Thursday, 10 December 2015

RISALA YA KATIBU MKUU (TOC) KWENYE UFUNGUZI WA KAMISHENI YA WANAMICHEZO ZANZIBAR TAREHE 10/12/2015.



Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kamisheni ya Wachezaji ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (Kawata) leo Zanzibar. Kushoto ni mwenyekiti wa Kawata, Ramadhan Zimbwe. Kushoto kwa Bayi ni Katibu Msaidizi wa TOC Jamal Adi na rais wa Toc Gulam Rashid.

 TANZANIA OLYMPIC COMMITTEE (TOC)
KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA

RISALA YA KATIBU MKUU (TOC), FILBERT BAYI KWENYE UFUNGUZI WA KAMISHENI YA WANAMICHEZO ZANZIBAR TAREHE 10/12/2015.

Ndugu Mgeni Rasmi Jamal Adi, Katibu Mkuu Msaidizi TOC

Ndugu Gulam Rashid, Rais wa TOC,

Ndugu Ramadhani Zimbwe, Mwenyekiti, KAWATA Taifa,

Ndugu Amina Ahmed, Katibu KAWATA Taifa

Viongozi Kamati yaUtendaji Waalikwa

Kamati ya Utendaji, KAWATA Taifa,

Wanamichezo Washiriki

Mabibi na Mabwana.

Kwa niaba ya Kamati ya Olimpiki Tanzania na kwa niaba yangu mwenyewe sina budi kumshukuru Katibu Mkuu Msaidizi wa TOC, pamoja na kuwa moja wa viongozi wa juu wa TOC kukubali mwaliko wa ofisi ya TOC kwa kuja hapa leo  kutufungulia Mkutano huu Mkuu wa Kamisheni ya Wanamichezo.

Ndugu Mgeni Rasmi, ofisi ya TOC imekuwa hapo awali ikialika wageni rasmi hasa katika shughuli hizi za ufunguzi wa mikutano yetu kutoka nje hasa taasisi na serikali, lakini kuanzia sasa itakapobidi shughuli hizi zitafanywa na viongozi wa TOC au Vyama/Mashirikisho ya Michezo.

Ndugu Mgeni Rasmi, tangu Kamisheni ya Taifa ilipoundwa hapo mwaka 2006, kazi kubwa ilikuwa kuhamasisha na kutoa wito kwa Vyama/Mashirikisho ya Michezo kuanzisha Kamisheni ya wachezaji katika Vyama/Mashirikisho yao ya Michezo. Ni Vyama/Mashirikisho chache ambayo yameitikia wito wetu kwa kufanya uchaguzi halali wa kidemokrasia.
Vyama vingi mpaka sasa vimekuwa vikiteua wajumbe wake kuhudhuria Mikutano Mikuu ya Kamisheni inayoandaliwa na TOC, lakini cha kushangaza kwa utafiti ulioofanywa na TOC/KAWATA Taifa, wachezaji hao siyo wajumbe katika Kamati za Utendaji na Mikutano Mikuu ya Vyama na Mashirikisho husika kama Muongozo wa Kamisheni unavyosema.

Sijui ni kwa nini Vyama/Mashirikisho ya Michezo yaogope kuwaingiza wachezaji kwenye chombo cha maamuzi (Kamati ya Utendaji/Mkutano Mkuu). Kuna siri gani kubwa katika vikao vya Kamati ya Utendaji na Mkutano Mkuu ambayo hayapaswi wachezaji kufahamu? 

Mimi nina imani kabisa wawakilishi wa wachezaji watakapokuwa kwenye vyombo hivyo vya maamuzi malalamiko na manung’uniko mengi ya wachezaji hayatakwepo, kwani watakuwa wameshiriki kikamilifu katika maamuzi.

Mahali ambako Mkutano Mkuu wa Kamisheni ya Wachezaji (Kawata) unapofanyikia leo Zanzibar.
Ndugu Mgeni rasmi, Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC), Vyama/Mashirikisho ya Kimataifa (IFs), ANOCA na NOCs kama TOC  zina Kamisheni zao ya Wanamichezo ambazo kazi zao kubwa ni kama:

1.     Kutoa ushauri, nasaha kwa wanamichezo waliostaafu na ambao bado wanaendelea na michezo.
2.     Kulinda maslahi ya wanamichezo ndani ya maadili ya Olimpiki.
3.     Kutoa mapendekezo kwa mambo yanayohusu maslahi ya wanamichezo ndani ya vikao ya Kamisheni husika.
4.     Kufanya lolote lile ambalo ni kwa faida ya wanamichezo kwa ujumla wake.

