Sunday, 9 August 2015

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania walivyohitimisha Siku kuu ya Nane Nane kitaifa Lindi 2015


Ofisa Utumishi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Fatma Matimba akitoa maelezo.

Ofisa Sheria wa TAA Nuru Nyoni akigawa vipeperushi.

Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bahati Mollel (kushoto) akitoa  maelezo kwa wanafunzi waliofika katika banda hilo kujua shughuli za siku hadi siku za mamlaka hiyo.




Mo Farah ataka majibu ya wanariadha wanaopimwa kutumia dawa za kuongeza nguvu yawekwe hadharani ili kukomesha tabia hiyo



Mwanariadha wa Uingereza, Mo Farah akionesha medali zake za Olimpiki.

LONDON, England
BINGWA mara mbili wa Olimpiki Mo Farah, amesema kuwa anataka majibu ya wachezaji wanaopimwa kama wanatumia dawa za kuongeza nguvu, yawekwe hadharani.

Farah ametaka majibu ya vipimo hivyo hadharani, huku awali akisema: 'Nimefurahia kufanya kile kitakachodhihirisha kuwa mimi ni mwanariadha safi.'

Wiki iliyopita lilidai pamoja na Shirika la Utangazaji la Ujerumani kuwa lilifanya uchunguzi katika vipimo 12,000 kutoka kwa wanariadha 5,000 na kubainisha kuwa upo udanganyifu mkubwa kutoka mwa wanariadha wanaoshiriki katika mashindano makubwa duniani.

Wanariadha wiki iliyopita walipinga matokeo ya vipimo vyao kuwekwa hadharani.
yao ya vipimo kuwekwa hadharani.

 Farah, ambaye kocha wake, Alberto Salazar amekuwa akisakamwa kuhusu tuhuma za dawa za kuongeza nguvu, tangu wakati huo amekuwa akikanusha madai hayo yaliyotangazwa na kipindi cha Panorama Juni, ikiwatuhumu wanariadha wakubwa wa Uingereza kutumia dawa hizo na kukitaka Chama cha Riadha cha nchi hiyo kutoa maelezo kuhusu tuhuma hizo.

Japan wakumbuka miaka 70 kwa Nagasaki kulipuliwa na bomu la Atomic na kuuwa watu 70,000



Mmoja wa manusurika wa bomu hilo la atomic miaka 70 iliyopita na kuuwa wato 70,000.

TOKYO, Japan
KUMBUKUMBU ya majonzi ilitawala katika mji wa Japan wa Nagasaki ambako ndege ya Marekani iliangusha bomu la atomic miaka 70 iliyopita.

Hotuba mbalimbali zilizotolewa wakati wa hafla hiyo zilimkosoa Waziri Mkuu aliyehudhiria Shinzo Abe kutokana na mipango yake ya kulegeza masharti ya jeshi la Japan.

Angalau watu 70,000 waliuawa katika shambulio hilo, ambalo lilitokea siku tatu baada ya kulipuliwa kwa bomu jingine huko Hiroshima.

Nagasaki ililipuliwa baada ya eneo lililopangwa awali kulipuliwa na Kokura, ambalo walishindwa kulifikia kutokana na mawingu kutanda.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni kutoka nchi 75 duniani, akiwemo balozi wa Marekani, Caroline Kennedy, ilianza Jumapili kwa kusomwa azimio lililosomwa na watoto.

Kimya cha dakika moja na kengele zililia wakati wa kuadhimisha mlipuko huo uliotokea mwaka 1945 saa 8:02.

Baadae Meya wa Nagasaki Tomihisa Taue alihutubia azimio la amani katika hafla hiyo. 

Aliyenusurika na shambulio la Nagasaki, Sumiteru Taniguchi, mwenye miaka 86 alielezea maumivu aliyoyapata akisema kuwa akubaliani na maelezo ya Bw. Abe.

Saturday, 8 August 2015

Floyd Mayweather aishi vituko abeba mamilioni ya dola katika mfuko kwa ajili ya maandalizi ya pambano lake la mwezi ujao

Bondia Floyd Mayweather akiweka dolali katika mfuko kwa ajili ya kulipia bili mbalimbali atakapokuwa kambini akijiandaa na pambano lake la mwezi ujao huko Las Vergas.Marekani.

Mwandishi Wetu na Mashirika
BONDIA Floyd Mayweather ameanza maandalizi ya kujiandaa kuchapana na Andre berto Las Vegas mwezi ujao huku akibeba mamilioni ya doa za Marekani kwa ajili ya maandalizi hayo.

Mayweather ambaye hajawahi kupigwa na ndiye anayeshikilia mataji ya WBC na WBA, aliweka katika mfuko mamilioni ya dola kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali atakapokuwa huko akijiandaa kwa pambano hilo.

Simba yasheherekea vizuri siku yao kwa kuifunga Club Sports Villa 1-0



Mfungaji wa bao pekee la Simba leo kwenye Uwanja wa taifa dhidi ya Club Sports Villa ya Uganda, Awadh Juma (kushoto) akikimbia kushangilia pamoja na Mganda Simon Sserunkuma.

Na Mwandishi Wetu
SIMBA ya Tanzania jana ilisherehekea vizuri siku yao (Simba Day), baada ya kuifunga Club Sports Villa ya Uganda 1-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa mahsusi za kuhitimisha wiki ya Simba Day, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Singida Mjini anayemaliza muda wake, Mohamed Dewji. Dewji hivi karibuni alitangaza kutogombea kiti hicho tena.

Ushindi huo ni mwanzo mzuri kwa kocha Muingereza Dylan Kerr ambaye hivi karibuni alilalamikia ubutu wa safu yake ya ushambuliaji timu hiyo ilipokuwa kambini Zanzibar, ambako ilicheza mechi kadhaa za kirafiki.

Bao hilo pekee lilifungwa na Awadhi Juma katika dakika ya 90 ya mchezo huo baada ya kutokea piganikupige langoni mwa Club sports Villa.

Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi lakini jitihada zao za kusaka bao zinakwamishwa na Hamisi Kiiza ambaye alishindwa kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 13 baada ya kupata nafasi nzuri lakini anachelewa kufanya maamuzi na beki wa Club Sports Villa, Mbowa Paul anauokoa.

Villa wanajibu mapigo katika dakika ya 17 wakati Achema Robert anakuwa katika nafasi nzuri ya kufunga, lakini anapaisha mpira nje ya lango.

Dakika ya 23 Simba iliendelea kukosa mabao wakati Mussa Mgosi akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga, alipiga mpira nje.

Dakika mbili baadae, Kiiza alipata mpira lakini kabla ya kulifia lango, mpira huo unazuiwa na beki mmoja wa Villa.

Villa ilipata pigo baada ya mchezaji wao, Waibu Yesenikutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea Ibrahim Ajibu.

Dakika ya 55 Simba wanakosa tena bao wakati Mgosi lakini anapiga shuti linalodakwa kirahisi na kipa wa Club Sports Villa, Odongo Steven, huku Mohamed Hussein akipiga shuti nje ya 18 na kutoka nje ya lango.

Kikosi Simba: Vicent Angban, Ramadhani Kessy/Emiry Nimuboma, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Justuce Majbva/Haji Nuhu, Said Ndemla, Ibrahim ajibu/Mwinyi Kazimoto,Hamisi Kiiza, Mussa Mgosi na Peter Mwalyanzi/Simon Sserunkuma.