Sunday, 24 September 2017

Tigo Fiesta 2017 yafunika kinoma Mwanza

 Ben Pol akifanya vitu vyake kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

NAWEZA  kusema ilikuwa shoo ya aina yake ambayo mikoa mingine ilikopita Tigo Fiesta 2017 mwaka huu haijatokea. Watu waliitikia wito kwa kuujaza Uwanja wa CCM Kirumba na kupata walichotarajia.

Ufunguzi wa jukwaa uliofanya na msanii wa kufokafoka Rosa Ree, ambaye alionesha jinsi gani anakuja kwa kasi kubwa na nyimbo zake zikiwemo mchaga mchaga na up in the air na kufuatiwa na Lulu Diva

 Sehemu ya umati wa wapenzi wa muziki waliofunika CCM Kirumba, Mwanza.

Wasanii Rostam akiwemo Roma na Stamina wao walikuja kivingine walipopanda jukwaani kila moja na baiskeli yake na kuweka kitu tofauti kwenye wimbo wao huku ama kule, kwa kweli ilikuwa burudani tosha.

Wasanii wengine waliofanya shoo iwe na bora kuliko zilizopita ni Ommy Dimpoz na Rayvanny ambao hawakushiriki tamasha zilizopita kila mmoja kwa nafasi yake alikonga nyoyo za masha
biki.

Ali Kiba akifunika.

 Msanii ambaye alifunika wote ni Alli Kiba a.k.a King Kiba kwa kweli aliitendea haki steji mashabiki hawakutaka ashuke kila wakati wanaomba arudie kibao chake 'SEDUCE' huu ni wimbo mpya wa Kiba ambao umetokea kupendwa kila kona alirudia mara tatu kutokana na maombi ya mashabiki.

 Kwa upande wa wadhamini Tigo, Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Edgar Mapande alisema mwaka huu tumeamua kudhaminj ili kusaidia vipaji vya wasanii na kuwaletea wateja wetu burudani, kadhalika kuwapatia vifurishi mara wanunuapo tiketi za Tigo Fiesta . Mteja wetu akinunua tiketi anapata Mbs 100, dakika 100 na sms 100 bure .

Tamasha linaendelea ijumaa ijayo mkoani Tabora kwenye Uwanja wa Ali  Hassan Mwinyi.






Tuesday, 19 September 2017

Tetemeko la Ardhi laua Watu 140 nchini Mexico

MEXICO CITY, Mexico

TETEMEKO kubwa la ardhi limeikumba Mexico na kupoteza maisha ya zaidi ya watu 140 na kuharibu majengo mengi katika jiji hili, imeelezwa.

Angalau watoto 21 wanahofiwa kufa na wengine wakiripotiwa kupotea baada ya shule kuanguka katika jiji hilo.

Tetemeko hilo linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa magnitude 7.1 pia limesababisha uharibifu mkubwa katika nchi za jirani.

Kwa mara ya mwisho tetemeko kubwa kama hilo liliwahi kutokea takribani miaka 32 iliyopita baada ya tetemeko kuua maelfu ya watu Mexico City.

Hilo ni tetemeko la pili kutokea baada ya lile la mapema mwezi huu ambalo lilikuwa na ukubwa na magnitude 8.1 ambalo liliua watu 90 lilitokea kusini mwa nchi hii.

Angalau watu 149 wamekufa nchi nzima, kimeeleza chanzo kimoja cha habari.

Angalau watu 55 wamekufa katika Jimbo la Morelose,kusini mwa Mexico City, huku 32 wakifa huko Pueblae. Watu 49 wanahofiwa kupoteza maisha Mexico City, huku wengine 10 wakifa katika Jimbo la Mexico, na watau wakifa huko Guerrero.

Karibu watu milioni 2 wakazi wa Mexico City wameachwa bila ya umeme huku nyaya za simu zikiwa zimeanguka. Wananchi wameonywa kutovuta sigara mitaani kwani gesi inaweza kulipuka.

Meya wa Mexico City Miguel Angel Mancera aliaimbia TV moja kuwa huduma za uokoaji zinaendelea kuchimba katika makazi 44 ili kuona kama kuna watu wamefukiwa na kifusi.

Kaimu Katibu wa Elimu Javier Treviño, alikaririwa na vyombo vya habari vya haba kuwa, watoto 21 na watu wazima wanne walikufa wakati shule ya Enrique Rebsamen iliyopo kusini mwa Mexico City ilipoanguka.

Baadhi ya wanafunzi waliokolewa, vyombo vya habari vya Mexico viliripoti, lakini wengine bado hawajapatikana.

Nyumba za gholofa, maduka makubwa na kiwanda navyo pia ni baadhi ya vitu vilivyoanguka jijini hapa.

Akihutubia kupia televisheni, Rais wa Mexico Peña Nieto alisema dharura imechukulia katika maeneo yaliyoathirika na jeshi limekwenda kutoa msaada.

Karibu sehemu zote katika jiji la Mexico, timu ya watu wa uokoaji na wake wakujitolea wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali kuwaokoa watu.

"Mke wangu yuko pale. Sijaweza kuwasiliana naye, “alisema Juan Jesus Garcia, 33, huku akitokwa na machozi jirani na jengo lililoanguka.

"Hajaweza kujibu simu na sasa tumeambia kuzima simu zetu za viganjani kwa sababu kuna gesi inayovuja inaweza kulipuka.”

Tetemeko hilo la ardhi limetokea  jijini Mexico wakati wa kumbukumbu ya miaka 32 ya tetemeko jingine la ardhi lililoua watu 10,000.


Mexico City ni moja ya majiji yenye watu wengi duniani, ambapo ina zaidi ya wakazi milioni 20 wanaoshi hapo.

Messi atupia manne Barca ikishinda 6-1

BARCELONA, Hispania

LIONEL Messi ameongeza mabao manne katika akaunti yake aliyofunga mapema msimu huu wakati Barcelona ikiendeleza kwa asilimia 100 rekodi yake ya ushindi katika Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga baada ya kuifunga Eibar 6-1 jana.

Paulinho na Denis Suarez nao pia walizifumania nyavu katia mchezo wa pili mfululizo wakati Barca ikizidi kujitanua kileleni katika ,simamo wa ligi hiyo hadi kufikia pointi saba zaidi dhidi ya wapinzani wao wakubwa, Real Madrid, ambayo leo watakuwa wenyeji wa Real Betis.

Mapema, Valencia ilipanda hadi katika nafasi ya tatu wakati Simone Zaza alipofunga mabao matatu `hat-tric’ ndani ya dakika saba wakati timu hiyo ikiisambaratisha Malaga kwa mabao 5-0.

Kocha wa Barca Ernesto Valverde alikibalisha sana kikosi chake kwa mara ya kwanza tanbgu alipoanza kuifundisha timu hiyo, ambapo alibadili wachezaji sita kutoka katika kikosi kilichocheza Jumamosi na kushinda 2-1 dhidi ya Getafe.


Messi alianza kufungua akaunti ya mabao katika mchezo huo baada ya kufunga kwa penalti katika dakika ya 21 baada ya Nelson Semedo kuchezewa vibaya  na Alejandro Galvez.

MSIMAMO LA LIGA:


PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Barcelona55001721515
2Sevilla431061510
3Valencia52309369
4Real Sociedad430111749
5Real Madrid42209458
6Atlético Madrid42208358
7Athletic Club42113127
8Villarreal42026516
9Levante41305416
10Leganés42023306
11Las Palmas420257-26
12Real Betis420257-26
13Eibar5203310-76
14Getafe411234-14
15Girona411235-24
16Espanyol411238-54
17Celta de Vigo410357-23
18Deportivo La Coruña4013511-61
19Deportivo Alavés400407-70
20Málaga5005111-100