Sunday, 24 January 2016

TAARIFA KWA WANAYANGA KUPITIA VYOMBO YA HABARI ILIYOTOLEWA NA MAJI LEO JUMAPILI JANUARI 24

Mwenyekiti wa Yanga Yussuf Manji akizungumzana waandishi wa habari. Kushoto ni Makamu wake, Sanga.
1. Baada ya kuupitia uamuzi wa Kamati ya Nidhamu kuamua sababu kuvunja mkataba kati ya klabu Yanga na mchezaji Haruna Niyonzima, nilihisi kulikuwa kuna kasoro hasa kwa mchezaji anayelipwa mshahara wa Sh milioni 6 anaweza vipi kupuuzia maisha yake na kuanzisha mgogoro usiokuwa na tija kwa maisha ya kipato. (angalia kiambatanisho 1)
 
Niliamua uchunguzi wa ndani ufanyike katika suala hilo zima na mwisho, Jonas Tiboroha alibainika kuwa hakuwasilisha ushahidi ya mawasiliano sahihi kwa Kamati ya Nidhamu kuhusiana na Haruna Niyonzima, hali iliyosababisha kamati kuchukua uamuzi ambao haukuwa sahihi kwa sababu;
 
Kulifanyika mambo ambayo hayakuwa sahihi, mfano barua za Niyonzima kutoka kwa Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa) ambazo zilitumwa kwa TFF na kupokelewa kama ambavyo Azam FC walipokea ya mchezaji wao kupitia kwa Afisa Mtendaji Mkuu wao. Lakini barua ya Niyonzima kuja Yanga, ilionekana haikupokelewa kama ilivyokuwa kwa barua yake ya utetezi na ile ya kuomba radhi alizoandika, nazo zilipokelewa lakini hazikuwasilishwa kwenye kamati ya nidhanmu na hili, mhusika ni Tiboroha. Ukiachana na kamati kufanya uamuzi usio sahihi, hili pia limemjengea mchezaji chuki kubwa kwa wanachama na mashabiki. (angalia kiambatanisho 2 & kiambatanisho 3)
 
Kamati ya Utendaji (EXCOM), bada ya kupitia kwa kina iliona uamuzi ilichukua haukuwa haukuwa ya haki kutokana na kupotoshwa na Tiboroha tena aliendelea kuipotosha kamati kwa makusudi kutokana na kuficha nyaraka hizo ili Niyonzima afukuzwe. Tulifikia maamuzi Tiboroha alikuwa na ajenda yake binafsi.
Hii kama ilikuwa haijagunduliwa mapema, ilikuwa na hatari ya kusababisha upotevu kifedha za Yanga kulingana na kanuni za TFF/FIFA na ukilichimba suala hili kwa undani, kwa kufuata weledi. Kamwe hauwezi kusema yalikuwa ni makosa ya kibinadamu badala yake ni chuki ya kibinadamu ambayo haistahili kufanywa na kiongozi wa Klabu kubwa yenye heshima kama Yanga.
Zaidi, Katika hali nyingine, uamuzi wa Kamati ya Nidhamu uliandikwa na Gazeti la Uhuru na mwisho wa uchunguzi ulidhibitisha mtoa habari hizo alikuwa ni Tiboroha, akilenga kutaka kuuchafua uongozi wa Klabu, mchezaji mwenyewe dhidi ya jamii na kuusukuma uongozi kufanya uamuzi usio sahihi kwa faida zake yeye binafsi na si klabu.
2. Aidha, EXCOM ilifanya uchunguzi wa ziada na kugundua vitendo, Tiboroha hakuweza kufikia malengo aliyekuwa ameyawekewa na EXCOM kwa kuwa zaidi alionekana kutaka kujiendeleza binafsi, kusikika peke yake na kujulikana mwenyewe kama “Mungu Mtu”, jambo ambalo lilichochea kelele ndani ya klabu kama vile yeye ni malaika:

Angalia kiambatanisho (3), eti Mwenyekiti wa Matawi (nafasi ambayo haitambuliki kwenye katiba ya Yanga), amekuwa akiniagiza kubadili nafasi za  waajiriwa, mfano ile ya (Tiboroha) ni lazima abaki kwa sababu mchango wake ni mkubwa na bila yeye hatuwezi kushinda au kufanya vizuri. Ukisoma barua yake utafikiri Tiboroha alikuwa akifanya kazi zake bure wakati anajua alikuwa ni mwajiriwa wa Klabu, tena kazi zake nyingi alikuwa akizifanya kwa kufuata “maagizo”  anayopewa kama mwajiriwa. Tayari kupinga kuondolewa kwake kumeanza kuripotiwa kwenye vyombo vya habari kama shinikizo la chinichini kupitia Msumi, huenda anafikiri kufanya hivyo inanitisha ili nibadili mambo kwa matakwa ya wasioelewa mamlaka ya Katiba. Naendelea kukumbusha Tiboroha alikuwa mwajiriwa anayelipwa mshahara (angalia kiambatanisho 4) huku mimi kama Mwenyekiti au Wajumbe wa EXCOM tumekuwa tukijitolea na kutolipwa hata posho. 
Ajabu Kichekesho zaidi, kila kizuri kilichokuwa kikifanyika, vyombo vya habari viliripoti kuwa ni kazi nzuri ya Tiboroha, lakini wakasahau kila zuri, yeye alikuwa ni mtekelezaji tu baada ya kuagizwa kutoka kwangu mimi mwenyekiti au baada ya ushauri wa kamati ya utendaji na baada ya hapo, yeye alipewa kibali cha kutekeleza jambo husika. Kila zuri lilikuwa lake, mabaya yakiwemo yale ya kuisaidia TFF kuiangamiza shingo ya Yanga, aliyeficha kapuni.
Kuna taarifa kwenye vyombo vya habari ambazo zilithibitisha wazi kuwa Tiboroha alipania kujijenga binafsi kama Katibu Mkuu Bora zaidi kuwahi kutokea Yanga; hoja potofu kwa sababu wakati akiwa Katibu, hata mwalimu wa Klabu alifanikiwa kupatikana kwa ubingwa moja tu. Lakini akasahau kabla yake, Yanga ilishachukua ubingwa mara 24. Tena, propaganda ya kuwa yeye ndiye aliyeisaidia  Klabu kusajili wachezaji wa kiwango cha juu zaidi huku akijua wazi kwamba wachezaji hao walikuwa ni pendekezo la Kocha Mkuu, huu ni uputofu wa hali ya juu kabisa. 
Ndani ya miezi yake 12 ya uongozi amechangia kushuka kwa kasi kubwa kwa mapato ya klabu huku matumizi ya klabu yakipanda mara nne zaidi kutoka Sh milioni 500 kwa mwaka hadi sasa takriban Sh bilioni 2. Kabla hajaja klabuni, tulikuwa tumekaribia kujikomboa na kuanza kujitegemea. Hii pia ni kwa yeye kukubaliana na ujinga wa kuitetea TFF ambayo mikataba yake, kwa kiasi kikubwa imeporomosha mapato yetu na kutuweka katika wakati mgumu kabisa, ajabu Tiboroha alikuwa upande huo.  
3.   Masuala ya kupotosha ya Tiboroha si mapya:
a. Wakati FIFA ilipoialika Yanga kwenye semina ya mafunzo iliyofanyika nchini Ghana, Tiboroha alijichagua mwenyewe asafiri kwa niaba ya Klabu bila kuitaarifa EXCOM, halafu akachukua “Cheti cha ugonjwa” na kukiwasilisha kwa mwajiri wake Yanga ili apate nafasi ya kusafiri kwenda nchini Ghana. Kujichagua yeye mwenyewe, ilikuwa ni kutofuata weledi.
b. Daktari (jina linahifadhiwa) aliajiriwa kwa ajili ya mechi dhidi ya MGAMBO likiwa ni pendekezo la Tiboroha, lakini baadaye Kamati ya Mashindano (baada ya kuwa imesababisha tatizo ndani ya Klabu), iligundua daktari huyo alikuwa ni mwanachama tena mwenye kadi wa Simba, akaondolewa’ pia.