Kamisheni yetu ya Kitaifa tangu ianzishwe mwaka 2006 na wajumbe wake Kitaifa kuchaguliwa tena mwaka 2012 mjini Dodoma  imechelewa kwa kiasi fulani kutokana na sababu ambazo ni pamoja na kukwamishwa na viongozi wa Vyama/Mashirikisho yao Kitaifa (NFs).

Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Kawaita mjini Zanzibar leo Alhamisi.
Wanamichezo wana uwezo mkubwa wa kushauri viongozi wa vyama/mashirikisho yao katika masuala yanayohusu maendeleo ya michezo, pia kushauri mashirika mbalimbali kuhusu ajira za wanamichezo pamoja na hali ya baadaye mchezaji mhusika anapostaafu.

Mhe. Mgeni Rasmi, michezo kwa sasa ni ajira, ndiyo maana IOC imehamasisha NOCs kuunda Kamisheni za Wanamichezo ili watambuliwe kuwa sekta muhimu ya maendeleo ya michezo katika Taifa letu.

TOC  inaamini kwamba kukiwa na uwakilishi wa wanamichezo katika vyama/mashirikisho ya michezo na asasi za umma nchi yetu itakuwa imepiga hatua katika kupiga vita madawa ya kuongeza nguvu katika michezo ambayo kwa sasa yamepamba moto duniani.
Baadhi ya waalikwa katika mkutano Mkuu wa Kamisheni ya Wachezaji Tanzania (Kawata) Kutoka kushoto Irine Mwasanga, Peter Mwita na Mwinga Mwanjala wakati wa mkutano huo leo Zanzibar.
Mhe. Mgeni Rasmi, bado vyama/mashirikisho ya michezo ya kutothibitisho yanaendelea. Mwaka huu kutoka Bara ni Vyama/Mashirikisho ya Kuogelea, Mpira wa Magongo na kwa Zanzibar Mpira wa Meza na Kikapu havikuthibitisha, lakini wakatma washiriki. Riadha Tanzania kuwasilishwa na wajumbe 3 (wm 2, mk 1).

Kwa haya machache naomba nikukaribishe ili uzungumze na wanamichezo walio mbele yako kisha utufungulie Mkutano huu wa Kamisheni ya wanamichezo kwa mwaka 2015 kama tulivyokuomba.


Ahsanteni kwa kunisikiliza.




Katibu Mkuu wa TOC Filbert Bayi akifuatilia jambo na mjumbe wa Kamati ya TOC Irine Mashanga wakati wa Mkutani Mkuu wa Kawata Zanzibar leo.
 



Katibu msaidizi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Jamal Adi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kamishenu ya Wachezai (Kawata) leo Zanzibar. Kulia kwa Adi ni Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi.

HOTUBA YA MGENI RASMI WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA KAMISHENI YA WACHEZAJI TANZANIA (KAWATA) ULIOFANYIKA LEO DESEMBA 10 ZANZIBAR



 
Ndugu Gulam A. Rashid, Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania,

Ndugu Filbert Bayi  Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania,

Ndugu Viongozi wa Kamisheni ya Wachezaji Tanzania,

Wageni Waalikwa,

Mabibina Mabwana.

Awali ya yote, napenda kutoa shukrani zangu kwa viongozi wenzangu wa TOC
kwa kunishirikisha na kunipa heshimahiiyakuwamgenirasmiwakuufunguaMkutanohuumuhimuwaKamisheniyaWachezaji Tanzania.

Kwanza naipongezaofisiyetuyaKamatiyaOlimpiki Tanzania kwakutekelezamaagizoyaKamatiyaOlimpikiyaKimataifayakuzitakaKamatizaOlimpikizaKitaifakujumuishawachezajikwenyeKamatizakezaUtendaji, naMikutanoMikuuyakehalikadhalikanaVyama/MashirikishoyaMichezowanachamawa TOC ambaomichezoyaoipokwenyeratibayaMichezoyaOlimpiki(Summer/Winter).

