Mbio za mbuzi kufanyika Jumamosi Septemba 10 na kutarajia kukusanya sh mil 120


Meneja wa Bia ya Kilimanjaro wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Pamela Kikuli akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo kwenye hoteli ya Southern Sun kuhuzu Mbio za Mbuzi zitakazofanyika Jumamosi. Kulia ni Meneja Maswaliano wa Tigo, Umi Mtiro. Kulia kwa Kikuli ni mratibu wa mbio, Karen Stanley, meneja masoko wa Coca Cola Nalaka Hettiarachchi na bosi kutoka Toyota-Tanzania, Eliavera Timoth.

Na Mwandishi Wetu
SHINDANO la Mbio za Mbuzi litakalofanyika Jumamosi jijini Dar es Salaam linatarajia kukusanya kiasi cha sh Milioni 120 kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali.
Fedha hizo zitatumika kusaidia watoto wenye saratani, kusaidia kliniki ya meno inayotembea na kuzisaidia jamii zenye shida mbalimbali nchini.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu Mbio za Mbuzi. Kushoto ni mratibu wa mbio hizo, Karen Staley au Mama Mbuzi.
 Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana mmoja wa waratibu wa mbio hizo Karen Stanley alisema kuwa mwaka huu wanatarajia mbio hizo kuwa na msisimko wa aina yake katika viwanja vya The Green Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Alisema mbio za mwaka huu zimedhaminiwa na Swiss Air, hoteli ya Southern Sun, Coca Cola, Toyota-Tanzania na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Umi Mtiro akizungumza katika hafla hiyo leo katika hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam. Kushoto ni meneja wa Bia ya Kilimanjaro Pamela Kikuli.
Swiss Air imesema itanunua tiketi 1,000 na kuziuza, ambapo katika tiekti hizo watacheza bahati nasibu na mshindi wawili, mmoja atapata tiketi ya daraja la pili kwenda Ulaya na nyingine kwenda mahali kokote duniani.

 Tangu kuanza kwa mbio hizo miaka 16 iliyopita tayari zimeshakusanywa zaidi ya sh Bilioni 1, ambazo zimesaidia miradi mbalimbali nchini kote ikiwemo ujenzi wa madarasa.

Mwalimu wa shule ya Muhogolo wa shule ya St. Paul English Medium ya Kibaigwa alisema mbio za Mbuzi zimesaidia shule pesa za kujenga madarasa.

Mwakilishi wa Toyota-Tanzania katika mbio za Mbuzi, Eliavera Timoth akizungumza leo katika hafla hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Umi Mtiro alisema kuwa wamekuwa wakidhamini mbio hizo kwa miaka miwili sasa, ambapo pamoja na mambo mengine wamekuwa wakitoa huduma ya mawasiliano uwanjani hapo.
Meneja Masoko na Mauzo wa Coca Cola nchini, Nalaka Hettiarachich akizungumza leo.
Mwaka jana mbio hizo ziliusanya kiasi cha sh Milioni 150, ambapo mwaka huu watakusanya pungufu ya mil 30 kutokana na ukata kwa baadhi ya makampuni.

Hispania yaichakaza kibonde Liechtenstein mabao 8-0, Italia ikishinda 3-1 mbio za kwenda Urusi 2018



Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya Hispania wakishangilia moja ya mabao yao dhidi ya  Liechtenstein.
MADRID, Hispania
HISPANIA imetoa onyo kwa timu zinazoshiriki katika kinyanganyiro chakusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Liechtenstein.

Mabao yao saba yalipatikana katika kipindi cha pili wakati Liechtenstein wakijaribu kupambana baada ya kuwapelekesha wenyeji wao mwanzoni mwa mchezo.

Diego Costa, David Silva na Alvaro Morata wote kila mmoja alifunga mara mbili wakati Sergi Roberto na Vitolo nao pia waliingia katika orodha ya wafungaji katika mchezo huo wa ufunguzi wa Kundi G.