c. Ngoma alipewa taarifa na Tiboroha kwamba anatakiwa kwenda kufanya majaribio na klabu moja nchini Uturuki. Tiboroha alifanya hivyo akijua Ngoma alikuwa anakwenda kushiriki michuano ya MAPINDUZI Cup, mbaya zaidi hakuwa amewasiliana na EXCOM kuhusiana na hilo kabla kumfahamisha mchezaji na kumpa taarifa hiyo. Baadaye kocha Kocha Mkuu, alilalamika kwamba kufanya vile ilikuwa ni kuondoa morali ya mchezaji katika michuano hiyo ya MAPINDUZI CUP na baada ya hapo, angekuwa akiwaza kuhusiana na Uturuki tu. Mwisho, kocha alisema, Ngoma alicheza chini ya kiwango katika michuano hiyo, akiamini Yanga inamzuia kusonga mbele kimaisha.

d. BDF ya Botswana ilianzima US$ 5,000/- ambazo hadi sasa hazijarejeshwa: EXCOM iligundua taarifa kuhusiana na deni hili, imekuwa ikifichwa na hakuna maelezo mrejesho kuhusiana hilo kutoka kwa Tiboroha ambaye amekuwa na ukaribu na wahusika kutoka Botswana.

e. Kuna mtu aliajiriwa kama Katibu Muktasi (PS) pamoja na mtu mwingine pia, lakini haikuidhinisha wala mwanasheria wa Yanga, hakutaarifiwa kuhusiana na hilo lilifanyika bila ridhaa ya EXCOM, badala yake alilifanya kwa kuwa anaona yeye ni mtu maarufu sana!

f. Hakufuata ushauri aliopewa na wataalamu wa TRA, hali iliyosababisha akaunti za Yanga kufungwa, hivyo mimi kulazimika kuanza kutoa fedha zangu za mfukoni katika uendeshaji wa Klabu kwa kipindi chote na wakati huo wachezaji walikuwa wakidai mishahara na tuko katikati ya msimu. 

g. Alikuwa akitetea maslahi ya TFF na sio Yanga na kukubali kila TFF ilichokipendekeza. Mtu mwenye akili anaweza kufanya hivyo utadhani alikuwa mwajiriwa wa TFF na si Yanga? Hii inaonyesha hakuwa akifanya kazi kwa maslahi ya Yanga kama ilivyotakiwa, angalia katika masuala dhidi ya TFF, ukijumuisha.

h. Lile la kushindwa kumpigania msemaji Msemaji wa Klabu, Jerry Murro asifungiwe na TFF, huku akimchimba huku akijua alikuwa akipitia taarifa zote kabla ya Jerry kuzitoa. Alikuwa na roho mbaya kwa kuwa Jerry alipata umaarufu zaidi kwa wanachama kutokana na kuipigania klabu.

i. Ukiangalia hayo juu, ni kati ya machache ambayo nimeona ninaweza kuyaanika kwenye vyombo vya habari, lakini yako mengi ambayo ni nyeti na haitakuwa sahihi kuyaanika kwenye vyombo vya habari kwa maslahi ya klabu. Yanga ilianza kung’amua mambo yanayomhusu Tiboroha muda sasa, alipoona mengi yamegundulika. Januari 14, 2016 aliandika barua kuomba radhi kwangu, akikiri kufanya makosa na kusema alikuwa akiyajutia. (angalia kiambatanisho 6)


4. Sisi, hatukukubaliana na kutoa msamaha kutokana na hofu ya unafiki wake, na nilitoa ushauri; kwamba vizuri akachukua hatua ya kujiuzulu mara moja na huenda ingekuwa vizuri aeleze ana matatizo ya kifamilia pia kiafya, lengo lilikuwa ni kumpa nafasi ya kuachana na Yanga kwa amani pia kuilinda familia maisha yake huko mbeleni. Lakini nilimtaka ahakikishe zile fedha tunazowadai BDF kutoka Botswana, mara moja zinawasilishwa Klabuni na baada ya hapo, rasmi atakuwa amejiondoa.

