Tuesday 21 June 2016

RISALA YA MGENI RASMI (FILBERT BAYI) WAKATI WA KUFUNGA MAFUNZO YA WALIMU MCHEZO WA “SAILING”, DAR ES SALAAM, TANZANIA 21/06/2016.

Makocha wa mchezo wa mbio za mashua wakiwa katika mafunzo ya kufundisha mchezo huo jana kwenye Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti, Chama cha Sailing Tanzania (TSAA)

Makamu Mwenyekiti Chama cha Sailing Tanzania (TSAA)

Waratibu wa Mafunzo, TOC/TSAA

Mkufunzi wa Kimataifa,

Washiriki wa Mafunzo,

Waandishi wa Vyombo vya Habari

Wageni waalikwa,

Mabibi na Mabwana.
Kwanza napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru TSAA kwa jitihada walizofanya kupata mafunzo haya ya kwanza ya aina yake.

Pamoja na kwamba mchezo huu ni mpya hapa Tanzania mtakubaliana nami kwamba siyo mpya kwa Watanzania kwani mara nyingi tumeona wavuvi wakienda kuvua samaki wakiweka matanga kwenye vyombo vyao vya kusafiria kwenda baharini.
Wakufunzi na viongozi wa Chama cha Mbio za Mashua Tanzania na wale wa TOC wakiwa katika picha ya pamoja leo.
Nimefahamishwa matanga katika vyombo hivyo ni kwa ajili ya kutafuta mwelekeo na kasi ya chombo.

Nimefahamishwa vile vile kwamba siku 11 zilizopita mafunzo haya yalipoanza rasmi pale DYC yalihudhuriwa na washiriki 12 kutoka  Dar Es Salaam, Zanzibar, Pwani na Tanga, Washiriki hao ndio wanaomaliza leo kwa sura ya furaha.
Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akipokea cheti kutoka kwa mwenyekiti wa Chama cha Mbio za Mashua Tanzania (TSAA), Al Bushi jijini Dar es Salaam leo.
Nikiwa kama mtendaji mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, idadi ya washiriki 12 ni ndogo sana nikilinganisha na mafunzo ya aina hii kwa walimu wa michezo mingine tuliyowahi kuandaa.

Pamoja na uchache wenu ni matumaini yangu kuwa mmepata dozi nzuri ya taaluma na mbinu mbalimbali ya kufundisha mchezo huu. TOC inauthamini sana  mchezo wa Sailing pamoja na kuwa mpya hapa nchini na ukitawaliwa zaidi na vijana wa wageni hasa panapotokea mashindano ya Kimataifa.
Mkufunzi wa kimataifa wa mchezo wa mbio za ngalawa, Rob Holden (kushoto) akizungumza na baadhi ya waandizhi wa habari katika boti wakati wa mafunzo ya walimu wa mchezo huo yaliyofanyika kwenye bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam leo Jumanne.
Kwa kuwa mchezo huu ni mpya, kwa kweli unahitaji kuenezwa nchi nzima pale miundo mbinu inaporuhusu (bahari na ma-ziwa lakes) kwani TOC inaamini kuwa mchezo huu ni kati ya michezo ambayo  inapendwa na itazidi kupendwa na Watanzania pamoja na changamoto ya maeneo rasmi ya TSAA kufanyia mazoezi na mashindano badala ya kutegemea vilabu binafsi ambavyo wakati mwingine vinakuwa na masharti magumu.

Upatikanaji wa vifaa (boats) nimefahamishwa ni changamoto kubwa kwa viongozi wa TSAA kwani hata vikipatikana bado ni ghali ambapo watanzania hawawezi kuvimudu.
Ninawasihi na kuwashauri viongozi wa TSAA kuwa karibu na Shirikisho la Kimataifa cha mchezo huu (ISAF) na Mtaalamu Rob Holden ambaye ndiye mhusika mkuu wa maendeleo ya mchezo wa Sailing katika bara letu la Afrika.