Ni matumainiyanguwengiwawawakilishiwaliohapaniwajumbehalaliwaliochaguliwanawachezajiwenzaondaniyaVyama/Mashirikishoyamchezohusikakwanjiayademokrasianasiyokuteuliwanaviongoziwavyama/mashirikishoyamichezoyenu, vile vilekutokaamadarakanizaidiyamudawauongoziambaoukokwenyemwongozowenukamamlivyoelekezwanaKamatiyaOlimpikiyaKimataifa (IOC) kupitiaKamatiyaOlimpikiyaTanznaia (TOC).

NatoawitokwaviongoziwaKamisheniyaWachezajiwanaowakilishavyama/mashirikishoyamichezokusaidiananaviongoziwaVyama/Mashirikishohusikailikamahavipohai, basiwajitahidikuvifufuakwamaanayakufanyauchaguzikwamudamuafakakufuatakatibazao. Kuna michezominginehufakutokananakutokuweponamsukumokutokawadauwavyama /mashirikishoyamichezoambaoniwachezaji. ViongoziwaKamishenikatikavyama/mashirikishovinawajibuwakusaidiamaendeleoyamichezokatikataifaletukupitiavyamanamashirikishoyao. Kamishenizilizochaguliwanazilizopoziwezekutoachangamotoyaushauriwanamnayakuendeshamichezonchini, kwanihadiduzarejeazakazizaonipamojanakuamshaariyawachezajiwenginewakitaifanakimataifakatikakufikiamahalipazuri pa kupatawachezajiwatakaowakilishavilabu, vyamanamashirikishoyetukatikangazimbalimbalizamashindano.KAWATA kuanziangaziyaVyama/MashrikishoyaMichezohadiTaifahaziwezikukwepalawamawakatitimuzetuzinapofanyavibayakatikaMashindanoyaKimataifa.

Nimefahamishwakuwawachezajiwengipamojanakwambammekamilikahapakuhudhuriamkutanohuu, lakinindaniyavyama/mashirikishoyenuhampewinafasiyakuwamojawawajumbewaKamatizaUtendajizaVyama, MashirikishonaVilabuvyamichezonakuwananafasiyauwakilishiwenyekurakatikaMikutanoMikuu.Ndaniyanafasihizokunamaamuzimengineyanawahusuwachezajiambaondiyowadauwakubwawavyombovyetuvyamichezohapanchini, lakinimaamuzihayoyamekuwayakiamuliwanaviongoziwavyama/mashirikishoyamichezo,ndiyomaanaTOC naIOC wakalionahilinakuamuawawepowawakilishiwaWachezaji. Ni matumainiyangukamamojawaviongoziwa TOC,VyamanaMashirikishoyaMichezo Tanzania Bara na Zanzibar wametekelezamaagizoya IOC kwafaidayaMichezokatikanchiyetu. .
  
Viongozi wa Kamisheni ya Wachezaji Tanzania Kawata), Katib u Mkuu Amina Ahmed (kushoto) na mwenyekiti wake, Ramadhabi Zimbwe pamoa na Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kawata leo Zanzibar.
Binafsi, ninaungakabisaumuhimuwaKamisheniyaWachezajikatika TOC, Vyama/MashirikishonaVilabuvyaMichezo, huuniuamuzimzuriwaKamatiyaOlimpiki Tanzania (TOC)naKamatiyaOlimpikiyaKimataifa (IOC), nanikatikakukamilishaazmayamaadiliyaOlimpikihasakuwapawachezajihakiyakutoamawazoyaokatikaKamatizaUtendajizaVyama/Mashirikishona TOC. 


PiaKamishenikupitiaVyama/MashirikishoyetuyaMichezoipingekwanguvuzoteutumiajiwamadawayakuongezanguvukatikamichezoambakokwasasaumeongezekakwakasi.Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF) imeshaanzakupambanananchiambazowanariadha wake wamekuwawakitumiamadawayakuongezanguvukatikariadha.