5. Tiboroha alikubaliana na hilo na kuandika barua ya kujiuzulu alioiwasilisha Januari 22, 2016 (angalia kiambatanisho 7)

6. Pamoja na kumshauri ili ajiuzulu kwa heshima, lakini alionekana kuanza kutengeneza “Presha ya wanachama” kama vile mtu aliyeonewa. Kuna mkutano wa ujanjaujanja uliitishwa makao makuu ya Klabu, Tiboroha akiwa mshiriki mkuu nyuma ya pazia, hii ilikuwa ni Januari 23, 2016. Lengo ni kutengeneza hali ya hofu kwa Wanachama, jambo ambalo si sahihi. (angalia kiambatanisho 8)

7. Kwa yote hayo hapo juu:
a. Kamati ya Utendaji (EXCOM) inapenda kutoa taarifa kuwa imevunja mkataba wa Tiboroha kama Katibu Mkuu wa Yanga.
a. Klabu inatangaza, mara moja kuwa: 
i. Baraka Deudeit atashikilia nafasi hiyo ya Katibu Mkuu wa klabu.
ii. Omar Kaya atachukua majukumu yanayohusiana na wanachama wa klabu. Pia atahakikisha anasimamia mikutano yote ya matawi, kusaidia maandalizi ya uchaguzi ujao pamoja na masuala ya wanachama wapya.
iii. Jerry Muro ataendelea kubaki katika nafasi ya msemaji wa klabu,
iv. Faidhal Mike ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha cha Klabu, akisaidiwa na Justina ambaye amepandishwa cheo na kuwa mhasibu mkuu msaidizi,
 
v. Klabu ipo katika kipindi cha kuboresha kitengo cha masoko cha klabu na hivi karibuni itatangazwa lakini kabla ya hivyo, Omar atashikilia kwa muda kitengo hicho.
vi. Mwanasheria Frank Chacha kama mkuu wa kitengo cha Sheria Klabuni, yeye tunamuacha aendelee na mambo yake na masuala yote ya kisheria, klabu itayafanya kutumia wanasheria, nje ya klabu.

8. Kuhusiana na uchaguzi na maneno ya kinafiki ya nungunungu ya chinichini kuwa eti ninaogopa uchaguzi; huku wakiwa hawajui kuwa katika maisha yangu sijawahi kushindwa uchaguzi: Ukweli mimi ndiyo nimekuwa nikusukuma kuitishwa kwa uchaguzi uitishwe ili nistaafu kupitia nafasi yangu ya uenyekiti. Nilimwaandika Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, kuitisha uchaguzi mara moja, akishindwa basi itabidi niivunje Kamati ya Uchaguzi na kuunda nyingine. (angalia kiambatanisho 9)

9. Kutokana na kuuguliwa na baba yake mzazi, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi alishindwa kutekeleza hilo na akaamua kujiuzulu. (angalia kiambatanisho 10)

10. Ikiwa ni sehemu ya majukumu yangu, kwa ushauri wa EXCOM niliomba kwao majina mapya ya Kamati ya Uchaguzi ili mchakato ufanyike (angalia kiambatanisho 11)
Hitimisho, nimegundua potofu ya kufikiri Tiboroha ni Katibu Mkuu wa kuchaguliwa, badala yake ni mwajiriwa wa kawaida ambaye aliingia mkataba kwa maslahi ya mapato yake. Tena kosa kumchukulia kama mtu ambaye amekuwa akitoa fedha zake za mfukoni kwa ajili ya kuendesha Klabu, mtu ambaye mimi nilipendekeza aajiriwe kama nililivyopendekeza kwa Mwalusako, Njovu, Mwesigwa, Maximo na wengine na nina mamlaka ya kuamua hatma ya mwajiriwa kulinda heshima na maslahi ya Klabu.
 
Kwa sababu mimi nimewekea dhamira ya uchaguzi ufanyike kwa haraka, huu unaweza ukawa wakati mwafaka wa wanachama kumpa Tiboroha imani ya kura zao ili awanie nafasi Mwenyekiti wa Klabu na wanipe uhuru wangu wa kuendelea na mambo yangu mengine, ambayo yapo karibu na moyo wangu kama vile kusaidi mandeleo ya Mbagala Kuu.
 