Ninaamini mmefaidika na elimu mliopata kutoka kwa mtaalamu wa Kimataifa Rob Holden ambaye amekuwa wakiwaandalia masomo yote ya nadharia na vitendo kwa muda wote wa siku 11. Ni mategemeo yangu elimu mliyopata itawasaidia kuandaa timu katika vilabu vyenu sambamba na kuwa wabunifu wa kutengeneza au kutumia vifaa (boats) za kawaida bila kutegemea tu za kisasa ambazo hatuwezi kumudu kuzinunua.
Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akisoma rizala yake wakati wa ufungaji wa mafunzo ya ufundishaji mbio za ngalawa. Kushoto ni mkufunzi wa mafunzo hayo, Rob Holden na mratibu wa mchezo huo hapa nchini, Nelly Coelho leo.
Ni ukweli usiopingika kwamba  mmejiongezea elimu ya kufundisha mchezo huu wa saiing kwa kiwango cha hali ya juu, mkilinganisha uwezo na elimu mliyokuwa nayo awali.

Wakati wote TOC imekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza taaluma ya ufundishaji na mbinu za kisasa za kuboresha uwezo wa walimu na wachezaji wetu, ili waweze kufikia viwango vinavyotakiwa na timu zetu zinaposhindana katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa.

Ningependa kusisitizia sana kwenu walimu mnaomaliza mafunzo haya, kwamba mhakikishe mchezo huu wa sailing  unapiga hatua kufikia kiwango ambacho wenzetu kama Afrika ya Kusini, Tunisia, Algeria, Morocco wanayo.

Ningependa kuwasihi walimu mnaomaliza mafunzo haya leo kuupeleka mchezo huu kwa wavuvi ambao nina uhakika mkiwashirikisha na kuandaa mashindano ya mara kwa mara kwa kushirikiana na TSAA mtapata washiriki wengi ambao inawezekana kabisa kuna siku watakuwa wawakilishi wazuri katika michezo ya Kimataifa na kuachana na zana kwamba washiriki wengi wa mchezo huu hapa Tanzania ni wageni kutoka nje ya nchi.
Mkufunzi wa mafunzo ya ufundishaji mchezo wa mbio za mashua, Rob Holden akimkabidhi Katibu wa TOC, Filbert Bayi zawadi kutoka Chama cha Kimataifa cha mchezo huo.

Ni matumaini yangu Wizara inayoshughulikia michezo hapa Tanzania imetayarisha mipango kwa kushirikiana na vyama vya michezo kuendeleza michezo ya aina yote ikiwa pamoja na Sailing.  

Kilio kikubwa cha vyama/mashirikisho ya michezo ikiwa pamoja na TSAA kwa sasa ni eneo maeneo ya mazoezi na mashindano. Ili kuondokana na masharti magumu wanayowekewa na klabu kwenye maeneo hayo. hususan sailing, ninaomba Serikali kutenga maeneo ya michezo hususani kwa TSAA kwani pamoja na ISAF kuweka nguvu nyingi katika kutoa elimu kwa walimu wetu bado TSAA inahitaji kumiliki eneo lake la bahari kwa ajili ya mafunzo, mazoezi na mashindano.

Katibu wa TOC, Filbert Bayi (kulia) akimkabidhi cheti makamu mwenyekiti wa Chama cha Mashua Tanzania (TSAA), Philimo Nasseri.
Mchezo huu bado haujatangazwa vizuri, na wanaoweza kuutangaza zaidi ni waandishi wa habari ambao tuko nao hapa leo, tofauti na baadhi yao  kukataliwa kufanya coverage hivi karibuni baada ya kuombwa na TSAA.

Linalotakiwa hivi sasa ndugu zangu walimu ni kutumia mafunzo haya katika kuendeleza mchezo wa sailing nchini.

Napenda nichukue nafasi hii kumpongeza na kumshukuru mtaalamu wa Kimatafa Rob Holden kwa jitihada zake za kutoa mafunzo haya kwa ufanisi mkubwa, kwa sasa tuna walimu ambao watatufundishia wanamichezo wetu wazalendo, lakini bila vifaa mafunzo haya hayatakuwa na tija kwa TSAA.

Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitawashukuru  waratibu wa TOC.TSAA kwa kufanikisha mafunzo haya, Olimpiki Solidariti (OS) kwa kufadhili mafunzo haya, Shirikisho la Kimataifa la Sailing (ISAF) kwa kumteua  Mkufunzi niliyemtaja hapo juu kuendesha mafunzo, TOC na TSAA kwa maandalizi mazuri.

Mwisho kabisa nawashukuru wale wote waliohusika katika kufanikisha mafunzo haya kwa namna moja au nyingine.

Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akonesha nembo ya Shirikisho la Kimataifa la Mbio za Mashua (ISAF) baada ya kukabidhiwa na mkufunzi wa mafunzo ya makocha wa mchezo huo leo katika hoteli ya Slipway.
Kwa haya machache sasa natamka kwamba mafunzo yenu ya ualimu wa mchezo wa Sailing ninayafunga rasmi.

Ahsanteni kwa kunisikiliza!

RISALA YA MGENI RASMI (FILBERT BAYI) WAKATI WA KUFUNGA MAFUNZO YA WALIMU MCHEZO WA “SAILING”, DAR ES SALAAM, TANZANIA 21/06/2016

 Mwenyekiti, Chama cha Sailing Tanzania (TSAA)

Makamu Mwenyekiti Chama cha Sailing Tanzania (TSAA)

Waratibu wa Mafunzo, TOC/TSAA

Mkufunzi wa Kimataifa,

Washiriki wa Mafunzo,

Waandishi wa Vyombo vya Habari

Wageni waalikwa,

Mabibi na Mabwana.

Kwanza napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru TSAA kwa jitihada walizofanya kupata mafunzo haya ya kwanza ya aina yake.

Pamoja na kwamba mchezo huu ni mpya hapa Tanzania mtakubaliana nami kwamba siyo mpya kwa Watanzania kwani mara nyingi tumeona wavuvi wakienda kuvua samaki wakiweka matanga kwenye vyombo vyao vya kusafiria kwenda baharini.

Nimefahamishwa matanga katika vyombo hivyo ni kwa ajili ya kutafuta mwelekeo na kasi ya chombo.

Nimefahamishwa vile vile kwamba siku 11 zilizopita mafunzo haya yalipoanza rasmi pale DYC yalihudhuriwa na washiriki 12 kutoka  Dar Es Salaam, Zanzibar, Pwani na Tanga, Washiriki hao ndio wanaomaliza leo kwa sura ya furaha.

Nikiwa kama mtendaji mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, idadi ya washiriki 12 ni ndogo sana nikilinganisha na mafunzo ya aina hii kwa walimu wa michezo mingine tuliyowahi kuandaa.

Pamoja na uchache wenu ni matumaini yangu kuwa mmepata dozi nzuri ya taaluma na mbinu mbalimbali ya kufundisha mchezo huu. TOC inauthamini sana  mchezo wa Sailing pamoja na kuwa mpya hapa nchini na ukitawaliwa zaidi na vijana wa wageni hasa panapotokea mashindano ya Kimataifa.

Kwa kuwa mchezo huu ni mpya, kwa kweli unahitaji kuenezwa nchi nzima pale miundo mbinu inaporuhusu (bahari na ma-ziwa lakes) kwani TOC inaamini kuwa mchezo huu ni kati ya michezo ambayo  inapendwa na itazidi kupendwa na Watanzania pamoja na changamoto ya maeneo rasmi ya TSAA kufanyia mazoezi na mashindano badala ya kutegemea vilabu binafsi ambavyo wakati mwingine vinakuwa na masharti magumu.

Upatikanaji wa vifaa (boats) nimefahamishwa ni changamoto kubwa kwa viongozi wa TSAA kwani hata vikipatikana bado ni ghali ambapo watanzania hawawezi kuvimudu.

Ninawasihi na kuwashauri viongozi wa TSAA kuwa karibu na Shirikisho la Kimataifa cha mchezo huu (ISAF) na Mtaalamu Rob Holden ambaye ndiye mhusika mkuu wa maendeleo ya mchezo wa Sailing katika bara letu la Afrika.

Ninaamini mmefaidika na elimu mliopata kutoka kwa mtaalamu wa Kimataifa Rob Holden ambaye amekuwa wakiwaandalia masomo yote ya nadharia na vitendo kwa muda wote wa siku 11. Ni mategemeo yangu elimu mliyopata itawasaidia kuandaa timu katika vilabu vyenu sambamba na kuwa wabunifu wa kutengeneza au kutumia vifaa (boats) za kawaida bila kutegemea tu za kisasa ambazo hatuwezi kumudu kuzinunua.

Ni ukweli usiopingika kwamba  mmejiongezea elimu ya kufundisha mchezo huu wa saiing kwa kiwango cha hali ya juu, mkilinganisha uwezo na elimu mliyokuwa nayo awali.