Huo n mwanzo mzuri katika mchezo wa kwanza wa kimashindano kwa kocha Julen Lopetegui, ambaye alihusika kwa timu yake kupata ushindi kiduchu baada ya kuwa mbele kwa bao 1-0 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

Matokeo hayo yaliwafanya kuwa vinara wa awali wa Kundi G lakini Italia nayo ilianza kwa ushindi wa 3-1 licha ya kujkuta ikipunguzwa na kubaki na wachezaji 10 walipocheza dhidi ya Israel katika mchezo uliofanyika Haifa.

Graziano Pelle alikiwezesha kikosi cha kocha Giampiero Ventura kuanza vizuri kampeni zake kabla Antonio Candreva hajaongeza bao jingine alilofunga kwa penalti na kuihakikishia ushindi timu hiyo.

Tal Ben Chaim aliifungia Israel bao la kufutia machozi lakini Ciro Immobile aliongeza na kuifanya Italia kukamilisha ushindi wake wa mabao 3-1 licha ya kutolewa kwa mchezaji wake Giorgio Chiellini.

Mchezo mwingie wa kundi hilo haukumalizika wakati Albania ikicheza na wajirani zao wa Macedonia huko Shkoder ilibidi kusimamishwa baada ya dakika 77 kufuatia mvua kubwa kunyesha.

Wakati mchezo huo unasimama timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1 kwa bao la Ergjan Alioski ambalo lilikuwa linajibu lile la Armando Sadiku alilofunga mapema.

Kosovo nao ilianza vizuri kucheza mashindano hayo ya kufuzu kwa Kombe la Dunia baada ya kutoka nyuma na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wao wa kwanza wa kufuzu katika mchezo uliofanyika Finland.l

Mchezaji wazamani wa Norway Valon Berisha mmoja kati ya wachezaji sita walihalalishwa kucheza saa chache kabla ya kuanza kwa mchezo huo, alifunga bao la kusawazisha kwa penalti baada ya dakika 60.

Paulus Arajuuri aliipatia Finland bao la kuongoza katika mchezo wa Kundi I, lakini Kosovo, ikicheza mchezo wake wa kwanza wa mashindano ya kimataifa, ilicheza vizuri na walipiga mwamba kupitia kwa Leart Paqarada kabla Berisha hajaiwezesha timu hiyo kuondoka na pointi.

Hiyo ni moja kati ya sare tatu za 1-1 katika kundi hilo, huku zingie zikiwa ni kati ya Croatia na Uturuki huko Zagreb na Ukraine na Iceland huko Kiev ambazo nazo zilimalizika kwa sare kama hiyo.

Katika Kundi D, mbaop kutoka kwa Martin Hinteregger na Marc Janko yaliisaidia Austria kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Georgia huko Tbilisi.Bao la kufutia machozi lilifungwa na Jano Ananidze.

Kwingineko katika Kundi D, Ireland ilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Serbia huku Wales ikiichapa Moldova 4-0.

bonanza la uzinduzi wa mashindano ya Shimiwi kufanyika jumamosi huku mashindano yakifanyika dodoma kuanzia Oktoba 14 hadi 27


Baadhi ya watazamaji wakifuatilia mashindano ya Shimiwi yaliyofanyika mkoani Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Na Mwandishi Wetu
BONANZA la uzinduzi wa Michezo ya Watumishi wa Serikali (Shimiwi), litafanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, imeelezwa.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Shimiwi Moshi Makuka, bonanza hilo linatarajia kuanza saa 12:30 asubuhi na kushirikisha watumishi wote wa Serikali kutoka katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema kuwa mgeni rasmi katika bonanza hilo atakuwa Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Watumishi wa Umma Balozi John Kijazi.

Michezo ya mwaka huu ya Shimiwi itafanyika mkoani Dodoma kuanzia Oktoba 14 hadi 27.

Makuka alizitaja sababu zilizopelekea kufanyia michezo hiyo mkoani Dodoma ni pamoja na kuunga mkono agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli la Serikali kuhamia katika Makao Makuu Dodoma.

Sababu nyingine ni kuwapa nafasi Watumishi wa Umma ambao hawajawahi kufika Dodoma kufahamu mazingira na kufanya maandalizi muhimu kwa ajili ya kuhamia.