Katika maisha yangu, sijawahi kutanguliza au kupigania cheo, ndani ya Yanga maendeleo yanaonekana lakini wapo watu ndani ya Yanga wanaona mandeleo ipo kwake. Basi tuache demokrasia itawale; lakini na mimi nitatangaza kugombea tena nafasi hiyo, ingawa sidhani kama nitamaliza kipindi chote cha uongozi iwapo nitashinda kwa kuwa kutoka awali nilieleza Yanga kuwa yenye mafanikio ni katika Ligi ya Mabingwa Afrika lakini hilo halitawezekana bila ya Klabu kumiliki uwanja wake binafsi pale Jangwani.
  Daima Mbele, Nyuma Mwiko _____________ YUSUF MANJI (MWENYEKITI YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB)

Saturday, 23 January 2016

Balozi wa Kuwait azindua kisima katika shamba la Mrisho Mpoto katika kijiji cha Kibogolwa, Mkuranga



Balozi wa kuwait nchini Tanzania, Jasem Alnajem (wa pili kushoto), akizindua kisima walichomjengea msanii mahiri wa mashahiri, Mrisho Mpoto kushoto) katika kijiji chake huko Mkuranga leo Jumamosi

Na Mwandishi Wetu, Mkuranga
SERIKALI ya Kuwait imeahidi kuwasaidia wananchi wa kijiji cha Kibogolwa kitongoji cha Kibamba Mkuranga mkoani Pwani, ili kuharakisha maendeleo katika eneo hilo.

Hayo yalisemwa leo na Balozi wa nchi hiyo nchini Tanzania, Jasem Alnajem wakati akizindua kisima kirefu kilichojengwa
 katika shamba la msanii nguli wa mashahiri, Mrisho Mpoto ``Mjombakijijini hapo.
Mrisho Mpoto akizungumza katika kijiji cha Kibogolwa, Kibamba Mkuranga leo wakati balozi wa Kuwait akizindua kisima katika mradi wa msanii huyo wa Kutoka Shambani.
Kisima hicho ni sehemu ya mradi wa Kutoka Shambani wa Mjomba uliopo katika zaidi ya hekali 40 akiwa na lengo la kuanzisha shughuli kubwa za kilimo kwa vijana wasio na mbele wa nyuma.

Balozi Alnajem akijibu risala ya mwenyekiti wa kijiji hicho, Salima Mussa aliyesema wanakabiliwa na matatizo kibao yakiwemo ya watoto wao kusoma mbali, kutokuwa na msikiti, zahanati na barabara mbovu.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem alnajem akifungua maji na watoto wakati wa kuzindua kisima Mkuranga leo.
Alnajem alisema suala la zahati watalidajili ili kuona jinsi gabi watakavyo lishughulikia wakati lile la madrasa na msikiti alisema hilo hakina shaka watapajengewa mara moja.

Karibu kaya 150 zitanufaika na maji hayo, ambayo kisima chake kimegharimu kiasi cha zaidi y ash. Milioni 12.

Mratibu wa Mpoto Foundation, Mwalimu Steph (kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhiwa kisima na balozi wa Kuwait, Jasem alnajem (kulia) katika kijiji cha Kibogolwa leo Jumamosi.
Naye mratibu wa mradi huo uliopo chini ya Mpoto Foundation, Mwalimu Steph aliushukuru ubalozi wa Kuwait kwa kuwachimbia kisima hicho na kukubali kutatua matatizo mbalimbali ya taasisi hiyo pamoja na yake ya wanakijiji.

Alisema kuwa mradi huo utasaidia kukomboa vijana wengi ambao hawana cha kufanya mitaani na kubaki kujiingiza katika masuala ya dawa za kulevya na ulevi mwingine.

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania baada ya kumtwisha ndoo ya maji mwanakijiji mmoja wa kibogolwa leo Jumamosi baada ya kuzindua kisiwa kilichojengwa kwa msaada wa nchini yake.
Nao wananchi wa eneo hilo wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti waliishukuru Kuwait na kusema maji hayo yatawapunguzia sana na matatizo ya kwenda mbali kuchota majia, ambayo pia hayakuwa salama.

Mussa alisema kuwa walikuwa wakitumia muda mwingi kwenda kusaka maji na kushindwa kufanya kazi zingine za kimaendeleo.
 
Katika mradi wa Kutoka Shambani, Mpoto kwa kuanzia ataanza na vijana 50, ambapo tayari kuna maombi ya vijana 3,500 wanaotaka kuingia katika mradi huo, utakaowawezesha kujifunza kilimo na sanaa.