Wakati wote TOC imekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza taaluma ya ufundishaji na mbinu za kisasa za kuboresha uwezo wa walimu na wachezaji wetu, ili waweze kufikia viwango vinavyotakiwa na timu zetu zinaposhindana katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa.

Ningependa kusisitizia sana kwenu walimu mnaomaliza mafunzo haya, kwamba mhakikishe mchezo huu wa sailing  unapiga hatua kufikia kiwango ambacho wenzetu kama Afrika ya Kusini, Tunisia, Algeria, Morocco wanayo.

Ningependa kuwasihi walimu mnaomaliza mafunzo haya leo kuupeleka mchezo huu kwa wavuvi ambao nina uhakika mkiwashirikisha na kuandaa mashindano ya mara kwa mara kwa kushirikiana na TSAA mtapata washiriki wengi ambao inawezekana kabisa kuna siku watakuwa wawakilishi wazuri katika michezo ya Kimataifa na kuachana na zana kwamba washiriki wengi wa mchezo huu hapa Tanzania ni wageni kutoka nje ya nchi.

Ni matumaini yangu Wizara inayoshughulikia michezo hapa Tanzania imetayarisha mipango kwa kushirikiana na vyama vya michezo kuendeleza michezo ya aina yote ikiwa pamoja na Sailing.  Kilio kikubwa cha vyama/mashirikisho ya michezo ikiwa pamoja na TSAA kwa sasa ni eneo maeneo ya mazoezi na mashindano. Ili kuondokana na masharti magumu wanayowekewa na vilabu vyenye maeneo hayo. hususan sailing, ninaomba Serikali kutenga maeneo ya michezo hususani kwa TSAA kwani pamoja na ISAF kuweka nguvu nyingi katika kutoa elimu kwa walimu wetu bado TSAA inahitaji kumiliki eneo lake la bahari kwa ajili ya mafunzo, mazoezi na mashindano.

Mchezo huu bado haujatangazwa vizuri, na wanaoweza kuutangaza zaidi ni waandishi wa habari ambao tuko nao hapa leo, tofauti na baadhi yao  kukataliwa kufanya coverage hivi karibuni baada ya kuombwa na TSAA.

Linalotakiwa hivi sasa ndugu zangu walimu ni kutumia mafunzo haya katika kuendeleza mchezo wa sailing nchini.

Napenda nichukue nafasi hii kumpongeza na kumshukuru mtaalamu wa Kimatafa Rob Holden kwa jitihada zake za kutoa mafunzo haya kwa ufanisi mkubwa, kwa sasa tuna walimu ambao watatufundishia wanamichezo wetu wazalendo, lakini bila vifaa mafunzo haya hayatakuwa na tija kwa TSAA.

Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitawashukuru  waratibu wa TOC.TSAA kwa kufanikisha mafunzo haya, Olimpiki Solidariti (OS) kwa kufadhili mafunzo haya, Shirikisho la Kimataifa la Sailing (ISAF) kwa kumteua  Mkufunzi niliyemtaja hapo juu kuendesha mafunzo, TOC na TSAA kwa maandalizi mazuri.

Mwisho kabisa nawashukuru wale wote waliohusika katika kufanikisha mafunzo haya kwa namna moja au nyingine.

Kwa haya machache sasa natamka kwamba mafunzo yenu ya ualimu wa mchezo wa Sailing ninayafunga rasmi.

Ahsanteni kwa kunisikiliza.

Sunday 19 June 2016

Taarifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016

TAARIFA YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, 2016

MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA), INAWAKARIBISHA WANANCHI NA WATUMISHI WA UMMA KUJA KUJUA NA KUJIFUNZA MASUALA MBALIMBALI YANAYOHUSU VIWANJA VYA NDEGE KUANZIA TAREHE 16 HADI 23 JUNI 2016.

ENEO: MAKAO MAKUU YA TAA, KARIBU NA KIWANJA CHA ZAMANI CHA NDEGE, BARABARA YA NYERERE.

MUDA: HUDUMA ZITATOLEWA KUANZIA SAA 01:30 ASUBUHI HADI SAA 10:30 JIONI.

KAULIMBIU- “UONGOZI WA UMMA UKUAJI JUMUISHI KUELEKEA KATIKA AFRIKA TUNAYOITAKA”.

*****NYOTEMNAKARIBISHwA***

IMETOLEWA NA KITENGO CHA SHERIA NA MAHUSIANO TAA,
Kny: MKURUGENZI MKUU
17/06/2016