Tuesday 30 August 2016

Alphonce Simbu asaini mkataba wa mwaka mmoja na DSTV ambao utamuwezesha kulipwa sh milioni 1 kila mwezi kama mshahara wake





Taarifa kwa vyombo vya habari

Mwanariadha Alphonce Simbu akisaini mkataba wa mwaka mmoja ambao utamuwezesha kulamba sh. milioni 1 kila mwezi kutoka DSTV kama mshahara ili aelekeze akili katika mazoezi tu. Kulia ni Mkuruenzi Mtendaji wa multchoice-Tanzania, Maharage Chande jijini Dar es Salaam jana.
Tarehe: 30th September, 2016
Utiwaji Saini wa Mkataba na Mwanariadha Alphoce Felix Simbu
Kampuni ya MultiChoice Tanzania imesaini mkataba wa mwaka mmoja na mwanariadha Alphonce Felix Simbu aliyeshiriki mashindano ya Olympic ya Rio 2016 yaliomalizika hivi karibuni huko nchini Brazil na kushika nafasi ya 5 kati ya wanariadha 157 kwenye mbio za Marathon za wanaume. 

Katika Mkataba huu, Kampuni ya Multichoice Tanzania imemzawadia Alphonce Simbu shilling za Kitanzania 1,000,0000 ambazo atalipwa kila mwezi kwa kipindi cha mwaka mmoja lengo likiwa ni kumsadia katika maandalizi yake ya mashindano yajayo ya IAAF WORLD CHAMPIONSHIP yanayotarajiwa kufanyika mjini London Uingereza August 2017. 

Vile vile bwana Alphonce Simbu atapatiwa vifaa maalumu vya kuumuwezesha kufanya mazoezi yake vyema. Vifaa hivi ni kama vile, viatu na nguo za mchezo wa Riadha.

Si hivyo tu bali  Kampuni ya MultiChoice itamtengenezea makala yenye kuonyesha matukio mbalimbili aliyopitia ya Kimichezo na Familia siku za nyuma. Vile vile watarekodi mazoezi atakayo anafanya akiwa katika kambi ya riadha Chuo cha Wakala wa Mistu Fiti kilichopo West Kilimanjaro eneo la Ngarenairobi Wilaya ya Sia Mkoa Kilimanjaro. Makala hii itarushwa kwenye DStv hapo baadae.

Katika Kipindi cha hicho cha mkataba huu Alphonce Felix Simbu atakuwa Balozi wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania ambapo atashiriki katika promosheni mbalimbali kutangaza huduma zake.

Alipokuwa akisaini mkataba huo Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania Maharage Chande mbele ya Rais wa Riadha Tanzania na mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka, mwalimu wa wake Alphonce Nd. Francis John Marcially pamoja na Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Furaha Samalu, alisisitiza kuwa “huu ni mwanzo na kadri mafanikio yanavyo ongezeka Multichoice itakuwa tayari kuwa mstari wa mbele kushirikiana na chama cha riadha Tanzania katika kunyanyua riadha Tanznaia na kurudisha heshma ya taifa kwenye mchezo huo”.


Imetolewa na:
Shumbana Walwa|Social Media Administrator

Telephone: +255222199600      Mobile: +255716578662    

Email: Shumbana.Walwa@tz.multichoice.com     





TTCL ndio wadhamini wakuu Miss High Learning 2016 watoa shilingi milioni 20 kwa shindano hilo




Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Mawasiliano Tanzania (TTCL) imetoa sh. Milioni 20 ili kudhamini shindano la kumsaka Miss Elimu ya Juu litakalofanyika Oktoba 17 katika ukumbi wa Sigara, Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Warembo wa shindano hilo leo Jumanne wametembelea Makao Makuu ya TTCL na kushuhudia shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo inayomilikiwa na Serikali, ambayo imepania kufanya mambo makubwa katika sekta ya mawasiliano hapa nchini.

Akizungumza katika ukumbi wa mikutano wa kampuni hiyo ya mawasiliano muandaa wa shindano hilo, Maya Nkini alisema kuwa jumla ya warembo 25 kutoka vyuo mbalimbali nchini wako kambini kujiandaa na shindano hilo, ambalo linatarajia kuwa na ushindani wa hali ya juu sana.

Nkini aliushukuru uongozi wa kampuni hiyo kwa kudhamini shindano hilo, ambalo sasa litajulikana kama “TTCL Miss Elimu ya Juu 2016”.