 
 
 
 

 

Sunday, 3 January 2016

Sherehe za Mapinduzi Zanzibar zazinduliwa kwa usafi wa mazingira kitaifa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (kushoto) akizoa taka leo wakati wa zoezi la usafi wa Mazingira katika soko la Mbogamboga la Mombasa mjini Zanzibar ikiwa ni uzinduzi wa sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akifanya usafi ikiwa sehemu ya uzinduzi wa miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo mjini humo.

Akudo Impact, Mashauzi Classic, Utalii Sound Band walivyokonga nyoyo mwaka mpya wa 2016

Muimbaji mahiri wa Akudo Impact, Ziggy Ston akiimba wakati kundi hilo likitumbuiza Msasani Beach siku ya mwaka mpya Ijumaa Januari Mosi, 2016.
Baadhi ya madansa wa Akudo Impact wakiongozwa na Christina Ngowi (kushoto) kabla ya kupanda stejini siku ya mwaka mpya Msasani Beach Club Januari Mosi.

Wapenzi wa muziki wa taarab wakicheza wakati kundi la Mashauzi likitumbuiza katika ukumbi Lunch Time Manzese jijini Dar es Salaam siku ya mwaka mpya Januari Mosi, 2016.
Baadhi ya waimbaji wa kundi la taarab la Mashauzi lilipotumbuiza katika ukumbi wa Lunch Time Manzese jijini Dar es Salaam siku ya mwaka mpya wa 2016.  
Isha Mashauzi; Kiongozi wa kundi la Mashauzi akiimba siku ya mwaka mpya katika ukumbi wa Lunch Time Manzese jijini Dar es Salaam.
Mpiga rythm, Duncan Ndumbalo wa kundi la Utalii Sound Band akifanya vitu vyake wakati wa Siku ya Mwaka Mpya kwenye ukumbi wa Mikocheni Resort Centre (MRC). 
Baadhi ya waimbaji wa Utalii Sound Band wakiongozwa na Elibariki Kunukula (kulia) wakati kundi hilo lilipotumbuiza katika ukumbi wa Mikocheni Resort Centre (MRC) wakati wa mwaka mpya.
Muimbaji wa Utalii Sound Band, Zulfa Omary akiimba wakati kundi hilo lilipotumbuiza katika ukumbi wa Mikocheni Resort Centre (MRC) wakati wa siku ya Mwaka Mpya Ujumaa Januari Mosi.

Friday, 1 January 2016

Rais Magufuli awaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wakuu wake leo Ijumaa Januari 1, 2016

Rais DKT John Pombe Magufuli akimuapisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi katika afra iliyofanyika ikulu jijini Dara es Salaam leo Ijumaa Januari mosi, 2016.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amjulia hali Muadhama Kadinali Polycarp Pengo Muhimbili leo Januari Mosi 2016

Rais wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli na mkewe, Mama Janeth wakimjulia hali askofu mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam, mudhama Kadinali Polycarp Pengo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili leo ambako yuko kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake. Askafu huyo alilazwa ana jioni.

Mh. Profesa Mbarawa ataka Taasisi Viwanja vya ndege ziwajibike kwa TAA




WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh.Prof.  Makame Mbarawa ameagiza  watumishi wa Tassisi  zote  zinazotoa  huduma katika viwanja vya ndege  hapa nchini kuwajibika kwa Mameneja  wa Mamlaka  ya Viwanja vya Ndege  (TAA)  wanaosimamia  viwanja  ambavyo  watumishi hao wamepangiwa  kufanya  kazi. 

Mh. Mbarawa ametoa agizo hilo jana wakati alipofanya ziara ya siku moja kwenye Makao Makuu  ya  TAA  ambapo  pamoja na mambo mengine  alikagua  ujenzi unaondelea wa jengo la tatu la abiria (TBIII), na  kituo cha Zimamoto na Uokoaji. Pia  alitembelea mradi  wa usimikaji wa vivuko vipya vya abiria (Passenger Boarding  Bridges) na  usimikaji wa mitambo mipya ya kufua umeme wa dharura (Standby Generators) iliyopo katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

Mkurugenzi wa  Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman akimuonesha kitu Prof. Makame Mbarawa wakati alipotembelea TAA jana.
Akizungumza  na menejimenti ya TAA ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi  Suleiman S. Suleiman  katika Ofisi  za TAA  ikiwa ni sehemu ya majumuisho ya ziara yake, Prof. Mbarawa  aliwapongeza TAA kwa kazi nzuri wanayoifanya hususan  katika uboreshaji wa muindombinu na kuhudumia wateja. Hata hivyo alisema pamoja na sifa hiyo nzuri, kuna haja kwa TAA kuwa mdhibiti wa taasisi nyingine zote  zinazofanyakazi katika viwanja vya  ndege hapa nchini kama njia ya  kuepuka kuchafua sifa nzuri ya viwanja hivyo na nchi kwa ujumla.

