Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) Jumamosi kati ya watani wa jadi Simba SC dhidi ya Yanga SC
utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, huku kiingilio cha chini
kikiwa ni sh.7,000 tu.
Kiingilio
cha juu cha mchezo huo kitakua sh. 30,000, (20,000) VIP B & C, Elfu Kumi (10,000) kwa
viti vya rangi ya machungwa (Orange), na 7,000 kwa viti vya rangi ya bluu na
kijani.
Tiketi
za mchezo huo zitaanza kuuzwa Ijumaa saa 2:00 asubuhi katika vituo vya TFF
(Karume), Buguruni Oil com, Ubungo Oilcom, Kidongo Chekundu (Mnazi Mmoja),
Posta (Agip), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Taifa, Makumbusho Stand, Kivukoni
Ferry.
Mchezo
huo utachezeshwa na waamuzi wote wenye beji za FIFA, mwamuzi wa katikati
Jonesia Rukyaa (Kagera), akisaidiwa na Josephat Bulali (Tanga), Samwel Mpenzu
(Arusha), mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) huku Kamisaa wa mchezo huo akiwa
Khalid Bitebo (Mwanza).
Ligi
hiyo ya Vodacom itaendelea Jumamosi kwa michezo sita, Young Africans v Simba
(Taifa), Mbeya City v Azam (Sokoine), Stand United v JKT Ruvu (Kambarage), Toto
Africans v Kagera Sugar (CCM Kirumba), Mgambo Shooting v Tanzania Prisons
(Mkwakwani) na Majimaji FC v Mtibwa Sugar (Majimaji).
Jumapili
ligi hiyo itaendelea kwa michezo miwili, Mwadui FC v Coastal Union uwanja wa
Mwadui Complex, huku Ndanda FC wakicheza dhidi ya African Sports uwanja wa
Nagwanda Sijaon mjini Mtwara.
No comments:
Post a Comment