KamisheniivihamasisheVilabunaVyamavyaMichezokuwanaKamishenizaoilizisaidiemaendeleoyamichezohapanchini, msikubalidaimakutumwakatikamikutanokamahiikwakuteuliwabilakuchaguliwa.

KwahayamachachesasanikotayarikufunguarasmiMkutanowenunakuwatakiakila la kheri.


Ahsanteni kwa kunisikiliza.
 
Baadhi ya wajumbe wa Kamisheni ya Wachezaji Tanzania (Kawata) wakiwa katika mkutano mkuu wao leo Zanzibar.

Wednesday, 9 December 2015

Mourinho: Kila timu inataka kucheza na Chelsea katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya



LONDON, England
KOCHA WA Chelsea Jose Mourinho anaamini kuwa wapinzani wao katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kila moja anataka apanwe na timu yake katika hatua ya 16 bora.

The Blues wamemaliza washindi wa Kungi G baada ya jana usiku kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Porto, ikiwa na maana kuwa wanatarajiwa kupangwa dhidi ya moja ya timu sita zilizomaliza katika nafasi ya pili katika makundi yao
Ratiba hiyo ya hatua ya 16 itapanwa Jumatatu.

Chelsea inaweza kupanwa ama na Paris St-Germain, Juventus, PSV Eindhoven, Benfica, Roma au Gent.

"Kila timu iliyomaliza katika nafasi ya pili inataka kucheza na sisi (Chelsea) au Zenit St Petersburg," alisema Mourinho mwenye umri wa miaka 52.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wamekuwa na wakati mgumu katika ligi hiyo ya nyumbani ambapo wamepoteza mechi nane kati ya 15 walizocheza katika ligi hiyo msimu huu na kujikuta wakiwa katika nafasi ya 14.

Lakini timu hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika mashindano ya Ulaya ambapo imeshinda mechi nne na kutoka sare moja katika mechi zao sita za hatua ya makundi na kutina hatua ya mtoano ya michuano hiyo.

The Blues walikata tiketi ya kucheza hatua hiyo ya 16 bora kupitia kwa Ivan Marcano aliyejifunga katika kipindi cha kwanza huku bao safi la Willian akilifunga baada ya mapumziko.

"Kila timu inaogopa kucheza na Barcelona, hawataki kucheza na Real Madrid, hawataki kucheza na Atletico, hawapendi kusikia wanapanwa kucheza na Bayern Munich," aliongeza Mourinho.

Mourinho ana nia ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa mara tatu taji la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na klabu tatu tofauti, ambapo aliziongoza Porto na Inter Milan kutwaa taji hilo mwaka 2004 na 2010.

Na kocha huyo Mreno anasema Blues, licha ya kufanya ibaya katika ligi ya nyumbani, inaweza kuwazishangaza zile timu zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

"Timu ambayo inachechemea ni wazi sio mshindani katika mbio a ubingwa kwa sababu kuna timu bora zaidi Ulaya alisema ourinho, ambaye aliwahi pia kuiongoza Real Madrid kati ya mwaka 2010 na 2013.

"Lakini hata tulipotwaa taji na Porto hatukuwa washindani. Na hata tulishinda na Inter Milan hatukuwa washindani wa taji hilo.

"Wakati tulipokuwa washindani tuliwa na Real Madrid tulishindwa katika robo fainali, na tulipoteza nusu fainali mbili na Chelsea.

Muhimu: Timu nane zilizoshikamnafasi ya kwanza katika makundi yao zinapanwa na nane zilizoshika nafasi ya pili, inawa timu kutoka nchi moja kamwe haziwezi kupanwa pamoja katika hatua hiyo ya 16 bora,

Pia timu zilizowahi kukutana katika hatua ya makundi haziwezi kupanwa pamoja katika hatua hiyo inayofuata.

Kutokana na utaratibu huo inamaana kuwa Chelsea haiwezi kucheza dhidi ya Arsenal au Dynamo Kiev katika hatua hiyo ya 16 bora.

TIMU ZILIZOFUZU KWA 16 BORA:

Real Madrid, Paris St-Germain, Wolfsburg, PSV Eindhoven,
Atletico Madrid, Benfica,Manchester City, Juventus,Barcelona,
Roma, Bayern Munich, Arsenal, Chelsea, Dynamo Kiev, Zenit St Petersburg na Gent.

