Tuesday, 19 September 2017

Kongamano la Kwanza Kitaifa la Usafiri wa Anga lafunguliwa Dar leo na Waziri Mbarawa

  1. Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka leo akifuatilia mada kwenye Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga, linalofanyika kwa siku mbili kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa akiongea na Balozi wa Ufaransa nchini, Bi. Malika Berak mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere katika Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga lililoanza leo.

Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (wa pili kushoto), akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa wananchi waliotembelea meza ya maonesho ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayokwenda sambamba na Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga linalofanyika kwa siku mbili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Prosper Tesha  (kulia) akiwa na Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Prof. Zacharia Magnilwa  (katikati), wakimsikiliza Mhandisi Kedrick Chawe, kwenye  maonesho yanayokwenda sambamba na Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (mwenye tai nyekundu waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kwanza la Usafiri wa Anga linalofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kushoto kwa Waziri  ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi na kulia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Bw. Hamza Johari.  

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),  Bw. Salim Msangi (mbele) leo akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Shirika la ndege Tanzania (ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi (hayupo pichani)  aliyekuwa akiwasilisha mada kwenye Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga, lililoanza leo kwenye  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Sunday, 17 September 2017

KMC yaanza vizuri LIgi Daraja la Kwanza Bara

Kocha wa KMC, Felix Minziro.
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya soka ya Mawenzi Market ya Manispaa ya Morogoro inayoshiriki kwa mara ya kwanza Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara imeshindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani baaada ya kufungwa na KMC ya Kindondoni, Jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-1.

Licha ya  kipindi cha pili Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini, Abdulaziz Abood kuwaahidi wachezaji donge nono la Sh 800,000 endapo wangeshinda mchezo huo huku ikiwa nyuma kwa  bao 1-0 hadi mapumziko ilishindwa kunyakua kitita hicho  kwa kupoteza mchezo huo kwenye uwanja wa nyumbani wa Jamhuri wa mjini Morogoro.

Bao la kwanza la Kinondoni ilipachikwa dakika ya nne na mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga  Stephen Mwasika  na lilidumu hadi mapumziko, ambbapo  kipindi cha pili dakika ya 51 vijana wa Mawenzi Market walisawazisha bao hilo kupitia mchezaji Maulid Iddi kwa shuti hafifu baada ya mpira wa adhabu uliookolewa na beki wa Kinondoni kumkuta mfungaji.

Timu ya Kinondoni ambayo ilikuwa na baadhi ya wachezaji wenye uzoefu wa Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza ikiwa na  Kocha Mkuu , Fred Felix Minziro ‘ Majeshi’ ilibadili  mfumo wa uchezaji wa  pasi fupi na kutumia pasi ndefu uliowezesha kupata  bao la pili na  la ushindi katika dakika ya 86 kupitia Cliff Athony baada ya mpira uliopingwa na Mwasika kugonga mwamba na kumkuta mfungaji huyo.

Hadi dakika 90 za mchezo huo vijana wa  KMC kutoka Kinondoni  Jijini Dar es Salaam waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao  2 -1 dhidi ya  Mawenzi Market.

Mourinho aeleza siri United kumsajili Lukaku

LONDON, England
KOCHA Jose Mourinho anaamini Manchester United ilimsajili Romelu Lukaku kwa sababu kwameweza  kulipa fedha kiasi cha fedha kilichotakiwa na Everton.

Man United walilipa kiasi cha fedha ambacho kinaweza kuongezeka hadi pauni milioni 90 kswa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Ubelgiji,ambaye leo anatarajia kupangwa katika mchezo wa Super Sunday dhidi ya Everton.

Lukaku mwanzo wake wa kucheza Old Trafford ulianza kiaina, ambapo alifunga mabao sita katika mechi sita, wakati mshambuliaji mwingine alikuwa katika mawindo ya United, lvaro Morata, alifunga mabao matatu katika mechi nne za Ligi Kuu ya England akiwa na Chelsea.