“ Pamoja na kazi nzuri mnayoifanya,nadhani  wakati umefika sasa kwa taasisi zote zinazotoa huduma katika viwanja vya ndege hapa nchini  ziwe chini ya TAA”,  alisema  Prof. Mbarawa  huku akisisitiza umuhimu wa  taasisi hizo kufanya kazi  kwa kushirikiana  kama timu moja.  “Nyinyi ndio kioo katika jamii yetu, taasisi nyingine mfano uhamiaji wakachelewa kugonga mhuri kwenye hati za kusafiria, watu hawatambui kama ndio wao waliochelewesha na lawama watawatupia nyinyi,” alisisitiza Mh. Mbarawa na kuongeza kwamba anafanya utaratibu wa kuwasiliana na Wizara zote zinazohusiana  na taasisi hizo ili kupanga utaratibu muafaka.

Mbali na idara ya uhamiaji,  taasisi nyingine zinazotoa huduma kwenye viwanja vya ndege ni pamoja na Idara ya maliasili,  afya, kilimo, mifugo, madini,  polisi na kitengo cha kuzuia madawa ya kulevya.  
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo ya uboresha unaoendelea wa terminal Two kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Suleiman Suleiman jana
Mh. Mbarawa  pia  ameiagiza  TAA kubuni  mikakati  ya kuongeza ukusanyaji wa mapato zaidi ili iweze kujiendesha na pia ihakikishe kuwa inaepukana  na matumizi yasiyo ya lazima. Aliitaka watumishi wa TAA  kuzingatia uadilifu na weledi katika utendaji wao wa kazi na kuhudumia wateja  ikizingatiwa kuwa viwanja vya ndege ni kioo cha nchi.

“Nisingependa taarifa za matukio mbalimbali yanayotokea kwenye viwanja niyasikie au kuyaona kwenye vyombo vya habari wakati mimi mwenyewe sijui, hivyo tujenge utamaduni wa kuwa waadilifu na tufanye kazi kwa kuzingatia weledi, tuepukane na matukio ya hovyo,” alisisitiza Mh. Mbarawa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi Suleiman alimhakikishia Waziri Mbarawa kutekeleza maagizo yake, likiwemo la kubuni mbinu mpya za mapato, na hata kuweka utaratibu wa kumpatia taarifa mbalimbali zinazotokea kwenye viwanja kabla hazijapelekwa sehemu nyingine yeyote, kwa ajili ya utekelezaji na kujenga uhusiano mzuri baina ya mamlaka na wizara kwa ujumla.

“Kuhusu mapato tunauhakika wakati wa jengo la tatu la abiria likifunguliwa yataongezeka, lakini tunaahidi kubuni mbinu nyingi zaidi, ili  tuwe na vyanzo vya uhakika vya mapato,” alisema Mhandishi Suleiman. Alisema kukamilika kwa jengo hilo kutaongeza idadi ya abiria watakaosafiri na ndege za ukubwa mbalimbali ikiwemo 380 Airbus yenye uwezo wa kubeba abiria 300.
Mkurugenzi wa TAA, Suleiman S. Suleiman akimuonesha Waziri Prof. Mbarawa ujenzi unaoendelea wa jengo la tatu la abiria (Terminal Three) wa uwanja huo wa ndege wa Julius Nyerere jijjini Dar es Salaam.
Awali,  Mh. Mbarawa alipotembelea ofisi za zimamoto zilizopo JNIA, alielezwa wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa na hususan  magari ya zimamoto ambayo mbali na kuhudumia viwanja vya ndege, wakati mwingine  kulazimika pia kusaidia  jamii endapo nyumba zao zinakumbwa na majanga ya  moto.

       Imetolewa na kitengo cha Habari na Mahusiano na Sheria TAA.