Muandaaji wa shindano la Miss Elimu ya Juu nchini,Maya Nkini akizungumza na waandishi wa habari leo.
Aliwataja wadhamini wengi kuwa ni pamoja na Time, Darling, AJ Events, ambao pia ndio waandaaji wa shindano hilo wakati wengine ni Radio E FM, Hussein Pamba Kali na  wengine.

Alisema kuwa washindi watatu wa kwanza watakata tiketi ya kushiriki katika shindano la Miss Tanzania 2016 litakalofanyika baadae mwaka huu.

Manager Customer Care wa TTCL, Aron Msonga.
Naye Maneger, Customer Care wa TTCL Aron Msonga aliwaelezea warembo hao kuhusu shughuli na mikakati ya mizima ya kampuni hiyo kuhakikisha inarejea kwa kishindo katika sekta ya mawasiliano nchini na tayarri imefanya mambo kibao.

Mmoja wa waratibu wa Miss Tanzania, Mr. Makoye akizunumza leo wakati warembo wa Miss Vyuo vya Elimu ya Juu walipotembelea TTCL. Wengine pichani ni muandaaji wa shindano hilo, Maya Nkini na Junior Makoye.
Mmoja wa waratibu wa Miss Tanzania Makoye alisema kuwa wamepokea kwa mikono miwili udhamini huo wa TTCL kwa Miss Elimu ya Juu na kuwaambia kuwa milango iko wazi kwa kampuni hiyo kuingia katika Miss Tanzania.
Warembo wakigawiwa kadi za Simu za TTCL na Manager Cutomer Care, Aron Msonga.
 Alisema kuwa TTCL imeonesha mfano kwa makampuni mengine kwa kudhamini shindano hilo na wao (Miss Tanzania) hawatawaangusha.

Warembo wote pamoja na viongozi wao waligawiwa line za simu za 4G zenye muda wa maongezi.








Meneja msaidizi wa TTCL mkoa  Kituo cha Dar es Salaam, Augustino Mwakyembe akiwapa maelezo warembo wa Miss Vyuo vya Elimu ya Juu nchini walipotembelea ofisi za kampuni hiyo ya mawasiliano mapema leo Jumanne.
 
Makoye akiteta na muandaaji wa Miss Vyuo vya Elimu ya Juu, Maya Nkini.

DSTV ilivyoandaa chakula cha usiku na kuwapa zawadi wachezaji wa Tanzania walioshiriki Olimpiki ya Rio 2016

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akipokea bendera ya taifa kutoka kwa nahodha wa timu ya Tanzania iliyoshiriki Michezo ya 31 ya Olimpiki iliyofanyika Rio, Brazil, Alphonce Felix Simbu katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi akizungumza na Meneja Masoko wa MultiChoice- Tanzania, Furaha Samalu kabla ya kuanza kwa hafla ya kuwapongeza wachezaji walioshiriki Michezo ya Olimpiki ya rio 2016 katika hoteli ya Serena.
Baadhi ya wadau wa michezo waliohudhuria tafrija hiyo.


Rais wa TOC, Gulam Rashid akizungumza katika hafla hiyo.
Aliyekuwa Mkuu wa Msafara wa timu ya Tanzania iliyoshiriki Michezo ya Olimpiki ya Rio 2016, Suleiman Jabir.

Waziri sa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akimkabidhi tuzo mwanariadha Alphonce Felix Simbu baada ya kumaliza wa tano katika Michezo ya Olimpiki iliyomalizika hivi karibuni Rio, Brazil.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akimkabidhi zawadi mwanariadha Fabian Joseph aliyeshiriki Michezo ya 31 ya Olimpiki.

Kocha wa timu ya Tanzania ya riadha iliyoshiriki Michezo ya Olimpiki, Francis John akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
Meneja Masoko wa Multchoice-Tanzania, Furaha Samalu akipokea cheti cha shukrani kwa kazi nzuri iliyofanywa na kampuni yake kutoka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye kilichotolewa na TOC. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice-Tanzania Maharage Chande.

Muogeleaji Hilal Hemed Hilal akipewa zawadi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice-Tanzania, Maharage Chande.
 
 
Wachezaji walioshiriki Olimpiki 2016, viongozi wa michezo na wadau wengine wote walipata mlo wa usiku ulioandaliwa na Multchoice-Tanzania katika hoteli ya Serena.