The Blues (Chelsea) walilipa kiasi cha auni milioni 6 kwa ajili ya kupata huduma ya Morata na Mourinho anahisi ni suala la fedha tu wakati linaokuja suala la mipango ya kumsajili mshambuliaji huyo, ambao klabu hiyo ilikua na kile muhimu kulipa kwa ajili ya kumsajili Lukaku.

"Sifikiri ni sababu ya ushawishi wangu, hapana, " alisema Mourinho. "Nafikiri tulilipa fedha zilizoombwa na Everton kwa ajili ya mchezaji huyo na mshahara ambao wakala wake aliuhitaji na tulimpa wakala kamisheni aliyoitaka.

"Nafikiri hiyo ndio ilikuwa sababu kubwa. Sioni sababu nyingine. Tulilia kile ambacho Everton walikuwa wakihitaji. Klabu inayomuuza mchezaji ndio inaamua kiasi cha fedha ambacho klabu inayomtaka mchezaji inatatakiwa kulia au kutoliap.

Saturday, 16 September 2017

Ismail Juma avunja rekodi ya nusu marathoni

Na Mwandishi Wetu
Mwanariadha Ismail Juma (pichani) leo Jumamosi ameweka rekodi mpya ya taifa ya Tanzania ya mbio za kilometa 21 au nusu marathoni.

Mtanzania huyo aliweka rekodi hiyo mpya ya taifa kwa kukimbia kwa muda wa dakika 59:30 katika mbio zilizofanyika Jijini Mattoni, Jamhuri ya Czech.

Rekosi ya zamani ya taifa ya dakika 59:52 ilikuwa ikishikiliwa na Dickson Marwa aliyoiweka Februari mwaka 2008 Abu Dhabi, Falme za Kiarabu.

Mshindi wa kwanza wa mbio hizo ni Barselius Kipyego wakati mshindi wa pili ni Josphat Tanui wote wa Kenya.

Manchester City yaikandamiza Watford mabao 6-0

LONDON, England

SERGIO Aguero amefunga mabao matatu au `hat-trick’ wakati Manchester City ikishika usukani wa msimamo wa Ligi Kuu ya England leo baada ya kutoa kichapo kikali cha  mabao 6-0 kwa Watford.

Awali, Watford ambao ilikuwa haijafungwa nayo pia ingeweza kuongoza msimamo wa ligi hiyo endapo ingekifunga kikosi cha kocha Pep Guardiola, lakini kilishindwa kufanya hivyo.

Kikosi cha Man City sasa kimeshinda mechi tatu na kufunga jumla ya mabao 15.

Watford baada ya kipigo hicho imebaki na pointi zake nane na kuangukia katika nafasi ya 10 ya msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha jumla ya timu 20.

Katika mechi zingine leo; Crystal Palace ilipokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Southampton, huku Huddersfield Town ikitoka sare ya 1-1 na Leicester City na Liverpool ilibanwa na Burnley kwa sare ya 1-1.

Mechi nyingine leo, Newcastle United iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Stoke City, West Bromwich Albion ilitoka suluhu na West Ham United.

Wakati huohuo, Chelsea kesho itacheza na Arsenal wakati Manchester United watakwaana na Everton kwenye Uwanja wa Old Trafford.


MSIMAMO LIGI KUU ENGLAND

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Manchester City54101621413
2Manchester United43101221010
3Chelsea43018539
4Newcastle United53026429
5Huddersfield Town52215328
6Burnley52216518
7Liverpool52219908
8Southampton52214408
9West Bromwich Albion52214408
10Watford522179-28
11Tottenham Hotspur42117347
12Arsenal420278-16
13Stoke City512256-15
14Leicester City511379-24
15Brighton & Hove Albion511347-34
16Swansea City411225-34
17Everton411226-44
18West Ham United5113410-64
19AFC Bournemouth510439-63
20Crystal Palace500508-80