Giroud afunga hat-trick Arsenal ikitinga kwa kishindo hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya



Olivier Giroud alikuwa shujaa wa Arsenal wakati alipofunga hat-trick na kuiwezesha Arsenal kuifuna Olympiacos na kutinga hatua ya mtoano ya 16 bora

ANTHENS, Ugiriki
LIVIER Giroud alifunga mabao matatu mwenyewe (hat-trick) wakati Arsenal ikijihakikishia nafasi ya kufuzu kwa hatua ya  16 bora ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwa kuifunga Olympiakos mabao 3-0.

Ikihitaji ushindi wa mabao angalau mawili kwa bila ili ifuzu kwa hatua hiyo, the Gunners ilionesha kiwango kizuri na kujikuta ikimaliza ya pili katika Kundi F.

Giroud alifunga la kwanza katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo kabla hajafunga tena katika kipindi cha pili baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Joel Campbell.

ARSENAL YAENDELEZA REKODI
Arsenal haijawahi kushindwa kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya tangu michuano hiyo ilipoanza mfumo mpya katika msimu wa mwaka 2003-04, na uzoefu wao ulidhihirika usiku wa jana katika mchezo huo uliofanyika jijini hapa.

Arsenal iliuanza mchezo huo kwa kasi huku wenyeji wakicheza na kuungwa mkono na mashabiki wa nyumbani waliokuwa wakishangilia bila kuchoka.

Mathieu Flamini alikaribia kufunga baada ya mpira alioupiga kugonga mwamba kabla Giroud hajafunga la kwanza kwa kichwa cha karibu na lango akiunganisha krosi ya Aaron Ramsey.
Giroud akifunga kwa kichwa katika dakika ya 29 dhidi ya Olympiacos katika mchezo dhidi ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya katika mchezo wa Kundi F
Bao la pili lilikuwa bora kwa usiku huo wakati Giroud alilifunga baada ya kukimbia na mpira kutoka katika mstari wa nusu ya uwanja kabla hajapiga na kuujaza mpira wavuni.
Bao la tatu ni la penalty, ambapo Omar Elabdellaoui aliunawa mpira uliopigwa na Nacho Monreal na Giroud alifunga kirahisi.

NINI KINACHOFUATA?
Arsenal ilifanya vizuri na kufuzu baada ya kufungwa mechi za awali mbili dhidi ya Dinamo Zagreb (2-1 ugenini) na  Olympiakos (3-2 nyumbani) ikiwa na maana kuwa ilishindwa kabisa kupata hata pointi moja katika kundi lao baada ya kucheza mechi mbili.

Timu hiyo iliendelea kupata kisago kwa kufungwa 5-1 na mshindi wa kundi hilo, Bayern Munich katika mchezo uliofanyika Ujerumani baada ya kushinda 2-0 dhidi ya kikosi cha kocha Pep Guardiola katika mchezo uliofanyika England.

Sasa wamemaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Bayern ikiwa na maana kuwa timu hiyo sasa itakutana na ratiba ngumu wakati wa upangaji wa ratiba hiyo ya 16 bora ukilinganisha na timu hiyo ya Ujerumani.

Timu inazoweza kukutana nazo ni pamoja na vigogo ya Hispania Real Madrid, Atletico Madrid na Barcelona, Wolfsburg kutoka Ujerumani au ile ya Russia ya Zenit St Petersburg.

Wataungana na ndugu zao wa Chelsea na Manchester City katika ratiba hiyo itakayopangwa Jumatatu

UNACHOTAKIWA KUJUA
Olivier Giroud ni mchezaji wanne wa Arsenal aliyewahi kufunga hat-trick katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya (baada ya Thierry Henry, Nicklas Bendtner na Danny Welbeck).

Hii ni mechi ya kwanza kwa kikosi cha Arsene Wenger kushinda nchini Ugiriki tangu Desemba mwaka 1998 (wakati walipoifunga Panathinaikos kwa mabao 3-1).

Matokeo hayo yanamaliza umwamba wa kutofungwa kwa timu hiyo ya Ugiriki dhidi ya zile za Uingereza