Tarehe 14 Oktoba, 1999 siku ambayo Mwalimu Nyerere alipoaga Dunia Watumishi wa Umma tulikuwa katika michezo hii mkoani Morogoro, hivyo sisi (Watumishi wa Umma) tahrehe hiyo ni kumbukumbu muhimu ya kifo chake, pia ni ni kuenzi agizo lake la kuhamia Dodoma, alisema Makuka.

Alisema kuwa michezo ya mwaka huu itaanza kwa ibada maalum kwa ajili ya kumuombea Baba wa Taifa pia kumtakia afya njema Rais Magufuli pamoja na wasaidizi wake.

Pia Shimiwi itatumika kupanda miti katika maeneo yatakayoelekezwa na Serikali ya mkoa wa Dodoma.

Kocha Mauritania hana uhakika na hatma yake licha ya timu kufanya vizuri michuano ya kufuzu kwa afcon 2017 gabon



NOUAKCHOTT, Mauritania
KOCHA wa Mauritania Corentin Martins (pichani) hana uhakika wa kuendelea kuwepo katika timu hiyo licha ya kuiongoza kumaliza vizuri hatua ya kufuzu ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2017).

Sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Afrika Kusini huko Nelspruit kuliihakikishia Mauritania kumaliza katika nafasi ya pili katika kundi lake.

Wamekosa nafasi ya kufuzu kwenda Gabon mwakani lakini Martins alisema kuwa kundi lao, ambapo pia likuwa na timu za Afrika Kusini na Gambia, lilikuwa moja ya makudni ya kifo.

Mchezaji huyo wazamani wa Ufaransa, ambaye timu yake ilikuwa na nafasi finyu kimahesabu ya kufuzu kwa fainali hizo kama ingeshinda mchezo huo, alisema alikuwa akitarajia kumaliza wa pili katika msimamo wa kundi lao.

"Kwan chi ambayo haija wachezaji wengi wenye uzoefu katika soka la kimataifa, tumepiga hatua kubwa, alisema kiungo huyo wazamani wa Auxerre.

"Zaidi ya miaka miwili, tulikuwa na nafasi kucheza na timu kutoka mataifa makubwa kisoka Afrika na kujifunza mengi kutoka kwa wazoefu. Ilikuwa nafasi finyu kwa Mauritania kupata nafasi kama ile ya kucheza na timu kubwa.

"Kufanya vizuri dhidi yao tulitupatia kujiamini sana. Mara mbili tumeshindwa kwa bao moja na Cameroon, na tulifungwa kidogo na Tunisia katika mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia na tulipata pointi nne kutoka kwa Afrika kusini. 
Nafikiri tunaweza kuendelea kupata matokeo mazuri.

Mauritania kwa muda mrefu ilikuwa ikichukuliwa kuwa ni taifa dogo katika soka lakini baada ya sare ya Ijumaa inatarajia kupanda viwango vya Fifa na kwa mara ya kwanza kufikia katika 100 katika kipindi cha miaka 20.

"Kwa kweli tulikuwa tukifanya kazi kwa bidii kuongezea ubora timu hii na ninafikiri tumesonga mbele kwa haraka sana, alisema Martins.

Lakini kocha huyo mwenye umri wa miaka 47, ambaye alinza kazi yake na Mauritania Oktoba miaka miwili iliyopita, alisema kuwa hajui kama atapewa ofa nyingine ya kuendelea kuifundisha timu hiyo.

Mkataba wake wasasa unatarajia kumalizika Desemba mwaka huu.

 "Nina furahia sana kazi hii, watu wa hapa ni wazuri sana kwangu na nimekuwa na uhusiano mzuri na uongozi. Bila shaka, sio kitu rahisi kuwa kocha wa timu ya taifa-unaathirika sana unapokuwa katika benchi.alitania kocha huyo. Lakini sijui kitu gani kitatokea sasa.

Mauritania ilipoteza mechi mbili tu kati ya sita za kundi lake la M, ambapo ilimaliza ikiwa na point inane.

Katika mashindano ya kufuzu yaliyopita ilimaliza ya mwisho kimsimamo, na haikuwahi kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika.