Wednesday, 13 May 2015

Barcelona yafungwa na Bayern, yatinga fainali Ulaya



 
BAYERN Munich, Ujerumani
MABINGWA wa Ujerumani, timu ya Bayern Munich jana usiku ilitupw nje ya mashindano ya ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Allianz Arena katika mchezo wa pili wa nusu fainali.

Katika mchezo wa awali, Barcelona ilishinda 3-0 na hivyo timu hiyo ya Hispania imesonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-3.

Barca sasa itamsubiri mshindi wa jumla kati ya Juventus na Real Madrid kwa ajili ya kucheza fainali itakayofanyika baadae mwezi huu.

Katika mchezo wa kwanza, Juventus iliibuka na ushindi wa bao 2-1 ns timu hizo zinakutana leo Jumatano katika mchezo wa marudiano huko Madrid.

ikutane katika fainali. Juve ilishinda 2-1 katika mchezo wa kwanza.

Mabao ya Bayern katika mchezo huo wa jana usiku yalifungwa na Medhi Benatia dakika ya saba, Robert Lewandowski dakika ya 59 na Thomas Muller dakika ya 74, wakati ya Barca mabao yake yote yalifungwa na Neymar dakika ya 15 na 29.

Waziri Korea Kaskazini auawa kwa kusinzia mbele ya rais



SEOUL, Korea ya Kusini
Idara ya Ujasusi ya Korea ya Kusini imesema kuwa Waziri wa Ulinzi wa Korea Kaskazini ameuawa kwa kutokuwa muaminifu kwa kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-un.

Taarifa hiyo iliyotolewa bungeni imesema Hyon Yong-Chol alikutana na mauti yake baada ya kupigwa kwa kombora la kuangusha ndege mbele ya mamia ya maafisa wakuu serikalini mwishoni mwa mwezi uliopita.

Bw.Hyon inadaiwa kuwa alisinzia katika hafla iliyokuwa ikihutubiwa na rais Kim, jambo lililomuudhi sana kiongozi huyo wa kiimla na kuamua kuuawa kwake hadharani.

Hata hivyo ukweli wa ripoti hiyo haujabainika kutokana na usiri wa Serikali ya Korea Kaskazini.
Taarifa zingine zinadai kuwa, Waziri wa Ulinzi wa Korea Kaskazini ameuawa kwa kutokuwa muaminifu kwa kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-un.

Bw.Hyon alipandishwa cheo na kuwa Generali mwaka wa 2010 na kuuawa kwake kunatia shaka udhabiti wa uongozi wa rai Kim Jong -un.

Hyon alipandishwa cheo na kutangazwa kuwa waziri wa usalama wa taifa mwaka uliopita.

Mwandishi wa BBC aliyeko huko Seoul anasema mauaji hayo ya kikatili mbele ya umma ikiwa yatathibitishwa, yanaonyesha athari za uasi dhidi ya Kim Jong-un.

Mapema idara hiyo ya ujasusi ilisema viongozi wakuu katika Serikali ya Korea Kaskazini wamekuwa wakiuawa kila mmoja kwa wiki.

Chang alikamatwa katika mkutano wa hadhara na kupelekwa katika eneo la hadhara alikouawa.

Mara ya mwisho kwa kiongozi huyo wa Korea Kaskazini kuamrisha kuuawa kwa kiongozi mkuu serikalini, ilikuwa mwaka 2013 alipoamuru aliyekuwa msaidizi wake Chang Song auawe
.
Chang alikamatwa katika mkutano wa hadhara na kupelekwa katika eneo la hadhara alikouawa mbele ya umma.

Monday, 11 May 2015

Duniani Kuna Mambo; Paka azaa mbwa nchini China



XUZHOU, China
MZEE mmoja wa Kichina alipigwa na butwaa baada ya kumsaidia paka wake kuzaa na mkubaini kuwa miongoni mwa vitoto vile kimoja wapo kilikuwa ni mbwa.

Mstaafu huyo anayejulikana kwa jina la Jia Weinuan akiwa amejipumzisha nyumbani kwake, alishuhudia paka wake mwenye umri wa miaka mitatu Niu Niu akizaa watoto watano.

Wakati akifanya ukaguzi wa karibu zaidi na kutoa huduma kwa mama paka huyo mzazi, Jia, mwenye umri wa miaka 74, alisema hakuamini macho yake wakati alipobaini miongoni mwa vitoto vile vilivyozaliwa na paka yule ni mbwa.

Alisema: "Nilifikiri kuna vitoto vitano vya mbwa wenye maumbo madogo, lakini badae nilipoangalia kwa ukaribu zaidi nilibaini viko vitano.

"Kwa maisha yangu yote, kamwe sijawahi kuona au kusikia mbwa na paka wakafanya mapenzi.

Jia, ambaye hana mbwa nyumbani kwake, alisema yeye na mkewe hawana maelezo zaidi kuhusu maajabu hayo.

Alisema haamini kama paka wake Niu Niu alikutana na mbwa-kwa sababu sio rahisi kuwapandisha wanyama hao.

Wiki moja kabla ya kuzaa, Niu Niu walimpeleka kwa rafiki yao kwa jili ya uangalizi wa karibu.

Lakini alisema kuwa rafiki yake huyo alimuweka paka huyo na wengine wakiume wawili, na imeendelea kuwaacha bila majibu yoyote.

Jia, kutoka jijini la Xuzhou, kaskazini ya China, alisema: "Hili tuki linachanganya sana.

"Nategemea vyombo vya habari vitaripoti tukio hili na bila shaka tutapata maelezo kamili kutoka kwa wanasayansi."

Friday, 8 May 2015

Pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara 2014-15 lafungwa Jumamosi



Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga.

Na Mwandishi Wetu
TIMU 14 ZA Ligi Kuu Tanzania Bara leo zinashuka kwenye viwanja tofauti viwanja tofauti kumaliza mechi zao za mwisho za kumalizia msimu wa 2014/2015.

Leo ndio itajulikana wazi timu zipi mbili zitakazoshuka daraja baada ya bingwa na mshindi wa pili tayari kujulikana katika kinyanganyiro hicho kilichoanza mwaka jana.

Yanga ndio mabingwa wapya wakati waliokuwa mabingwa Azam FC wameshika nafasi ya pili huku Polisi Morogoro ndio iko kwenye hatari zaidi ya kushuka daraja baada ya kushika mkia katika msimamo wa ligi hiyo yenye timu 14.

Washindi wa Pili Tanzania Bara.
Polisi wenye pointi 25 wanakabiliwa na kibarua kizito dhidi ya Mbeya City, mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Tayari Mbeya City yenye pointi 31 ilishajiondoa kwenye mstari mwekundu wa kushuka, hivyo itakuwa ni kazi kwa timu hiyo ya Morogoro. Iwapoitashinda itafikisha pointi 28, ambazo haziwezi kumvusha popote.

Lakini kama wataruhusu kufungwa pia bado ni lazima washuke daraja. Maafande hao ambao wamekuwa wakishuka na kupanda kila baada ya miaka kadhaa, wameshacheza michezo 25, wameshinda mitano, sare 10 na kupoteza 10.

Timu zinazofuatana nane zikiwamo Stand United, Mgambo Shooting, Ndanda FC na Tanzania Prisons nazo ziko hatarini kama zitashindwa kufanya vizuri katika michezo ya leo kwa vile hufungana kwa pointi sawa 28.

Stand United inaikaribisha Ruvu Shooting yenye pointi 29 kwenye Uwanja wa Kambarage Shinyanga.

Timu hizi mbili zimetofautiana kwa pointi moja, ambazo kama hazitashinda, moja itakuwa hatarini ikiwa nyingine zitashinda.

Stand United wameshacheza michezo 25, wameshinda saba, wana sare saba, wamepoteza michezo 11, hivyo wanahitaji kushinda leo ili kuendelea kubaki kwa msimu mwingine hasa ikizingatiwa wamepanda kwa mara ya kwanza msimu huu.

Mgambo Shooting inamaliza na Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex, Timu hii yenye maskani yake Tanga ina uwezekano wa kushuka kama haitashinda mchezo huo mgumu kwao. 

Simba kutopanda ndege tena baada ya kushika nafasi ya tatu msimu huu.
Tayari wameshacheza michezo 25, wameshinda nane, sare nne na wakifanya mzaha watashuka na kuwapa nafasi African Sports iliyopanda daraja ya kuchukua nafasi yake.

Kwa upande wa Ndanda FC inamaliza mchezo wake na Yanga utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Timu nyingine ni Tanzania Prisons, ambayo inacheza dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Maafande hao wanahitaji kushinda ili kuendelea kubaki na pia Kagera wanahitaji ushindi.

Michezo mingine ni kati ya Simba itakayokwaruzana na JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, huku Coastal Union ikicheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu.

Timu tano zinazofungana kwa pointi 31 ni Coastal Union, JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Mbeya City na Kagera Sugar.

Zote zinahitaji ushindi kujitofautisha na zile ambazo zina pointi 28 ambazo zikishinda zinaweza kufanana na wao.

 Msimamo:




MPWDLGFGA+/-Pts

1
Young Africans25174452173555

2
Azam25139336181848

3
Simba SC25128536181844

4
Mtibwa Sugar2571082424031

5
Mbeya City2571082122-131

6
Kagera Sugar2587102226-431

7
JKT Ruvu2587101923-431

8
Coastal Union2571081924-531

9
Ruvu Shooting2578101628-1229

10
Tanzania Prisons2551371822-428

11
Ndanda2577112029-928

12
Mgambo JKT2584131828-1028

13
Stand United2577112234-1228

14
Polisi Morogoro25510101626-1025